Career husika mtu alioichagua inabidi aifanye kwa uwezo wa juu sana na kuwa productive person kwa grade A,
Kuhusu ndoa hata machizi wanaoana, sio big deal sana kuachieve ndoa mzee, ukiamua kuoa/ kuolewa ni easy tu, issue kuoa/kuolewa na soulmate au mtu unaemtaka, sasa hapo ndio watu mnawapa pressure wadada wakubali tu mtu yeyote for the sake of ndoa, life has quality and that quality should be maintained
Sawa tufanye Career ni kitu muhimu na kuwa Productive person Grade A ni important achievement.
Naomba nikuulize maswali yafuatayo;
1. So kwa mantiki (logic)hii una maanisha wanawake wanapozaliwa kitu cha kwanza kwao kwenye maisha ni careers zao, je kama hilo ni kweli, vipi sehemu ambapo hakuna shughuli za kibiashara (tertiary industry),yaani hakuna room for employment mfano huko vijijini, majangwani, au zile jamii zilizopo nyuma ya kimaendeleo, so huko ina maana wanawake hawana watakalofanya zaidi ya kuexist kama misukule tu, si ndio?
2. Kwa mtazamo wako ina maana mabinti wote wafocus na careers na kuwa Productive katika hizo careers tu, je, how long does it take to be a full fledged career woman?
Kwa ninachojua kwa wastani binti anamaliza form 4 akiwa na wastani wa miaka 17 hadi 19. Plus form 5 na 6 ni 2 years added, chuo hapo akianzia cheti hadi kuhit degree level ni wastani wa 6 years on top, akianzia degree straight ni 3 years minimum some careers degree kama medicine inaweza take over 7 years.
Hajaingia mtaani sasa kutafuta experience ili awe fully cooked kwaajiri ya career. Hapo mpe hata 5 years tops. Hivi hapo tuna assume hajihusishi kabisa na mahusiano. Ukijumlisha huo umri unadhani anaangukia kundi gani la wanawake kama sio msimbe direct?
Okay by statistics, wanawake wote wanaosoma huwa wanafanikiwa kuwa na successful careers? [emoji848]
Tuassume ameamua kufanya biashara, how long does business guarantee a successful career?
Why kurisk kutokuwa na mahusiano serious eti kwasababu ya career?
So mfano anafanikiwa at that going age, je ni mwanaume gani atakuwa katika finish line amsubirie yeye amalize hizo shughuli zake za kujitafutia career awe successful ili amuoe amuweke ndani kama mke bora na kufanya nae familia, na hapo hapo nikuulize huyu dada hiyo experience ya kuwa mke anatoa wapi, given anatakiwa kuwa mama wa familia alee watoto, mume na kutunza familia? [emoji848]
So technically tunazungumzia binti kuwa set for life failure?