Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,367
- 11,604
Nimetimiza wiki ya pili tokea kuhamia kwenye makazi haya mapya. Kama ilivyo kwa mwanaume lijal, ilinipasa kutengeneza mahusiano mapya ya karibu ili nipate mahala pa kupozea kiu yangu ya kimwili.
Kusema kweli, nimehamia uswazi nikitokea maeneo yenye hadhi yake. Siyo kwamba niko tofauti sana na vijana niliyowakuta huku, labda tu katika ongea yangu na muonekano umeongezeka kidogo, si mnajua tena uraibu wa maisha ya chuo na hali halisi ya maisha?
Ndani ya wiki ya kwanza tokea kuhamia hapa nilikuwa kauzu, sikutaka kuzungumza na binti yeyote hapa mtaani, lengo kuu hasa lilikuwa ni kusoma mazingira kwanza.
Wiki ya pili ndipo nikaanza kutupia nyavu, cha ajabu wengi wao nikiwasimamisha barabarani hawasimami badala yake huongeza kasi, wengine najaribu kwenda nao sambamba ila wanajawa na uoga, hata wanapozungumza wanakuwa ni watu wa kutetemeka!
Wengine huwa wanapita kwenye njia inayopita karibu na mahali nilipohamia, ila baada ya kuwatongoza hubadili njia. Kuna binti tuliahidiana nimuumize siku ya jana, lakini naye kapotea jumla! Lakini ninapoingia kwenye baa, vyombo vya usafiri au wanachuo nawanasa kirahisi tu kama kawaida tu.
Shida itakuwa wapi wakuu?