Wanawake siku hizi hamjui mapenzi mmebakiza wivu.

na wanaume wa siku hizi hawajui majukumu yao ya nyumbani. mtu anaondoka asubuhi kwenda kazini haachi hela ya mboga wala unga akirudi jioni anataka umpikie wali na samaki, seriously!

cpiki ng 'o
halafu Nasubiri aniulize swali
 
Wanaume wengine wanashindwa kubadilika na mazingira mtu anaelekea miaka 40 anataka kushinda vijiweni kama watoto wa 20's,kwa nini mke wake asinune...hajui maendeleo ya familia wala nini kazi kwenda kwa washkaji...
Kama haujajiandaa kukaa na familia usioe ishi na washkaji kijiweni..
Mkeo akienda sokon akichelewa dakika tano tuu maneno yanakutoka kama mlio wa injini ya mando nonstop...

Hahahaa haaaa uwiii nimecheka
 
Kwani wewe ndio unajua mapenzi au ndio kusema tu watu wakusikie kuwa umeongea kuwa wanawake hawajui mapenzi sema uliyekutana naye ndio hajui tu siyo wote na kama umeoa mke wako hajui ni huyo tu si wote yaani watu tunaenda offisin lakini muda wa kutoka job tunawahi home kwa sababu ya huduma tunayopata na wala sichelewi kurudi
ukipata mwanamke hajui mapenzi mfundishe ajue ili ulidhike tofauti na hapo unatafuta sababu ya kusaliti ndoa yako kwa kigezo cha kijinga kabisa
Wanawake wengi hasa walioolewa wamekosa ubunifu wamebaki na wivu, mnajua tu hamuwezi kazi ndo maana tukichelewa kidogo nyumbani mnanuna wiki nzima, ndoa/mapenzi kisiwe kigezo cha kumfunga mwenzio hata asipite kijiweni au kupata 2,3 na washikaji.
Tata Molembe.
 
Last edited by a moderator:
hivi ww kwann usiyaintroduce hayo maubunifu kwa mkeo? tatzo wanaume wengi na nyie hampendi kujiweka karibu na familia zenu.... kijiweni unaenda kufanya nini badala ya kuwahi home japo ukute watoto hawajalala. mnakeraaaaaaa!!!
 
Kwani ukimwambia tu kuwa hela ya mboga utapungukiwa nini au hautaitwa mwanamke au utaoza ya nini muishi kwa matatizo kwa vitu ambavyo havina msingi kabisa masiha ya ndoa mkiishi kama alishababu hamdumu wakati mwingine na yeyey anasahau kwa sababu na yeye ana mapungufu kama wewe
cpiki ng 'o
halafu Nasubiri aniulize swali
 
..wa hivi mzuri kweli nampikia vitamu mpaka afurahi mwenyewe..asipojishtukia atakua ana matatizo...
na wanaume wa siku hizi hawajui majukumu yao ya nyumbani. mtu anaondoka asubuhi kwenda kazini haachi hela ya mboga wala unga akirudi jioni anataka umpikie wali na samaki, seriously!
 
Definition ya wivu huo mzuri ambao ni ingredient ya mapenzi.

Wivu ni hisia zenye utandu wa hofu, zinazosababishwa na hali ya kudhani kuna ushindani wa kimaslahi katika suala zima la kimapenzi.

Hisia hizo zinaweza kujumlisha na maumivu yanayotokana na wasiwasi wa kuhisi hakuna uaminifu kati yako na mwenzi wako.

Kuna aina tatu za wivu:

1. Wivu wa mashindano. Hii hutokea pale ambapo kuna hali ya kushindana. Yaani kuna mtu mwingine anakuwa na lengo na mwenzi wako, hivyo unajitahidi kumbakiza kwenye himaya yako. Ukimuona naye moyo wako hautakuwa sawa.

2. Wivu wa kusingizia. Hii inamaana kuwa unakuwa unamtuhumu mpenzi wako kwamba ana wivu kupindukia, wakati ni wewe mwenyewe ndiye unayesumbuliwa na wivu.

3. Wivu wa kujidanganya kimawazo. Hapa unakuwa hauna imani na mpenzi wako, kwa hiyo ukikaa unakuwa na fikra kwamba mwenzio anakusaliti au anafanya yasiyopendeza, wakati hilo halipo.

Ukisoma kwa tafakari nzuri, unaona kuwa sababu zote za wivu ni kutaka kuendelea kumuweka mwenzi katika himaya yako au kutokutoa nafasi ya kumpoteza au kupoteza uwepo wake.

Kitaalamu, inashauriwa kwamba kiasi fulani cha wivu ni muhimu kwenye mapenzi. Sayansi ya saikolojia inatoa muongozo kuwa hisia zako za wivu zinaweza kukusaidia kukulinda kwenye uhusiano wako.
Faida za wivu ni kama vile kuongeza kiwango cha mawasiliano. Mpenzi wako akiwa anakuonea wivu, atakuwa anakupigia simu mara kwa mara, hivyo kusaidia kuwaweka karibu.

NB:
Hili ni somo refu linalohitaji thread mkuu...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom