Wanawake punguzeni ubabe

Wanawake punguzeni ubabe

Vijana buana. .acha kumsaidia ujnga wa kujlaumu, mpe nguvu ya kuzidi kupambana na kutafuta ili ajipatie vyakwake. Lakini ni somo zuri sana kwa vijana wenzangu
 
Tatizo sio ubabe ila wanaume wengi siku hizi wanapenda kulelewa, mwanaume mzima na akili timamu utaongozwaje na akili ya mwanamke na umeambiwa wewe ni kichwa cha nyumba? Mnatakiwa kuwa strong kweli kweli kuongoza akili ya mwanamke wa sasa. Bila hivo mtaishia kulialia kila siku.
 
uzoefu unaonyesha kuwa ndoa ambayo mke ana pato kubwa kuliko mume haidumu na ikidumu inakuwa na migogoro mingi kwani kwa pato mke atataka amiliki nyumba na awe mwamuzi mkuu.
 
huyu bibie hakumpenda jamaa kiukweli... there is no way in a million years utafurahi kumuona mtu unaempenda akihangaika.. ila maskini akipata..........

maisha ya kuanzia chini kwenye mapenzi nayapenda sana though najaribu kupata picha kama mwanaume ndo angekua kafanya hivi ingekuaje! mpe pole muhusika, Mungu atamsaidia apate ujasiri wa kuanza 0 tena
 
uzoefu unaonyesha kuwa ndoa ambayo mke ana pato kubwa kuliko mume haidumu na ikidumu inakuwa na migogoro mingi kwani kwa pato mke atataka amiliki nyumba na awe mwamuzi mkuu.

sio kweli... napingana na wewe asilimia mia tano
 
1. Mwanaume kuongozwa na mwanaumke nyumbani lazima una matatizo (Mwanaume atamtawala Mkewe - Refer Eden)
2. Kwenye jamii yetu hii mwenye pesa ndio ana maamuzi - Hekima ya masikini haisikilizwi -Refer Proverbs.
3. Aliye nacho Huongezewa, na asiye nacho hata kile kidogo alichodhani kuwa anacho... atanyang'anywa.. Ajitahidi KUWANACHO
4. Mwanamke akikuzidi kila kitu, Hio imekula kwako (akuzidi hela, elimu, akili, sijui nini hio imekula) Pride at it peak
5. Mwanaume ndio kichwa cha Nyumba.. Ukiangalia tu kirahisi hatuna taifa lolote masikini duniani lenye sauti ila yenye hela ndio yana sauti... Sasa wewe mkeo ndio kashikilia usukani unategemea sauti uitoe wapi?
6. Mtaji wake, kila kitu chake... Bila aibu unalaghaika unaenda kumkuzia mtaji... ona yatokanayo... hujaongeza hapo hata shs tano unasema biashara yetu... wewe na nani? Unawafahamu akina hawa au unawasikia? With all due respect I have enough back ups..... One or two among 20 ndio wanaweza kuwa na uwezo kifedha juu ya mwanaume bado wakajishusha... otherwise Money corrupts
7. Mwanaume always ni wajanja... huyu alilala.

Mhhh ... Hakika wanawake tuna sheeeda. Tumeoana wewe umeajiriwa mm nafanya biashara baada ya 2 years biashara imependeza imekuwa maradufu kumbe inakuwa imekula kwako Tized dahhhh sasa ulitaka nikifanya biashara isifanikiwe au? Kuna vitu vinakuwa judged in a very wrong way....
 
uzoefu unaonyesha kuwa ndoa ambayo mke ana pato kubwa kuliko mume haidumu na ikidumu inakuwa na migogoro mingi kwani kwa pato mke atataka amiliki nyumba na awe mwamuzi mkuu.
So what is your suggestion, conclusion and the way forward?
 
mpaka ufanyiwe ubabe na mwanamke huwezi kumu handle kabisa atakusumbua
 
DUUU, Siwezi kumlaumu sana mume, huenda aliamini maneno aliyoambiwa ''MMEKUWA MWILI MMOJA''. Suala la kuachana sioni tatizo, mke angefanya uungwana wa kumpa kianzio cha maisha.
 
