Wanawake / Wanaume ambao ukishiriki nao tendo la ndoa 'mambo yako yanaenda vizuri zaidi'

JBourne59

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
941
8,547
Wanawake / Wanaume ambao ukishiriki nao tendo la ndoa ‘mambo yako yanaenda vizuri zaidi’
------------------

Habari wana JF?

Najuwa kuna uzi unaofana na huu, lakini kwa heshima na taadhima nawaomba MODs wasiunganishe uzi huu huko.

Kizazi hiki kipya cha JF tungependa kupata uzoefu wao kwa mada tajwa na Wahenga wenzangu uzoefu wenu bado unahitajika sana kuleta uelewa kwa vijana wetu.

Kwamba:-
Kuna baadhi ya wanawake ‘ukilala nao’ mambo yako yataenda vizuri zaidi, yaani utapata kinachoitwa ’kismati’ na kinyume chake wapo ambao ukishiriki nao mambo yako yanaharibika, unapata kitu kinachoitwa ‘nuksi’.

Vivyohivyo kwa wanaume na inasemekana, kwa wanaume imeenda mbali zaidi kwamba ‘wa hivyo’ hata ukipeana naye mkono tu kwa salamu ‘umekwisha’ hususani ‘wanaoingiliwa’ basi siku yako inakuwa mbaya na mambo ‘hayaendi’

Inasemekana wanawake / wanaume hao kuna majina wamepewa lakini hutofautiana kila mkoa ama kabila, na inasemekana pia kuna baadhi ya dalili / sifa ukiwanazo basi unaweza kuwa mmoja wa wenye nuksi ama ngekewa.

Hebu tupeane uzoefu kwa mjadala wenye staha.

(Picha hapo chini hazihusiani na maelezo hapo juu, picha ni kwa hisani ya google)

Jbourne59
View attachment 2014136View attachment 2014137
 
Tupige kazi wakuu maana kama kuna wanawake wenye nuksi na wanaume wenye nuksi, sasa nani atawajua???

Maana ili ujue lazima ukwichikwichi nae kwanza, sasa hapo kuna wale ambao hufuata misingi ya dini kwamba Haonji chakula mpaka kipigiwe Dua au kuombewa, Huyu naye atamuacha mke wake au mumewe baada ya kuona mambo hayaendi???

Ugumu wa Maisha usifanye tusingizie mambo mengi bn, maana fundi mbovu hulaumu vyombo vyake.

Ukiitafuta pesa itakuja, ila ukibweteka hata kama una mke mwenye neema pesa haikufuati Ng'o.
 
Jamani mgawo wa Umeme umeleta na mgawo wa maji tena?

Screenshot_20211117-163247_WhatsApp.jpg
 
Wanawake / Wanaume ambao ukishiriki nao tendo la ndoa ‘mambo yako yanaenda vizuri zaidi’
------------------

Habari wana JF?

Najuwa kuna uzi unaofana na huu, lakini kwa heshima na taadhima nawaomba MODs wasiunganishe uzi huu huko.
Hii ni kweli kabisa. Ingawa ina work kwa mfumo tofauti tofauti, kuna wanaume haijalishi mwanamke gani, ila mafanikio yake yanapata nguvu pindi anapokuwa na mwanamke ( mmoja ). Hii binafsi ina fanya kazi kwangu, na mkizinguana haichukui round unaanza ona picha picha zenye chenga mbele
 
Wanawake / Wanaume ambao ukishiriki nao tendo la ndoa ‘mambo yako yanaenda vizuri zaidi’
------------------

Habari wana JF?

Najuwa kuna uzi unaofana na huu, lakini kwa heshima na taadhima nawaomba MODs wasiunganishe uzi huu huko.

Kizazi hiki kipya cha JF tungependa kupata uzoefu wao kwa mada tajwa na Wahenga wenzangu uzoefu wenu bado unahitajika sana kuleta uelewa kwa vijana wetu.

Kwamba:-
Kuna baadhi ya wanawake ‘ukilala nao’ mambo yako yataenda vizuri zaidi, yaani utapata kinachoitwa ’kismati’ na kinyume chake wapo ambao ukishiriki nao mambo yako yanaharibika, unapata kitu kinachoitwa ‘nuksi’.

