mutant gene
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 876
- 326
hivi mtu unaamua kuoa, halafu unaishi na mke yako miaka tisa, mumezaa watoto 2, siku mnakorofishana anakuambia mtoto sio wako!! unaamua kuenda kuangalia DNA unakuta ukweli sio wako!! yani miaka yote ulikuwa unalea mke na mitoto ambayo sio ya kwako ambayo unajua ni yako !! hii ni true story imetokea rafiki yangu inaweza ikakutokea wewe mimi pia...usiamini kiumbe kinachoitwa ke hata usiku mmoja, bora upoteze pesa na muda wako mapema pale tu mtoto anakozaliwa kuepuka gharama zisizokuwa za kwako. Bora kulea watoto yatima huku ukijua kabisa ni yatima kuliko kulea mitoto ya kusingiziwa halafu baadae unakuja kujua sio yako!! inauma sana...kuwa makini na wadada wa mjini.