Tatizo sio ubabe ila wanaume wengi siku hizi wanapenda kulelewa, mwanaume mzima na akili timamu utaongozwaje na akili ya mwanamke na umeambiwa wewe ni kichwa cha nyumba? Mnatakiwa kuwa strong kweli kweli kuongoza akili ya mwanamke wa sasa. Bila hivo mtaishia kulialia kila siku.

Hakuna mwanaume mwenye uwezo wa kumuongoza mwanamke, wanawake wana hekima, ujanja na ulaghai. Mwanamke mara nyingi huamua kujishusha ili maisha yaende. Wanaume ni JASIRI uwanja wa vita lakini si ktk uwanja wa mapenzi.Kumbuka ya Samsoni na Delila au ya Adam na Eva na tunda la katikati.
 
Watu wengi wana underestimate 'power of a woman...'

Nadhani ni kwenye kujipa moyo...

Wewe umenifurahisha sana kwa kuwakumbusha...

Hakuna mwanaume mwenye uwezo wa kumuongoza mwanamke, wanawake wana hekima, ujanja na ulaghai. Mwanamke mara nyingi huamua kujishusha ili maisha yaende. Wanaume ni JASIRI uwanja wa vita lakini si ktk uwanja wa mapenzi.Kumbuka ya Samsoni na Delila au ya Adam na Eva na tunda la katikati.
 
Hakuna mwanaume mwenye uwezo wa kumuongoza mwanamke, wanawake wana hekima, ujanja na ulaghai. Mwanamke mara nyingi huamua kujishusha ili maisha yaende. Wanaume ni JASIRI uwanja wa vita lakini si ktk uwanja wa mapenzi.Kumbuka ya Samsoni na Delila au ya Adam na Eva na tunda la katikati.

Hayo maandiko yamewekwa ili ujifunze. Hadithi inatolewa unaulizwa umejifunza nini, siyo muhusika alifanya makosa basi wewe ukafanye tena yale makosa.

Kuwa kichwa cha nyumba ni pamoja na kuongoza familia yako. Kama ingekuwa haiwezekani basi maandiko yangesema mwanamke ni kichwa cha nyumba.

Hata hivyo kama mmekubali kuwa mko weak, sasa yanini kulialia? Wacha mpelekeshwe maana kujielewa ninyi bado. Kwa taarifa yako mwanamke ni kiumbe dhaifu.
 
Hiyo ni ndoa ya utotoni. Mwanaume alikuwa hajakomaa hata kuishi na mke ndio maana hata baada ya maisha kumshinda karudi nyumbani,
 
Hayo maandiko yamewekwa ili ujifunze. Hadithi inatolewa unaulizwa umejifunza nini, siyo muhusika alifanya makosa basi wewe ukafanye tena yale makosa.

Kuwa kichwa cha nyumba ni pamoja na kuongoza familia yako. Kama ingekuwa haiwezekani basi maandiko yangesema mwanamke ni kichwa cha nyumba.
Kuwa kichwa cha familia hakutufanyi kuwa ndio ALFA NA OMEGA. Mwanaume anao wajibu wa kuunganisha Maono ya wanafamilia ili yaweze kuwa na matokeo chanya na katika hili kushauriana ni jambo la msingi. Kina mama sio viumbe DHAIFU, PENGINE DHANA hii ilitumika ili kuleta amani na maelewano kwani wahenga walisema, ''Mafahali 2 hawakai zizi 1''.
 
Sasa wewe umetoa details nyingi kiasi kwamba inakuwa rahisi sana kumjua huyo jamaa yako kama mtu akiamua kufuatilia. Jifunze kuficha ficha details.
 
