Wanawake ni viumbe wa kuheshimiwa

Wanawake ni viumbe wa kuheshimiwa

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
6,632
Reaction score
8,452
Japo inatambulika kuwa baadhi ya majukumu ni wajibu wao, ila endapo huo wajibu tungepewa sisi wananume, hakika ungetushinda.

1. Mwanamke anavunja ungo
2. Mwanamke anatokwa damu kila mwezi sehemu zake za siri
3. Kama asipotokwa damu basi anaujauzito ambao ataubeba miezi tisa
4. Mwanamke anajifungua kwa maumivu makali sana
5. Mwanamke anajukumu la kunyonyesha
6. Mwanamke anajukumu la kuhakikisha mtoto anakua salama
7. Mwanamke analea

Hayo ni baadhi ya majukumu ambayo ni lazima anayatimize. Tuje kwenye ambayo ameongezewa na hawa wanaojifanya walimtoa ubavuni.

Mwanamke akiamka asubuhi atafanya usafi wa nyumba, atafanya usafi wa nje, ataandaa maji ya kuoga mumewe, ataandaa kifungua kinywa cha mumewe, ataandaa nguo za mumewe, atafua nguo za mumewe, atandaa chakula cha mchana kama mumewe anarudi kula, ataandaa chakula cha usiku. Hapo bado wale wanaoenda na kazini kwaajili ya kuipiga tafu familia.

Hakika wanawake mna mioyo ya ajabu sana.
Nitawaheshimu mpaka naingia kaburini na nitawafundisha wanangu kuwaheshimu wanawake. Nyinyi ndo msaada wetu mkubwa. Bila ninyi, tusingeweza
 
'Mwanamke akiamka asubuhi atafanya usafi wa nyumba, atafanya usafi wa nje, ataandaa maji ya kuoga mumewe, ataandaa kifungua kinywa cha mumewe, ataandaa nguo za mumewe, atafua nguo za mumewe, atandaa chakula cha mchana kama mumewe anarudi kula, ataandaa chakula cha usiku. Hapo bado wale wanaoenda na kazini kwaajili ya kuipiga tafu familia.' haya ni wanawake wachache sana wanaofanya kazi wanaweza kuyafanya...
 
Na bado anadharaurika lakini anavumilia yote
'Mwanamke akiamka asubuhi atafanya usafi wa nyumba, atafanya usafi wa nje, ataandaa maji ya kuoga mumewe, ataandaa kifungua kinywa cha mumewe, ataandaa nguo za mumewe, atafua nguo za mumewe, atandaa chakula cha mchana kama mumewe anarudi kula, ataandaa chakula cha usiku. Hapo bado wale wanaoenda na kazini kwaajili ya kuipiga tafu familia.' haya ni wanawake wachache sana wanaofanya kazi wanaweza kuyafanya...
 
Nje ya mada.

Huwa tuna katabia ka kusema "Wamama wa nyumbani hawana kazi" ila nilijaribu siku kukaa nyumbani (wife alikuwa hayupo) na kufanya kazi zote anazofanyaga wife nyumbani aisee nilichoka , nikasema kumbe huwa tunawadharau bure tu hawa "Viumbe" wanaokaa nyumbani (hata kama kuna house girl) lakini kukaa nyumbani kulea watoto ni shuhuri nzito sana.

Hongereni Wamama wote mnaoitwa wa "Wamama wa nyumbani"
 
Sidhani kama hizi ni sifa za kupongezwa bali ni nature ya maisha.....ndivyo tulivyoumbwa.......

Ni sawa sawa na kumsifia mtu kula wakati ni process ya maisha na kula ni lazima ili uishi......


Sasa iwaje kumpongeza mtu kwa vigezo ambavyo MUNGU amemteuwa kuwa navyo.........
 
Mambo mengine ni nature.Kila kiumbe kina majukumu yake yakijinsia naiyo inatokana na biolojia yenyewe.Let it nature balance itself.
 
Sasa unataka tubebe mimba na kuingia hedhi sisi wanaume? Hayo ni maumbile,pia kazi zingine kimsingi zakwao,na sisi tuna misalaba yetu.
 
Sasa unataka tubebe mimba na kuingia hedhi sisi wanaume? Hayo ni maumbile,pia kazi zingine kimsingi zakwao,na sisi tuna misalaba yetu.
Robo tatu ya misalaba yetu wamebeba wanawake
 
Back
Top Bottom