Vivyohivyo kwa wanaume na inasemekana, kwa wanaume imeenda mbali zaidi kwamba ‘wa hivyo’ hata ukipeana naye mkono tu kwa salamu ‘umekwisha’ hususani ‘wanaoingiliwa’ basi siku yako inakuwa mbaya na mambo ‘hayaendi’

Inasemekana wanawake / wanaume hao kuna majina wamepewa lakini hutofautiana kila mkoa ama kabila, na inasemekana pia kuna baadhi ya dalili / sifa ukiwanazo basi unaweza kuwa mmoja wa wenye nuksi ama ngekewa.

Hebu tupeane uzoefu kwa mjadala wenye staha.

(Picha hapo chini hazihusiani na maelezo hapo juu, picha ni kwa hisani ya google)

Jbourne59
View attachment 2014136View attachment 2014137
Nafurahi mkuu umeanzisha uzi nakuchokoza hii mada,
Binafsi nimoja kati ya mambo nnayo jiuliza zaidi na nitasubiri kupata ushahidi shirikishi na kutoa tongotongo,

Elimu haina mipaka..🙏
 
Kama una amini Mungu Muumba mbingu na nchi na vilivyomo yupo, basi lazima uamini kuwa Ibilisi yupo na nguvu za giza zipo, kwa maana nguvu za giza ni katika elimu iliyozuiliwa.

Kwa wale wasioamini uwepo wa Mwenyezi Mungu nao ninaheshimu Imani yao.

Napenda watu wajadili bila mihemko, tupeane uzoefu, kwa umri kama huu niliokuwa nao siwezi kukurupuka bila sababu ya msingi kuleta mada hii, lakini kama unaona kukatika katika kwa umeme na maji au hali ya joto kuongezeka kunakuharibia mood kiasi cha kukosa namna bora ya kuchangia ama kujadili mada, nakuomba upite kimya kimya tu pasi na kuharibu uzi.

Kupata uelewa wa mambo haya hayakufanyi uwe mshirikina, ni kuongeza uelewa tu, yapo mengi tunayoyajuwa lakini si kwa kuyafuata ama kuyafuatilia.

Aliyeniambia mimi ni mpenda papuchi halafu nakaa kwa shemeji yangu nadhani hajanifahamu vizuri, papuchi kweli napenda, lakini sikai kwa shemeji yangu na wala sina shida za pesa kiasi cha kuombwa na kuwa sina (angalau kwa kiwangu changu)

Kwa wale waliooa ama kuolewa wakiwa ‘bikra’ na wakadumu kwenye ndoa zao bila kuchepuka mada hii hawawezi kupata uhalisia wake maana hawatakuwa na ulinganisho.

Kwa wale wanaume wenye wake zaidi ya mmoja wanaweza kujuwa au kufanya utafiti wakajionea wenyewe.

Kwa wanawake ambao wanatembea na wanaume zaidi ya mmoja wanaweza kuwa mashahidi wa dhana ya mada hususani baada ya kujuwa kumbe kuna kismati na nuksi…

Kwa vijana ambao bado bikra (kama wapo humu wake kwa waume), tulieni mjifunze…
Kwa ambao hawajaoa na hawajaolewa lakini ni washiriki wa zinaa kwa kuchanganya wenza zaidi ya mmoja anzeni kufuatilia dhana hii.

Kismati ama nuksi inayozungumziwa hapa ni ile ambayo baada ya tendo la ndoa mambo yako kwa siku hiyo ama siku mbili tatu zijazo yanaenda vizuri ZAIDI ama hayaendi vizuri KABISA, inakuwa si nuksi au kismati cha kudumu.

Kwa mwenye shuhuda anaweza kutuambia jambo humu akipata nafasi ya kuandika.

Hatimaye tutawaomba wataalam wa tiba kwa njia za kiroho watupe muongozo nini cha kufanya endapo umehisi kupatwa na hali ya namna hii kwa wale ambao wapo kwenye ndoa.

Kwa wale ambao hawapo kwenye ndoa dawa ni KUJUWA yupi ni yupi na kujihadhari, basi.

Tuendelee kujadili kwa staha.

___________
JBourne59
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom