Wanawake, ukitaka mwanaume akuoe fanya hii kitu

Wanawake, ukitaka mwanaume akuoe fanya hii kitu

Khaaaaah!!! Akuu taabu yote ya nini!!!!
 
Sio kwa Kila mtu,sio Kila mwanaume anampenda mama ake,Mimi binafsi katika wanawake ninaowachukia duniani ni mama angu
 
Wanawake wengi wanapenda sana kuolewa pia wanaume wanapenda sana kuoa ni heshima kwa hao waliooana kuwa sasa wamekuwa wakubwa na wana majukumu ila bahati mbaya au nzuri, mwanaume ndio mwenye maamuzi ya kuoa na sio mwanamke.

Endapo wewe mwanamke uko na mpenzi wako na unataka akuoe cha kufanya ni cheza na mama yake hakikisha unakuwa mtu wa karibu na mama yake kwa kuwa rafiki yake. mama yake akikukubali, asilimia kubwa umemaliza kazi.

Muda unajizoesha kwa mama yake ni matumaini yangu baina yenu mnajuana tayari vizuri.
Mkuu hiyo ni kwa wanaume wasiojielewa na wanaopangiwa cha kufanya na wazazi wao.
Ila sisi wanaume wenye maamuzi bila kupangiwa, swala ni moja tu kuwa mpenzi bora kwake na fanya kila ubunifu wako jamaa aone unafaa kuwa wife. Hapo ni automatically utaenda kutambulishwa na kuolewa.

Wanaume huwa tunafikilia pafupi kama dem unamkubali.
 
Kwa sisi tusio na mama wewe cheza na dushelele zetu vzuri na kuwa na tabia njema, pika chakula kitamu, fua nguo, safisha nyumba, kama sina hela nielewe, mche Mungu vzuri, Nipe mapenzi vzuri zen jitahidi kuact kwamba ww ni mke bora kwenye mambo ya uchumi na mambo ya kijamii. Mengine utasimuliwa na kungwi wako. Basi nshakuoa.
 
kuna ka ukweli,hamna mwanaume hampendi mwanamke anaependwa na familia yake na hata ikitokea ana taka kumuacha lazima ajiulize maswali 50 kidogo.

hapo mwanamke anakua kajitengenezea ka kitu flani hiviii,asee mimi mwanamke ampende mama angu amfanye shost ake sijui kama ntamuacha.

ndio mana stakagi kabsa story za kuwaongelea wazazi asije niambia "ebu nipe nimsalimie mama" story mwisho anogewe aniwekee password mimi.
 
Kama hana mama unafanyaje [emoji125]‍♀️[emoji125]‍♀️
 
Back
Top Bottom