Nandinii
JF-Expert Member
- Jun 19, 2019
- 2,572
- 2,829
Habari zenu wakuu, wengi wa wanawake nimeweza kuwashuhudia pale wanapoona kuwa wenza wao hawana dalili ya kuwaoa basi uamua kubeba mimba kama ticket ya kuolewa. Anaona kwamba kama nikiamua kubeba mimba atanioa au lah kama nikibeba mimba basi wazazi wataweza niruhusu niende kwa yule mwanaume nikaishi nae.
Binafsi hili jambo huwa sioni kama ndiyo suluhisho sahihi kwa wadada ili wapate kuolewa mapema. Nimeweza kushuhudia zaidi ya mara 2 wanawake kubeba mimba ili waolewe lakini matokeo yake ndoa imekuwa yenye karaha na vituko kila kukicha, kiasi kwamba nikiwaangalia nawaonea huruma sana. Ingawa sio wanaume wote ambao watakutesa kwasbb umelazimishia mimba.
Ni bora hata iingie kwa bahati mbaya lakini sio uibebe kwa makusudi , huwa ni jambo baya sana wadada wenzangu, mana muda mwingine unakuwa umejifunga kitanzi mwenyewe bila kushurutishwa na mtu. Kama imeingia bahati mbaya basi mshukuru Mungu na ilee mimba yako lakini sio kubeba mimba ili uweze kuolewa mapema sababu tu mwanaume hana uelekeo wa kukuoa au umekaa na Pete ya uchumba kwa muda mrefu, huwa si jambo jema.
Naongea ili jambo kwa uchungu sana na lenye kuniumiza, sababu ya watu wa karibu ninaowafahamu kupitia tabu sababu ya kulazimishia mimba ili wapate kuolewa. Siyo wote ambao wataharibikiwa pale wanapobeba mimba kwa makusudi ili waolewe, mana wapo wanaume waelewa ,atakuoa na mtaishi vizuri tu lkn wapo wengine ambao atakuongezea machungu na maumivu ya moyo usiyoyatarajia.
Wadada wenzangu tuwe makini katika hili swala na tusipende kuchukua maamuzi ya ghafla bila kufikiria, kwa sbb tu huyu mwanaume hana dalili ya kunioa basi komesha yake ni mimba tu. Wazazi hawataki kuniruhusu niolewe na mwanaume hana uwezo wa mahali basi komesha yake ni mimba tu ili niende. Si jambo zuri hili, km anakupenda atakuoa kwa wakati sahihi na mtaishi kwa amani, utazaa kwenye ndoa lkn si kubeba kwa makusudi maana matokeo yake ni makubwa.