Habari Wanajf..
Hii Habari Nimetoa BBC Swahili..
Wanawake Tuwe Makini Na Tunaowaita Wapenzi Wetu..
Polisi nchini Austria wanawahoji
wanawake ambao wamehadaiwa na
mwanamume mwenye mazoea ya
kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
wanawake wengi tu.
Mwanamume huyo raia wa Gambia
mwenye umri wa miaka 28 ameoa
wanawake watatu huku akiwa katika
uhusiano wa kimapenzi na wanawake
wengine 15
Kwa mujibu wa mtandao wa 'ASN
American street news', Tijan Sonko,
alikamatwa tarehe mbili mwezi
Oktoba katika uwanja wa ndege
mjini Vienna akiwa anarejea kutoka
nchini Gambia.
Pia anatuhumiwa kwa udanganyifu
baada ya kuwapora wapenzi wake
yuro 38,000.
Kadhalika ameshtakiwa na kosa la
wizi na kutumia vitambulisho
bandia.
Kulingana na shirika la habari la
Austria alitumia bima ya afya ya
rafiki yake kudai faida anazopata
mtu ambaye hana ajira kutoka kwa
serikali.
Mwanamke mwenye umri mdogo
sana kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na Sonko ana umri wa
miaka 22 huku mzee zaidi akiwa na
umri wa miaka 44.
Msemaji wa polisi mjini Vienna
alisema kuwa wanawake wote
waliohusika na Sonko wanahojiwa
kubaini ikiwa walidanganywa na
kuibiwa.
Sonko alidai kuwa alihitaji pesa ili
kuwatumia jamaa wake nchini
Gambia na wapenzi wake kadhaa
walimpa pesa na vifaa vingine vya
thamani.
Ameishi mjini Vienna tangu
Septemba mwaka 2010.
Udanganyifu wake ulijulikana wakati
wanawake wawili walijuana kupitia
Facebook, na kugundua kuwa
walikuwa wanatoka na mwanamume
mmoja.
Sonko ana watoto wanne mjini
Vienna, na wapenzi wake wawili
wanaaminika kuwa na mimba .
Ana mke nchini Gambia, na
anaaminika kumpa zawadi na
mapambo mengine aliyopewa na
wapenzi wake wa Austria.
Tangu picha yake kuchapishwa na
polisi, wanawake wengine wawili
wamejitokeza wakisema na wao
wamehadaiwa.
Hayaa Mapenzi Yamitandao Ya Kijaamii Kama Fb, Jf n.k madhara yake ndo hayoo...
Hii Habari Nimetoa BBC Swahili..
Wanawake Tuwe Makini Na Tunaowaita Wapenzi Wetu..
Polisi nchini Austria wanawahoji
wanawake ambao wamehadaiwa na
mwanamume mwenye mazoea ya
kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
wanawake wengi tu.
Mwanamume huyo raia wa Gambia
mwenye umri wa miaka 28 ameoa
wanawake watatu huku akiwa katika
uhusiano wa kimapenzi na wanawake
wengine 15
Kwa mujibu wa mtandao wa 'ASN
American street news', Tijan Sonko,
alikamatwa tarehe mbili mwezi
Oktoba katika uwanja wa ndege
mjini Vienna akiwa anarejea kutoka
nchini Gambia.
Pia anatuhumiwa kwa udanganyifu
baada ya kuwapora wapenzi wake
yuro 38,000.
Kadhalika ameshtakiwa na kosa la
wizi na kutumia vitambulisho
bandia.
Kulingana na shirika la habari la
Austria alitumia bima ya afya ya
rafiki yake kudai faida anazopata
mtu ambaye hana ajira kutoka kwa
serikali.
Mwanamke mwenye umri mdogo
sana kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na Sonko ana umri wa
miaka 22 huku mzee zaidi akiwa na
umri wa miaka 44.
Msemaji wa polisi mjini Vienna
alisema kuwa wanawake wote
waliohusika na Sonko wanahojiwa
kubaini ikiwa walidanganywa na
kuibiwa.
Sonko alidai kuwa alihitaji pesa ili
kuwatumia jamaa wake nchini
Gambia na wapenzi wake kadhaa
walimpa pesa na vifaa vingine vya
thamani.
Ameishi mjini Vienna tangu
Septemba mwaka 2010.
Udanganyifu wake ulijulikana wakati
wanawake wawili walijuana kupitia
Facebook, na kugundua kuwa
walikuwa wanatoka na mwanamume
mmoja.
Sonko ana watoto wanne mjini
Vienna, na wapenzi wake wawili
wanaaminika kuwa na mimba .
Ana mke nchini Gambia, na
anaaminika kumpa zawadi na
mapambo mengine aliyopewa na
wapenzi wake wa Austria.
Tangu picha yake kuchapishwa na
polisi, wanawake wengine wawili
wamejitokeza wakisema na wao
wamehadaiwa.
Hayaa Mapenzi Yamitandao Ya Kijaamii Kama Fb, Jf n.k madhara yake ndo hayoo...