Wanawake tuna maneno

Wanawake tuna maneno

Hivi sisi hatuwezi kuwa marafiki mpaka tusemane vibaya, yani usipomsema mwenzio unaona siku haiendi au inakuwaje, unakuta unakuwa na rafiki mnasaidiana kwa hali na mali lakini au akiwa na shida unamsaidia tena vya kwake mchoyo kweli, unajitoa kwa kila kitu lakini utakuta linakusema vibaya sijui ni wivu, chuki hata sielewi aisee!

Hii tabia tunayo sana wanawake tubadilike jamani, maisha yashakuwa magumu maneno ya nini, mimi nishaamua sasa niwe mwenyewe tu sitaki marafiki maana ukigeuza tu mgongo wauaji, halafu ukitaka kukumbuka kitu ambacho umemuudhi huoni au ukimuuliza anasema hakuna kitu yaishe tu nisamehe.

Au wengine bila kusema wenzao siku haziendi vizuri "lazima tuji control "
Yaani nishaamua toka mwaka jana hakuna rafiki yeyote kushika simu yangu, wala kujua password, misele yangu napiga kimya kimya, sitambulishi mpenzi wangu tuonane wenyewe tu. Maana maneno mengi mpaka unachoka.

Wanawake sisi ni kibokooo
Dina wamekichukulia Kamikaze wako nini

Wewe ndo unashtuka saiviii poleeee!!!
Mie sinaga rafiki wa kike kabisaa wala sitaki, ukiwa na shida nitakusaidia nawe nikiwa na tatizo nisaidie lakini sio ushost wa kupeana sijui simu, pochi, nguo urafiki wa hivyo siutaki kabisaa kila mtu afanye yake, hayo mengine ni unafiki tuuu
Duuh kwa hiyo rafiki zako ni wa kiume tu?

Mfano ukienda kwenye hizi sherehe za wanawake watupu (kitchen party) inamaana unakuwa huna kampani kabisa??
 
Kuwa rafiki na MTU ni mtu mwenyewe mwingine anajua maana ya rafiki ni nn na mwingine anajua urafiki ni kupeana umbea na kuongozana pamoja that ol mengine yy hatambui
 
Duuh kwa hiyo rafiki zako ni wa kiume tu?

Mfano ukienda kwenye hizi sherehe za wanawake watupu (kitchen party) inamaana unakuwa huna kampani kabisa??
Sina hata rafiki wa kiume nina watu ambao tunasaidiana wakati wa matatizo na wakati wa furaha kama tukijulishana.

Bahati mbaya mie sio muumini wa sherehe za akina watupu sababu hazina umuhimu wowote kwangu
 
Ukitaka kumwandalia mwanao sherehe au sherehe ya namna yoyote inaonekana zinapooza sana kwa kuwa huna rafiki wa kukufuta jasho
 
Ukitaka kumwandalia mwanao sherehe au sherehe ya namna yoyote inaonekana zinapooza sana kwa kuwa huna rafiki wa kukufuta jasho
Sherehe ya mwanangu kama Mungu akija jaalia naamini kila kitu kitaenda sawa, marafiki haohao waweza kukuharibia.

Ndo maana nikasema nina watu ambao tunasaidiana wakati wa matatizo na wakati wa furaha, sio mashost kila mmoja yuko na mambo yake
 
Attachments

  • 1486113350486.jpg
    1486113350486.jpg
    8.4 KB · Views: 24
Mimi siku hizi nimebadilisha life style marafiki zangu ni wanaume tu.Wanaume mnaongea maendeleo na maisha ila wanawake mhhh nimekoma kabisa, sitaki .
 
Back
Top Bottom