Sasa wewe umetoa details nyingi kiasi kwamba inakuwa rahisi sana kumjua huyo jamaa yako kama mtu akiamua kufuatilia. Jifunze kuficha ficha details.

Mkuu hizo details nilizotoa ni za kawaida, bado nimeficha mambo mengi kama sehemu aliyokuwa anakaa na mkewe,kampuni aliyowahi kuajiriwa na nyingine nyingi.
 
Kuna rafiki yangu niliyemaliza nae chuo kikuu cha ardhi mwaka 2010, mimi na yeye wote tulikuwa tunasoma architecture baada ya kuhitimu rafiki yangu(jina lake naliifadhi) alifanikiwa kupata kazi katika kampuni moja hapa D'salaam, na muda haukupita sana kwani mwaka 2011 kwenye mwezi oktoba alifunga ndoa na mwanamke aliyempenda(jina naliifadhi).

Yule mwanamke aliyemuoa alisomaga mambo ya biashara na hata baada ya kuingia kwenye ndoa alikuwa akijishughulisha na mambo ya biashara wakati mume wake akiwa ameajiriwa, mambo ya biashara kwa yule mwanamke yalimuendea vizuri sana na akawa anapata pesa nyingi sana akamshauri na mume wake aache kazi wafanye wote biashara na yule mume kwa kufikiria kipato alichokuwa anakipata mke wake kutoka kwenye biashara akaamua aache kazi na wafanye wote biashara.

Haukupita mda mrefu sana ndoa yao iliyumba sana kiasi cha kwamba mwanamke akamwambia mume wake mimi na wewe basi, kuanzia leo tusijuane. Mwanaume(rafiki yangu hakuamini) akaamua kumpigia simu mama mkwe wake naye alijibu hivi alichosema mtoto wangu ndo hicho hicho na mimi nipo huko huko, kumbe ata nyumba waliyokuwa wakiishi ilikuwa ya mwanamke kwa hiyo jamaa ilibidi aondoke pale na arudishe mpira kwa goli kipa( aende nyumbani kwa wazazi wake).

Amerudi nyumbani kwa wazazi wake akiwa hana kazi na akiwa hajui pakuanzia.Ndoa ikawa imevunjika baada ya kudumu kwa miaka mitatu tu.

Mkuu mwambia Frendi wako wala asishtuke, sialiwahi kufanya ile biashara...hivyo afungue "the same bizness(trade) ili awe competitor wa Ex-wife, I am sure atamshinda na kumaliza kibiashara!!! just give a try !! or pM me..
 
msweet simaanishi ivyo!!! Nachokijua ni kuwa inahitajika juhudi binafsi sana kuweza kuzuia mafanikio yasikubadilishe... na haswa kwa wadada. Kuendelea kuwa mnyenyekevu na msikivu kwa mtu uliempita kila kitu ni NEEMA na kujitambua kwa hali ya juu sana na utambuzi kuwa mali na vyoote ni vikorombwezo tu.

Wanawake walio wengi ni rahisi kuwa influenced haswa wale wasio na utambuzi mzuri kinachopelekea baada ya kufanikiwa anaanza kuabudu alivyonavyo na mume hapo anakuwa ni ziada tu tena anaonekana msumbufu flani hivi na ana visheria sheria vya nini bhana wakati nikiwa mwenyewe naweza jihudumia kwa kila kitu na kwa chochote na kwa uhuru wote.... sijui kama naeleweka piacha nayoleta apa..

Inahitaji juhudi binafsi kuendelea kuwa wewe wakati wa mafanikio.

Mhhh ... Hakika wanawake tuna sheeeda. Tumeoana wewe umeajiriwa mm nafanya biashara baada ya 2 years biashara imependeza imekuwa maradufu kumbe inakuwa imekula kwako Tized dahhhh sasa ulitaka nikifanya biashara isifanikiwe au? Kuna vitu vinakuwa judged in a very wrong way....
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom