Kuna Mwamba alimtokea dada mmoja huko Babati, mdada akaringa jamaa akapiga chini Kwa kukausha tu kimya, leo tukaja Babati kikazi, jamaa akaona isiwe shida amtafute japo wasalimiane, mdada akasema yuko kijijini kwao sijui kunaitwa Basutu, jamaa akasema poa kama hatajali mdada aje town waonane, mdada akakubali, baada ya ya kukata simu, nusu saa baadae mdada anamtumia sms Mwamba kwamba amtumie hela akasuke, Mwamba akamwambia atakuja asuke akifika town, mdada akanyamaza, nusu saa nyingine akabadilisha gear , akatuma sms kwa Mwamba kua amtumie basi hela akanunue kiatu, dah! Maana yake anatembea peku??? Jibu ni hapana
So wadada wengi wanaweza kukosa waume kwa uzembe wa kitu kidogo sana na Cha kijinga sana, hawafichi matatizo yao na hayo matatizo yao yanafikirisha sana
Shida zinaibuka baada tu ya mwanaume kumtafuta, sometimes mtu ana makusudi nae mazuri kabisa lakini mtu anastuka kua huyu hawatapendana bali wataishi kimaslahi.
Wanaume wengi huvutiwa na maumbo au face ya mwanamke, lakini mwanaume akimkuta huyo mwanamke ana kitu kingine kama heshima, staha na nidhamu.. jumlisha na uzuri wa sura na tabia, ni rahisi sana mwanaume kumchukua huyo mwanamke na kuishi nae, so ni kweli mabinti wengi hua wanaweza kuwafukuza waume wa kuwaoa kwa mambo ya kipuuzi ya kutojizuia
N:B Thubutu kwa Single MAMA sasa uone jinsi Dunia ilivyo na maajabu