Wanawake na wanaume naombeni majibu

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,983
5,051
Fikiria kwamba umeoana na mwanaume/mwanamke na mnaishi kwa amani.

Ikatokea mmoja wenu hana uwezo wa kuzaa au kubeba/kubebesha mimba utafanyaje?

Mmehangaika sana bila mafanikio yoyote na umri ndio unakwenda hivyo.

Utamruhusu akaoe/kuolewa kwingine ili aendeleze uzao wake?

Utamruhusu azae na mtu mwingine na mtoto alelewe na nyie wawili?

Au utaamua tu nyie ndio muwe wa mwisho kwenye hicho kizazi cha uzao wenu??

Naomba tujadiliane kijamii zaidi kuliko kinadharia.
Karibuni ndugu zangu.
 
Last edited by a moderator:
Dini yangu ya uislamu inaruhusu mume kuoa mke mwengine. Lakini pia inatokea sana kua mume hazai na baada ya kuoa mke mwengine basi anazaa, hii sijui inakuwaje kibiologia
 
Dini yangu ya uislamu inaruhusu mume kuoa mke mwengine. Lakini pia inatokea sana kua mume hazai na baada ya kuoa mke mwengine basi anazaa, hii sijui inakuwaje kibiologia
kuna wanawake huwa wanachepuka na kukubambikia watoto.
lengo lake kubwa ni kuwa na wewe.
 
mkuu tuachane na hizo nadharia ambazo hata kitu kiidogo watu wanavunja ndoa.
Ndio msimamo/mtazamo wangu mkuu kwangu ndoa ni zaidi ya hayo na pia kama mtu hajakosa kizazi kwa maswala yake mwenyewe (kama abortion na magonjwa ya zinaa) basi ni kuacha mwenyezi Mungu atende kazi yake.
 
Mnaachana fasta, mme aende shule ya uPadre na mke uSista then mkimaliza mnaomba mpangwe parokia moja.
 
Ndio msimamo/mtazamo wangu mkuu kwangu ndoa ni zaidi ya hayo na pia kama mtu hajakosa kizazi kwa maswala yake mwenyewe (kama abortion na magonjwa ya zinaa) basi ni kuacha mwenyezi Mungu atende kazi yake.
ok nimekupata mkuu.
je, unadhani inawezekana katika jamii ya kawaida??
 
Mkuu, mie kwa ushauri wangu. Kama mna uwezo wa ku adopt mtoto mfanye hivyo lakini mjadiliane na kila mmoja aafiki kwa amani. Kutoka nje ya ndoa kutafuta mtoto ni issue na itawapa shida. Ni bora muadopt kisheria na huyo mtoto atakuwa wa kwenu...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom