Wanawake tulieni na ndoa zenu

Wanawake tulieni na ndoa zenu

Nyamalapa

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
211
Reaction score
470
Unakuta mwanamke ameolewa na anapewa mahitaji yote na muwe wake lakini hatulii kwenye ndoa yake, anaanza kurukaruka na wanaume tofautitofauti ambao hawamsaidii chochote zaidi ya kumpotezea tu muda na kumuharibia ndoa yake.

Kuna mwanamke nilijuana nae kwenye moja ya mitandao ya kijamii yapata kama wiki mbili tena yeye ndie ambae amekua akinisumbua inbox kutaka chatting za mara kwa mara.Nimemueleza kwamba nina mke lakini chakushangaza bado anaendelea kusumbua na sms zake nakulazimisha urafiki ambao binafsi siuhitaji sababu naheshimu ndoa yake na sitaki anisababishie matatizo.

Ushauri wangu kwa wanawake, msikimbilie kuolewa wakati nafsi zenu hazipo tayari kufanya hivyo.Hakikisha unaolewa na mtu ambae umemridhia ili kesho na keshokutwa utulie na ndoa yako na uache mambo ya kuhangaika na wanaume wengine ambao hakuna chochote cha maana watakachokusaidia zaidi ya kukutumia tu na kukutupa.

Huu ni ushauri wa bure.
 
Kwa hiyo kama mtu hapati mahitaji yote

Kurukaruka ruksa.

Mie kuflirt siachi ng'oo
Sijaamnaisha hivyo, ndio maana nikasema mwishoni kwamba olewa na mtu amabe umeridhika nae kwa kila kitu ikiwemo mali mana kuna wanawake wanapenda wanaume wenye uwezo.
 
Sijaamnaisha hivyo, ndio maana nikasema mwishoni kwamba olewa na mtu amabe umeridhika nae kwa kila kitu ikiwemo mali mana kuna wanawake wanapenda wanaume wenye uwezo.
Binadamu siyo nguzo.

Leo mnaoana kwa furaha na bashasha,
Miaka kadhaa anabadilika na kuwa mtu wa tofauti kabisa.
Wanaocheat wacheat ni kwa sababu zao binafsi na mostly ni kutoka kwenye nafsi zao yakakolezwa na external force.

Wasiocheat Mungu awabariki.
 
Kwa hiyo kama mtu hapati mahitaji yote

Kurukaruka ruksa.

Mie kuflirt siachi ng'oo

Hiyo ni selfishness ya hali ya juu kutoka kwa decent woman.

Sasa ukishikwa au kupata mimba ya nje ndoa ikawa sio ndoa,hapo unaumiza WATOTO wako wewe mwenyewe!

Ni heri uache kuokoa WATOTO wako.Usifikirie sana kujiridhisha wewe,kumbuka una watoto!

Na ukiachika utakuja kugundua kua wanaume ni walewale hamna mwenye tofauti na mwingine.You are just chasing the ghosts!

Kumbuka mwanaume na mwanamke ni tofauti,usije jifanya unashindana na mwanaume au mwanamke,ndoa ikifa consequences kwa mwanamke ni kubwa mnoo psychologically.Kwa watoto ni hatari zaidi!

Chagua kusuka au kunyoa mama!
 
Imemikumbusha shost yangu kilichomtokea. Mume wake alikwenda Ujerumani safari ya kizazi. Ni dada baada tu ya kumshusha hubby Airport alitupigia simu mamemba wa club ili Ijumaa tukayarudi.

Tulikuwa na dereva ambae tulihakikisha hapigi pombe alitushusha wote kila mtu nyumbani kwake

Tumefika kwa shost tunamkuta mumewe yuko barazani anamsubiri, pombe zote zilikwisha alikuwa sober

Kumbe mumewe alihitajika haraka kazini na safari kufupishwa ghafla.
 
Hiyo ni selfishness ya hali ya juu kutoka kwa decent woman.

Sasa ukishikwa au kupata mimba ya nje ndoa ikawa sio ndoa,hapo unaumiza WATOTO wako wewe mwenyewe!

Ni heri uache kuokoa WATOTO wako.Usifikirie sana kujiridhisha wewe,kumbuka una watoto!

Na ukiachika utakuja kugundua kua wanaume ni walewale hamna mwenye tofauti na mwingine.You are just chasing the ghosts!

Kumbuka mwanaume na mwanamke ni tofauti,usije jifanya unashindana na mwanaume au mwanamke,ndoa ikifa consequences kwa mwanamke ni kubwa mnoo psychologically.Kwa watoto ni hatari zaidi!

Chagua kusuka au kunyoa mama!
Kwani nikiondoka kwa baba yao watoto wanakufa?
 
Kwani nikiondoka kwa baba yao watoto wanakufa?

Aisee!

Yaani hujui effect ya baba na mama kukaa mbali mbali kama familia na watoto wao?

Yaani hujui hilo mpaka makamo haya uliyofikia?

Unajua maana ya Broken Home?

Unajua matatizo yote dunia hii ya moral decay yanatokana na Broken Homes?

Aisee tuliza ubongo,usiingie kwenye ndoa kwanza,cheza weee ufurahi then ukishapata akili vizuri ndio uingie.

Otherwise moto utauona vizuri sana mkuu!
 
Ya wewe kucheat au kucheat na mimi?

Kama ya wewe kucheat haya

Ila kama ya wewe na mimi hapana,
Huwa napiga one night stand

One night stands?

Hiyo sio cheating?Tena kwa mwanamke?Aisee ni hatari sana!
 
Aisee!

Yaani hujui effect ya baba na mama kukaa mbali mbali kama familia na watoto wao?

Yaani hujui hilo mpaka makamo haya uliyofikia?

Unajua maana ya Broken Home?

Unajua matatizo yote dunia hii ya moral decay yanatokana na Broken Homes?

Aisee tuliza ubongo,usiingie kwenye ndoa kwanza,cheza weee ufurahi then ukishapata akili vizuri ndio uingie.

Otherwise moto utauona vizuri sana mkuu!
Ni kawaida tu hawatakuwa wa kwanza wala wa pili

Kwani mzazi mmoja akifa wanakuwaje?

Binafsi sijinyimi raha ya dunia kwa ajili ya mtu.
Moto nilishauona toka nimezaliwa na kwa sasa ni muendelezo tu
Wala sijali saana.

Mtu akiamua kuondoka aende tu akiamua kubaki abakie.
I live once no need to pretend
 
Nimependa sana mawazo yako Hornet ,ni very challenging hasa kwa jamii yetu hii iliyoathirika na maisha ya kuigiza zaidi
 
Back
Top Bottom