Wanawake wengine hawajui kusamehe

Wanawake wengine hawajui kusamehe

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
19,229
Reaction score
17,659
Kweli ukikosea step kwenye kuoa ni regret kubwa.Mshikaji wangu Rob alifunga ndoa yake Mwaka 2007, Alimwoa mdada wa kisukuma beautiful in body structure and face tall and attractive mshikaji alimpenda sana wife wake and good thing alikuwa anampa kila alichotaka.

Mwaka mmoja baada ya ndoa yao walifanikiwa kupata Mtoto. Kuna kamgogoro kaliibuka, it was a normal conflict as hata plates zina collide.Hii conflict ilimsababishia dada kurudi kwao bahati nzuri Rob alipenda kujishusha akaenda kwa wakwe yakaisha.

Wakapata mtoto wa pili Rob akawa kwenye harakati za kufanya ujenzi wake kule Bushushu it was a good step in life Kamgogoro kengine kakaibuka kakali kuliko kale ka kwanza as usual mdada akasepa.

More than a year in separation, Rob juzi kati hapa akadhamiria kabisa kurudiana na wife wake walee watoto wao wawili, akaamua kwenda hadi kwa mchungaji.

Wife akaitwa Rob akamwomba sana wife wake warudiane.Akaomba msamaha mkubwa tena ule wakupiga Magoti mbele ya Pastor wife kachomoa, akagoma kabisa,inasemekana kuna deal alishazianza huko Dar.. Na kwa msisitizo akaamua hadi kwenda kuchukua alivyokuwa amebakiza kwa Rob.

Hii kitu ilimuumiza sana Rob compare na nguvu aliyotumia ku apologies and what he got in returns.Alipata shida moyoni mwake, alihuzunika sana watoto wake kuwa mbali na mama yao, na ujenzi ulikwishakamilika.Ilichukua kama siku 2 hivi akili kumrudi.

Last thursday Rob alitoka walau kukutana na baadhi ya wadau kabla yakurejea kwenye deal zake.
He spoke few words on what happen and then kapiga beer zake mbili.Around 4pm akawasha gari yake kuelekea Kahama.Aisee Rob hakufika Kahama salama, maeneo ya Usanda few Kilometers to Tinde.

Akapata ajali, bad accident kwenye gari walikuwa wawili,yeye na fundi mmoja.Fundi alifariki palepale,Rob alikimbizwa hadi Hospital ya Mkoa Shinyanga government he passed away.

Mke wake nae ndiyo alikuwa anarudi Dar after a completely separation.
Alivyopata habari za kifo cha Rob, akageuza safari back to Shinyanga, akapata ajali maeneo ya Igunga bahati nzuri yeye hakuumia sana, alipelekwa hospital na akaruhusiwa na kashajiung

Hii kitu inaumiza sana msamehe mtu kabla usiku haujaingia hujui what is next.Rob's wife hakusamehe and Rob is not alive anymore atazikwa kesho.Bushushu. R.I.P bro & friend.
 
R.I.P maskini . Watoto do washakosa baba hivo
 
RIP Rob.Katika ndoa au mahusiano yakawaida msamaha ni kitu kizuri sana.Asante kwa kutukumbusha kuwa tuwe tunasamehe before haijawa too late maana kama Mungu anatusamehe na midhambi yetu lukuki why sisi tusisamehane?Na tumuombe Mungu sana atuongoze katika hizi chaguzi zetu maana ukikosea tu kidogo lazima ujute maisha yako yote.
 
Sijui huyo mama ataishije na atakuja kuwaambia nini watoto wakikua, marriage is not always a bed of roses, inahitaji kuvumiliana hasa kama kuna watoto na kusamehana kama makosa hayana madhara kimwili, kama hauko tayari kwa hayo bora tu ukae single.
 
R.I.P jamani hizi ndoa zenu hizi mweh mnapeana stres tu kila kukicha furaha zenu za msimu why?pole watoto wa Rob
 
Very sad..na touching kisa!! Mungu ampumzishe kw amani... Pole kwa wafiwa. Watoto Mungu atawakuza kivyake.
 
Mhh!! Maskini jamani inaumiza sana, watoto washakosa baba, katika vitu namshukuru Mungu kaniwezesha ni Kusamehe kama Biblia inavyosema jua lisizame una uchungu moyoni hilo nazingatia sana siku haipiti na likiwa zito kabisa kabisa kiasi kwamba sina jinsi siku 3 mwisho baada ya hapo ni amani amani hata kama sijaombwa msamaha natangaza mwenyewe na maisha yanasonga mbele .
 
Jambo moja nilijualo katika maisha:-
Kusamehe na Kusamehewa kunawaweka watu HURU.
 
Kuna binadamu wengine wana sio wana roho mbaya tuu ila hawajui kupendwa wala kupenda,yani wapo wapo tuu kazi yao kuangalia life ya watu wengine wanavyo ishi hawajali mtu mwengine anawapenda kiasi gani,atakuja kuja kukumbulka pale atakapo pata mwangine na akianza kumsugua roho ndio atajua thamani ya yule aliokua akimfikicha roho,nawakati huo anakumbuka shuka kushakucha...
 
Duh.... mkewe ataumia sana

Ataweweseka maisha yake yote yaliyosalia, mikosi itamuandama mpaka kwenye kucha, alikuwa shujaa kwa wanae lakini sasa ni sawa na jambazi.

Simpendi na afadhali simfahamu
 
Back
Top Bottom