Wanawake wanasayansi walioifanyia makubwa dunia

abelauthor

New Member
Jul 19, 2021
4
4
UTANGULIZI
“The world need science and science needs women and girls”/Dunia inahitaji sayansi na sayansi inawahitaji wanawake na wasichana"

Huu ni msemo maarufu unaotumika kila wakati kuwahamasisha watoto wa kike na wanawake kujikita na kujihusisha na mambo ya kisayansi lakini hasa hasa msemo huu ni maarufu na hutumika zaidi siku ya Februari 11 ya kila mwaka.
Februari 11 ya kila mwaka ni Maadhamisho ya siku ya kimataifa ya Wanawake na watoto wa kike katika sayansi(International Day of women and Girls in Science).
Siku hii Ilianzishwa na umoja wa mataifa tarehe 22 desemba mwaka 2015 kupitia shirika lake la Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO),(Resolution AIRES/70/212)kwa lengo la kuwahamasisha wanawake na watoto wa kike kujikita na kujihusisha na mambo/masomo ya sayansi.
Mwaka huu 2021 siku hii iliadhimishwa kama kawaida na ilikuwa imebebwa na kauli mbiu”Women Scientists at the forefront of the fight against COVID-19”/Wanawake wanasayansi katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa uviko- 19”

NINI KILICHOCHEA ZAIDI KUANZISHWA KWA SIKU HII?
Sababu kubwa iliyochochea kuanzishwa kwa siku hii ni ushiriki hafifu wa wanawake na watoto wa kike katika masomo/shughuli za kisayansi,hii inatokana na tafiti zilizofanya na shirika la umoja wa mataifa UNESCO pamoja na UN women.
Tafiti zilionyesha kuwa ni:
Asilimia 30 tu ya watafiti wote duniani ni wanawake kwa maana nyepesi tunaweza kusema kuwa katika kila watafiti 10 kuna wanawake 3 tu .
Lakini pia tafiti zilizofanywa na shirika la UNESCO mwaka 2014-2016 zilionyesha kuwa ni asilimia 30 pekee ya wanawake na watoto wa kike wote wanaofika vyuo na vyuo vikuu huchagua kozi zinazohusiana na mambo ya kisayansi.
Tafiti hizi zilienda mbali zaidi na kuainisha kwa asilimia idadi ya wanawake waliopo katika kila eneo linalohusiana na sayansi na tafiti zilionyesha:
3% wanajihusisha na mambo ya kompyuta(ICT)
5% wanajihusisha na mambo ya natural science,hesabu na takwimu.
8% wanajihusisha na mambo ya uhandisi na ujenzi.
(Tafiti zote zipo kwenye tovuti ya www.unesco.org)
Siku hii ni maalumu na ipo kuwaamsha watoto wa kike wajikite zaidi katika masomo ya sayansi.
Licha ya uchache wa wanawake katika sayansi,wachache waliopata nafasi ya kuwa wanasayansi wameifanyia makubwa dunia.
Leo nitakutajia wanawake hao na kazi kubwa walizozifanya lengo kubwa likiwa kuwahamasisha mabinti na wanawake wengi zaidi kujikita kwenye masomo ya sayansi,Karibu uhamasike……..

ELIZABETH BLACKWELL
Huyu ndiye mwanamke wa kwanza dunia kuwa daktari wa binadamu .
Alizaliwa Tarehe 3 Februari mwaka 1821 nchini Uingereza.
Toka akiwa mtoto alitamani sana kuwa daktari hasa alipowaona madaktari wa kiume,
Haikuwa rahisi kutimiza ndoto zake hasa kwa nyakati hizo ambapo wanawake hawakupewa nafasi kabisa ila alipambana mpaka mwisho ikawa.

MARIE SKOLODOWSKA CURIE
Mwanamama na mwana sayansi hodari kweli kweli kuwahi kuwepo ulimwenguni,
Mwanamama wa kwanza kupokea tuzo za Noble peace prize na binadamu wa kwanza kuchukua tuzo ya Noble peace prize mara mbili.
Alizaliwa nchini Ufaransa katika jimbo la warsaw mwaka 1867 na kusomea masomo ya Fizikia katika chuo kikuu cha Paris.
Dunia inamkumbuka kwa mambo makubwa mawili.
Moja,Ndiye aliyegundua Sayansi ya Mionzi(Radioactivity).
Pili,Ndiye aliyegundua tiba ya kansa(Effective cure of cancer) kwa njia ya mionzi.
Asante Mama Marie curie,uliigusa dunia na dunia yote bado inakuimba mpaka leo.

