Wanawake watawala Dunia soon

UPOPO

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
3,697
Reaction score
6,099
Niko naangalia CNN nikaanza kutafakari mambo mengi kimoja nikavutiwa na uchaguzi wa Marekani huku nikifuatilia kwa makini mijadala ya uraisi wa Marekani.

Lakini navutiwa na mwenendo wa sasa ambapo soon wanawake wanakuja juu kwa kasi kutawala mataifa makubwa duniani.Hilary Clinton akishinda Uraisi wa Marekani inamaana ,Uingereza kwa sasa inatawaliwa na wamama wawili(Malkia na waziri mkuu aliyechukua nafasi ya waziri mkuu aliyejiuzulu).

Ujerumani inaongozwa na mwanamke.Sasa naona wanawake wanakuja juu kwa kasi ,kwa miongo mingine miwili nahisi wanaume watakuwa spices nyingine kabisa.

Sasa swali langu ni hili,Je wanaume wapi wamebaki?na wanafanya nini.Pili,je walipoambiwa watakuwa vichwa ,jewamekosea wapi au sisi wazazi au serekali tumefanya nini kwa malezi ya watoto wetu wa kiume.

Kingine tunashuudia ndoa za wanaume kwa wanaume(sikatai za wanawake kwa wanawake hazipo)ila hizi za wanaume zimeshamiri.Je tumekosa wapi?
 
Hakuna namna acha watawale.
Wana sapoti kubwa si waona siku hizi watu wanajipeleka wenyenye kubadili jinsia
 
Kimsingi hillary clinton hana Ushawishi mkubwa yeye kama yeye buli watu wanaamini nasaha za clinton na ukaribu wake na watu wengine kama obama utamsaidia kuiongoza nchi otherwise lile ni pazia tu hata chakusema anapangiwa na ukichanganya na kauzoefu alikonalo mambo ndo yanaenda
 
Ila kiukweli wanawake wanakuja juu sana, tazama hata Taasisi mbali mbali, vyama kama vikoba, semina za ujasilia mali na mambo mengi. Wanatafuta elimu kwa udi na uvumba ili kujikwamua na kukwamua familia zao kiuchumi.

Tofauti na sisi wanaume, tunashabikia mipira kuliko wanao faidika na hiyo mipira.. tumejawa na hanasa za kipumbuvu mpaka tunafikia kupenda dressing table kuliko wanawake. Simu zetu zimejaa magroup ya watsap ya hovyo hovyo, picha zote ni za kingono ngono na kuwadhalilisha mama zetu na dada zetu pamoja na wake zetu.

Muda huu tuna wadhalilisha. je umeshawah kujiuliza gharama gani tutakayo ipata kwa kuwa dhalilisha uko?

Ipo siku mwanamke ataingia na mwanaume kwenye ndoa kwaajiri kupigwa deki tu, na mwanaume ukatafuta aina nyingine ya kumaliza haja zako.

Kama sio sisi basi ni kwa watoto wetu wa kiume. Nafikiri hatuja chelewa sana. Ni muda wa kumjenga mtoto wako kama baba mtalajiwa. Ajue majukumu ya baba ni yapi? Na nini mtoto anastahili afanye ili kuwa na idea ya utafutaji kama mwanaume.

Nakumbuka zamani ili kuwa ni jambo rahisi kusikia fulani kaaga kwao kaenda sehemu fulani kutafuta. Ni wakati wetu kuwa katika umoja wenye nguvu mpya ili kuwajenga watoto wetu, kuwa wababa wa kesho.

Haiwezekani kila mtoto sasa hivi msanii, kila mtoto ana uhuru kupita uhuru wa Nchi. Nchi ina misingi yake, hivyo sio mbaya na sisi kama mababa kujenga familia yenye misingi imara ya kukua katika mazingira ya kiuchumi kama ndugu zetu wa Asia hapa nchini.

Mila tamuduni za wazazi wetu walizo tuachia ni za kuenziwa na za kuunga mkono hasa mila za kifamilia. Haiwezekani umlee mtoto wako kiasi kwamba anajua matunda yanaoteshwa kwenye frige!!

Kuna muda nilimwambia mke wangu, natamani sana kuanzisha DADIES EVENT, Lakini bahati mbaya nilimwambia wakati nimekula mmea wetu pendwa, Hakunijibu nikajua anahisi mmea ndio unaongea. Kwenye hii DADIES EVENT nilitaka tuwe na watu maalum wenye kujua mila na desturi za makabila, pili kukabiliana na ugonjwa wa wallet kuwa nyeupe, tatu changamoto za kifamilia, nne jinsi ya kuwapa malezi watoto na kuendeleza vipaji vyao na mwisho kuenjoy na Baber Q hisiyo kuwa na kilevi.

Umoja wetu kina baba ndio ushindi, na ushindi wetu ni ushindi wa familia zetu pamoja Taifa kwa ujumla.


NB Si mmesikia ukiwa huendi kwenye nyumba za ibada hawakuziki? Ni wakati wetu tusio na dini kuanzisha hiki kitu DADIES EVENT.

By

Kanyela mumo
 
Kwa kweli Hilary amejaribu sana last lime wakati wa Obama alikuwa wapili kwenye chama chake na hakukata tamaa.

kule hawana ujinga huu wa huku kijani kule haipo mama yulee white house ataiongoza dunia
 
Apa naona kiladalili ya Putin kutawala ulimwengu kwa urahisi kabisa maana hakuna atakaye m challenge
 
Dada yangu (Mpendwa), usiangalie tu hao ambao walikuwa nominated na wakaukwaa uongozi wa juu tu.

Angalia Majority, yaani MP's wa nchi zote hizo huoni karibu wote ni wanaume?

Pia Jeshini, kuanzia macaptains mpaka mabregadia na Commandos ni Wanaume.

Angalia globally, marais wangapi ni Wanaume na wangapi ni wanawake?

Halafu Mwanaume ni "KICHWA" cha familia katika ndoa takatifu. According to the Bible na si vinginevyo.
 
Hata nikiwaona wanavyolia lia humu naishia kusikitika tu,siku hizi wimbo wa haki sawa wao ndio waimbishaji, tena wanadai haki sawa kwenye kuchambana!!! Eeeh Mungu tusaidie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…