Kuna mada zingine zinatokana na watu kutokufuata kile ambacho wanafundishwa katika dini zao.Mko mnafanya uzinzi ,kisha jamaa anakuambia anataka mtoto,na wewe unakubali.Hushituki kama jamaa anatumia gia kubwa kujihakikishia kila mwezi mko mnatafuta mtoto?Biblia iko wazi,watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.Vipindi vingine redioni ni maarufu,stori zinahuzunisha na kutia huruma ukifuatilia chanzo ni kutokutii Mungu ameagiza nini.
Nimesikia Tanga kuna tamasha linakuja,mtangazaji anatangaza kabisa bila kujua kama kuna watoto wanaisikiliza hiyo redio "ukiniona niombe kondom za fie...." Mtangazaji anamtangaza mwezake eti kila akitembea na binti mpya yeye hutumia kondom za vinundu.Hiyo ni redio inatangaza.Hapa ndipo tumefika wanadamu
Utachuma ulichopanda.Maisha unayoishi leo ni matokeo ya yale uliyotenda siku za nyuma,kuwa makini na unachokitenda leo,matunda yake yanakuja.