HYPATIA
Huyu ni mwanamke mwanamahesabu wa kwanza kupata kuwapo ulimwenguni.

ANNE OF DERNMARK (1532-1585)
Mfamasia wa kwanza mwanamke

ELIZABETH BRAGG
Huyu ni mwanamke wa kwanza kuwa mhandishi(engineer),alitunukiwa digrii ya kwanza ya uhandisi ujenzi mwaka 1876 katika chuo kikuu cha califonia.
Alizaliwa Tarehe 23/4/1858 nchini marekani.

ADA LOVELACE
Huyu ni mwanamke wa kwanza kujihusisha na mambo ya sayansi ya kompyuta,its first woman computer programmer in the world.

FLORENCE NIGHTINGALE
Wengi wanapenda kumuita”The lady with the lamp” au “angel of the crimea”
Huyu ni mama wa tasnia ya wauguzi duniani hodari na kiigizi cha watu wengi.Alipata umaarufu mkubwa kutokana na namna alivyoipenda kazi yake.Iwe mvua,iwe jua hakuna kilichomzuia kufanya kazi ya shauku yake.
Jambo hili lilithibitishwa na utayari wake wa kwenda vitani mwaka 1853 kuwahudumia wanajeshi wa taifa lake la uingereza waliokuwa wanapambana na dola la kirusi .(vita hivyo viliitwa Crimeen war)
Umahiri huo ndio uliomfanya watu wampe jina la “the lady with the lamp” au “angel of the crimea”

WANAWAKE WANASAYANSI WA TANZANIA
Kutokana na uhaba wa data zilizopo kwenye vyanzo mbalimbali nimeshindwa kupata taarifa nyingi na za kutosha juu ya wanawake wanasayansi wa hapa nchini kwetu,Lakini walau nitawapa kile nilichofanikiwa kukipata:

DKT: MARGARETH.E.BILLINGHAM
Huyu ni daktari bingwa wa magojwa ya binadamu.
Alizaliwa septemba 20 mwaka 1930 mjini Tanga,Tanzania.
Baba yake alikuwa ni mwingereza na mama yake mtanzania.
Alipata elimu yake nchini kenya na baadaye nchini Uingereza katika chuo cha Stanford University Medical centre aliposomea udaktari wa binadamu na kubobea katika masomo ya pathology.
Alipewa heshima na anakumbukwa mpaka leo duniani kwa kufanya tafiti juu ya Transplant rejection (billingham criteria).

PROF:JULIE MAKANI
Profesa na mtafiti wa mambo ya afya ya binadamu.
Ni mkuu wa kitengo cha Hematology na blood transfusion katika chuo kikuu kishirikishi cha Afya Muhimbili.
Alizaliwa mwaka 1970
2011 alipewa tuzo ya Royal society Pfizer kwa kazi yake nzuri ya tafiti juu ya ugonjwa wa selimundu(sickle cell diseases)
2019 aliorodheshwa miongoni mwa wanawake 100 wenye ushwawishi mkubwa Tanzania na shirika la BBC.

DKT: WINNIE MPANJU SHUMBUSHO
Aliwahi kuwa mkurugezi msaidizi wa shirika la afya duniani katika kitengo kinachoshughulikia magonjwa ya Kifua kikuu,Malaria na Magonjwa yasiyotiliwa mkazo mwaka 2015.
Daktari mbobezi wa magonjwa ya watoto katika hospitali ya taifa Muhimbili.

MARY MGONJA
Mtafiti na mtaalamu wa kilimo,anamiliki kampuni inayojihusisha na shughuli za kilimo iitwayo Nambari Agriculture Co.ltd

HITIMISHO
“The world need science and science needs women and girls”/Dunia inahitaji sayansi na sayansi inawahitaji wanawake na wasichana/watoto wa kike”
Hakuna cha kuwazuia tena,dunia inawasubiri mlete suluhisho la matatizo yaliyopo kupitia sayansi.
Mnaweza kuwa madaktari,Mnaweza kuwa wa kemia,Mnaweza kuwa wanaanga,Mnaweza kuwa wanasayansi
MNAWEZA, MNAWEZA, MNAWEZA
Andiko hili likawaamshe,
MKAAMKE, MKAAMKE, MKAAMKE KWELI KWELI
 
Back
Top Bottom