Wanawake unganeni; kwa hili Polisi wanawavunjia Heshima .......... (picha)

To me hayo yalikuwa maandalizi ya kumbaka!
Uyu dada afungue kesi tuu na ushaidi anao!

Hao Polisi wanajulikana maana picha zinaonyesha ni akin nani ila kwa sababu wametumwa kufanya hiyo kazi sidhani Kama watachukuliwa hatua yeyote huu unyanyasaji ndiyo ambao unalalamikiwa sana siku hizi.
Hii post nilishangaa sana jana usiku ilipelekwa kwenye jamii photo ilionekana Kama haina umhimu.
 

katu tusitarajie eti POLISI watakuja kuwa na heshima ya HAKI ZA BINADAMU kama jamii hatujaamua wawe nazo. Kila kitu is a socia product, hakuna kilichopo hapa kwetu jamii haijakibaliki. This is essentially social product.

Kama kweli tunataka POLISI waheshimu haki za binadamu, kuna utaratibu wa kisheria kufanikisha hili. Hivi tuna wanashaeria wangapi ambao wanashugulika na utetezi wa haki za binadamu? Ushahidi wa picha katika ukiukwaji wa haki za binadamu uko wazi kwa nini wasimtafute mdada huyo na kumpa msaada wote wa kisheria ili kurejesha adabu ya jeshi la polis kwa wananchi?

Hapa tanzania kuna japo utawala wa sheria ingawa wanajamii hatutaki kuhakikisha unatumika. Polis sio MUNGU kwamba sheria itamsamehe. Naye ni mwanadamu anayeongozwa na matakwa ya sheria tena anatakiwa kuwa mfano. Kwa jinsi ninavyojua, iwapo hao watu watashitakiwa, Jeshi litawakana na wanaweza kufukuzwa kazi. Na iwapo JESHI LITAJITOKEZA kuwatetea, basi watalazimika kulipa fidia kubwa, kwani suala liko wazi kuwa nguvu za ziada zimetumika katika kumkamata.

Naamini kama wangemuita tu, mdada huyo angetoka, na kama angegoma, wangeweka ulinzi wakawatafuta polisi wa kike waje kumkamata. Huu ndo utartibu hii ndo sheria.

Wanasheria msitulazimishe tufikirie weledi wenu
 

aliyewatuma wakisha shitakiwa, atawakana. Unakumbuka yale maujai ya ARUSHA miaka ile ambapo RPC aliwashinikiza askari wake kuua, liliposanuka, wale askari wakajitetea tulitekeleza maagizo ya boss, bosi wao akawakana kweupe?

suala ni utawala wa sheri, wamekiuka sheria, kesi ipelekwe mahakamni uone kama hawatapatikana na hatia. Jeshi la polis la sasa si la kutumia maguvu, ni akili zaidi
 
Sisiemu wanapigania haki za viongozi sio haki za wanawake.yaliyo mkuta mke wa dr wa ukweli lilikua na fundisho tosha kwa wanawake wote wa tanzania.wanawake amkeni leo ukiona kwa mwanamke mwenzio ujue kesho kwako
 
Wanawke JF nanyi mmenishangaza sana! Kazi kuchangia threads za ma-love tu... Haki zenu hamjitokezi! Ukifutilia hii thread ni wanawake wachache sana wametoa maoni... wapi FF, Pretty na wengineo?

Pili, Juzi mama Migiro alizungumzia ukatili dhidi ya wanawake... leo tunashuhudia ukatili huu kitaifa na hakuna viongozi wa wanawke kitaifa wanaochukua hatua!

Polisi wamezoea kuvunja haki za binadamu bila kuwajibishwa! Tujiulize iwapi kesi ya kutaka kumbambikia mtoto wa Reginald Mengi madawa pale Dar Airport? Wapo wapi wale waliotajwa? Ukweli wa jambo lile ukoje je ile tume ya IGP ilikuja na ukweli gani? Na hata waandishi wetu wakikutana na IGP hawaulizi hilo. au ni wnananchi, waandishi na serikali tumezoea impunity?
 
Akina mama kamwe hawawezi kuungana na kukumea ushenzi huu. Hao polisi wangekuwa ni vijana wa chadema, hapo ndio ungemsikia nape na makamba wakiwataka viongozi wa dini na wanaharakati kuilani chadema. Hivi sasa hawajui haki za wanawake hadi kwenye kampeni na wakifanyiwa wao, lakini wakifanya wanakaa kimya. Siku inakuja ambapo hayo yote yatazikwa jangwani au baharini katika kaburi moja na ccm. TUJIPE MOYO, TUTASHINDA.
 

Intelijensia haikuwa na habari siku Twiga walipoibiwa.
Ila siku ya maandamano ya Chadema intelijensia inapata habari kuwa ktk maandamano hayo panaweza kuwa na matukio ya wale swahiba zangu wala Gomba toka Kismayu Somalia...dah hii nchi ushuzi kweli
 

Police wa bongo hawataki kusoma ili wapandishwe vyeo wanataka kupanda vyeo kwenye matukio kama haya kwahiyo ukatili kama huu tuutegemee sana hapaTZ
 

Tena limetokea kipindi kizuri sana ambacho bunge linaendelea kazi kwenu wadada wabunge, je mashirika ya haki za binadamu mpo wapi? Wanaharakati je?
 
Muanzisha thread ni mnafiki sana ulikuwa wapi kutoa kauli kama hii wakati wahuni wa Chadema walivyomdhalilisha DC Fatma Kimario wa Igunga?
 

Aangalie lipi jipya kwake kama yeye yupo hivyohivyo kwa wameiga wapi hawa?
 

zipo ila zinatumika kama upinzani na masikini wa tz hii wakivunja otherwise haitumiki
 

Bora roboti lina garama ya kutumia umeme
 
sasa nimeanza kuelewa kwanini Ghadafi aliingizwa kijiti.
Pata picha huyo ni dadako, utaacha kujifunga mabomu kweli?

Magamba hawajalitambua hilo akili zao zinafikiria hapo hapo kama za kuku washiba leo hawajui akiba ya kesho
 
Muanzisha thread ni mnafiki sana ulikuwa wapi kutoa kauli kama hii wakati wahuni wa Chadema walivyomdhalilisha DC Fatma Kimario wa Igunga?
Uliata Thread ngapi kuhusu Fatuma? kulikuwa na tread ngapi humu za Fatuma? au lazima mimi ili niwe na uwezo kutoa hii mada? nilidhani hakifanya mwingine sitakiwi kurudia

Anyway nini msimamo wako kwa vitendo hivyo vya polisi ukiachilia mbali unafiki wangu
Mwisho fatuma sio muislamu anafuga nguwere na haku dume lililomshika kiuno kama huyp polisi na mwana UDSM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…