Wanawake wa Online Dating Mbona Waongo???

Vaislay;

mimi wa ukwel nipog.find me

Atajuwaje kama wewe ni wa ukweli na hutaitupa engagment ring yake kwenye takataka kama ulivyomfanyia huyo mwingine?
 
Siko hapa kuwakebehi wanawake ama dada zetu lakini hii habari ni ya ukweli na iko-based na my own personal experience huko ughaibuni na kwa sasa hapa Dar. Nimejaribu mara kadhaa kutafuta rafiki kwaajili ya dating then kama chemistry ipo na tuna-click basi sitosita kuendelea kumpenda ambaye tutapatana ili eventually tufunge ndoa na nitulizane na mwenza wangu ili tuendelea na safari ya maisha.
Baada ya kuwasaka akina dada wa mitaani/makazini/makanisani na miskitini etc. bila mafanikio nikaona sasa nihamie online dating, ambako nimekutana na wanawake wa aina mbalimbali lakini tatizo wanawake wengi wa mtandaoni sio wakweli.
Utakuta mtu kaweka kwenye profile picha yake nzuri anapendeza na anavutia. Lakini tukikubaliana tuonane nakuwa nabaki mdomo wazi.
1. Unakuta kwanza hiyo picha kumbe ni ya zamani alipokuwa bado umri haujaenda na akitokea unakuta umri umekwenda
2. Mdada ni mnene zaidi transforma wakati alisema kwenye profile yake kuwa maumbile yake ni slim/average.
3. Anadai ktk profile yake kuwa ni mrefu kumbe ni mfupi. n.k.

Nimeshakutana na wadada 13 (8 ughaibuni 7 hapa hapa Dar) na mara zote nimepoteza muda wangu na pesa zangu kwaajili ya hizi dates na kuambulia kulipia gharama za dinner, wine, taxi etc at expensive restaurants.
Swali:
1.Je wanawake wanaotafuta wapenzi online ni wale ambao hawavutii kimaumbile na wako desperate?
2. Kwa nini akina dada hawako wakweli ktk online profiles zao? mnaweka picha za zamani, mnadai wembamba kumbe wanene?

Mkuu nafikiri kwako kuna tatizo na linasababishwa na wewe mwenyewe
Wife material hatafutwi kama nyanya sokoni na just note that huwezi ukampata perfect au mwanamke perfect one hundred percent. Ni kumtengeneza mtu wako mkuu. Ni kumtayarisha na kumuandaa kuwa mke na hali ukijua kuwa kuna mapungufu mengi tuu utakumbana nayo kaktika safari yenu ya maisha na wala sio kuwa kila kitu kitakuwa perfect
Najua wewe una mapungufu yako na yeye ana yake sasa mnajitahidi kuzika tofauti zenu na kutengeneza kitu ambacho nyie wenyewe mtakifurahia
Mkuu katika wanawake wote uliokuwa nao kuna kitu ambacho hakiko sawa maana sidhani katika hao wote kumi na tano hakuna hata mmoja ambeye alifaa kuwa mke
Jievaluate ukpya jna ujiangalie kuna nini kwako kabla ya kumuapproach mwanamke yoyote na hicho ambacho kiko kwako kitoe
Sidhani katika hali ya sasa wanawake wote eti wanakuambia hawako tayari kuolewa au wana mambo yao hayako tayari au wewe hukuona hata mmoja wkao wa kuwa mke
 
The Boss, kama nilivyoeleza ktk thread yangu kuwa nimehangaika kwenye real world bila mafanikio kwa hiyo nikaona sasa nhamie mtandaoni labda ndio bahati yangu iko huko, lakini duu! yani nimepoteza muda na pesa.
Kwenye real world nimekutana na wanawake lakini sijafanikiwa kukutana na wife material women
Nadhani wewe utakuwa na matatizo tu, siyo rahisi kwamba hujafanikiwa kukutana na material women. Yawezekana kabisa pia kuwa wewe ndiyo siyo husband material man!
 
Wanawake wa online dating huwa ni wale ambao aidha wameachwa au hawana mvuto kabisa kiasi ambacho hawatokewi na wanaume.Wale walioachwa hutaka kuziba pengo la kuachwa haraka iwezekanavyo.Mimi nilikutana na mdada mmoja mfupi,mnene na ana mustachi!Nilitaka kukimbia,lakini nikajikaza tukazungumza.Alipoondoka sikumtafuta tena.
 
inawezekana maneno yako yana ukweli ndani yake
 
Mkuu Vuvuzela, uko sawa kabisa na wala mtu asikudanganye, ukitaka kujua uko sahihi angalia hakuna mchangiaji anayejibu hizo namba 1,2 na 3 ambazo umeweka hapo juu kuhusu baadhi ya uongo wa wadada mtandaoni, labda hawataki kujibu kwa sababu jamii nzima (incl wanaume) imeharibika kiasi cha kuona hayo uliyoandika kuwa ni ya kawaida! Kuna watu kwao ni kitu kidogo sana kudanganya jina, umri, kimo, uzito nk! Kuna mdada niliwahi kuwa na mawasiliano nae, akanifunga kamba ana 21, siku ya siku niko bongo kuwasalimia bandugu nikamzukia huwezi amini alikuwa kama 35+ na mkorogo juu...Ilibidi nimpe shikamoo!! Sasa hivi mdada akisema ana 18 inabidi niongeze angalau 5..akisema anaitwa Asha, najua anaweza itwa Hadija pia.... Yaani ni full pasua kichwa... So mkuu hauko peke yako kuna watu tunachukia uongo.
 
Mkuu thanks for your testimony!
Nilifikiri nadanganywa mimi tu kumbe tuko wengi.
 
mkuu mi nikupe tu pole ila kwa ushauri wangu mi naona kwa ajili ya kupunguza gharama za maisha ni bora ukawa na hawa ambao unakutana nao face to face,
hapo wewe binafsi unakua jaji kwa kwanza
walio wengi hasahasa facebook utakuta kaandika visifa kibaooooooooooooooo kumbe hana hata kazi inayoeleweka

so take right selectin before you have lost totally hope!
 
mbona na wanaume wa online nao ni matapeli vile vile.tit for tat.binafsi mimi siamini mapenzi ya mitandaoni.relax,ipo siku utampata wako.
 
hahahaa hii mada imenigusa,am guilty as charged lol ukiniona facebook mrembo size14 kumbe nimekongoroka na niko size 22 lol
 
Pole sana kwa yaliyokukuta.
Online hakuaminiki, bora huyo aliyesema mnene kumbe mwembamba. Wapo wengine matahira kabisa.
 
Mkuu Vuvuzela, uko sawa kabisa na wala mtu asikudanganye, ukitaka kujua uko sahihi angalia hakuna mchangiaji anayejibu hizo namba 1,2 na 3 ambazo umeweka hapo juu kuhusu baadhi ya uongo wa wadada mtandaoni, labda hawataki kujibu kwa sababu jamii nzima (incl wanaume) imeharibika kiasi cha kuona hayo uliyoandika kuwa ni ya kawaida! Kuna watu kwao ni kitu kidogo sana kudanganya jina, umri, kimo, uzito nk! Kuna mdada niliwahi kuwa na mawasiliano nae, akanifunga kamba ana 21, siku ya siku niko bongo kuwasalimia bandugu nikamzukia huwezi amini alikuwa kama 35+ na mkorogo juu...Ilibidi nimpe shikamoo!! Sasa hivi mdada akisema ana 18 inabidi niongeze angalau 5..akisema anaitwa Asha, najua anaweza itwa Hadija pia.... Yaani ni full pasua kichwa... So mkuu hauko peke yako kuna watu tunachukia uongo.
<br />
<br />
hahahaha! Kumbe mnakamatika wengi. Lol
 
Eh! Suala gumu kweli kweli kisaikolojia ninayomengi ya kueleza juu ya uamuzi wako wa kuleta suala ilo hapa jamvini, hasa nikiangalia Content na maudhui yake, kwakweli PYSCHOLOGICALY inanipa nafasi ya kuchanganua mengi...any way niachane na upande huo niichukulie/niitazame kawaida, kisha niseme...

1. Dunia ya leo watu hawaangalii mwanamke sura/Umbile wala rangi. watu wanaangalia mwanamke mwema, mwenye upendo kwa familia na jamii ya Ndg na marafiki, mwanamke mwenye mtazamo chanya wa kujenga familia kiuchumi na kukusaidia kufikia malengo ya maisha zaidi sana mwanamke mcha mungu.

kwa maana hiyo ukimwitaji mwanamke wa namna hii "Mdau mwenzangu" hapatikani kwenye mitandao au online, kwani sifa hizo zinaitaji kumwona mtu na kumfahamu kisha umwambie NAKUPENDA. unampendea nini? jibu ni hayo uliyokwisha yaona.

Kwa mwanamke wa online huwezi ona sifa hizi! utaishia kuona umaili wake wa kuandika mail nzuri, kuchati kwa speed na kujaza profile yake sifa za uongo na picha fake kama yaliyokukuta. kwa hiyo utafutapo online uwe unahitaji sifa hizi basi utapata lakini kama ni sifa za mke bora ambaye wanaume wengi uHitaji leo basi andika maishani neno "NOA" Kwa watafutao wenzi wa maisha mitandaoni

Watu weupe {wazungu} na nchi baadhi za afrika hutumia online dating ku-earn money toka kwa wanaume waroho na wenye tamaa, wengine hufanya kuendeleza shughuli zao za ualifu wa mitandao (Cyber crime).

Tanzania kuna warembo kibao kila kona wenye sifa njema (uzitakazo) kazini, chuoni, mtaani kwenu, mtaa wajirani, rafiki yake rafiki yako, mtoto wa shangazi jirani na kwa wifi/shemeji hapo pia yupo mmoja, au nako hujaona? Natia Shaka!

Naomba kuwakilisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom