KILAKA
JF-Expert Member
- Feb 15, 2014
- 374
- 127
Kuna rafiki yangu niliyemaliza nae chuo kikuu cha ardhi mwaka 2010, mimi na yeye wote tulikuwa tunasoma architecture baada ya kuhitimu rafiki yangu(jina lake naliifadhi) alifanikiwa kupata kazi katika kampuni moja hapa D'salaam, na muda haukupita sana kwani mwaka 2011 kwenye mwezi oktoba alifunga ndoa na mwanamke aliyempenda(jina naliifadhi).
Yule mwanamke aliyemuoa alisomaga mambo ya biashara na hata baada ya kuingia kwenye ndoa alikuwa akijishughulisha na mambo ya biashara wakati mume wake akiwa ameajiriwa, mambo ya biashara kwa yule mwanamke yalimuendea vizuri sana na akawa anapata pesa nyingi sana akamshauri na mume wake aache kazi wafanye wote biashara na yule mume kwa kufikiria kipato alichokuwa anakipata mke wake kutoka kwenye biashara akaamua aache kazi na wafanye wote biashara.
Haukupita mda mrefu sana ndoa yao iliyumba sana kiasi cha kwamba mwanamke akamwambia mume wake mimi na wewe basi, kuanzia leo tusijuane. Mwanaume(rafiki yangu hakuamini) akaamua kumpigia simu mama mkwe wake naye alijibu hivi alichosema mtoto wangu ndo hicho hicho na mimi nipo huko huko, kumbe ata nyumba waliyokuwa wakiishi ilikuwa ya mwanamke kwa hiyo jamaa ilibidi aondoke pale na arudishe mpira kwa goli kipa( aende nyumbani kwa wazazi wake).
Amerudi nyumbani kwa wazazi wake akiwa hana kazi na akiwa hajui pakuanzia.Ndoa ikawa imevunjika baada ya kudumu kwa miaka mitatu tu.