Mama Sabrina
JF-Expert Member
- Jul 30, 2016
- 16,607
- 27,607
Wanawake mnapewa pesa za matumizi yaani mahitaji ya nyumbani wewe unachukua pesa unapeleka kwenye vicoba sijui marejesho.
Mara ulichukua mkopo Brac basi pesa ya matumizi inaishia huko, huku nyumbani unabakia kuhangaika kutafuta na kukopa pesa kwa watu za chakula mnavyofanya sio vizuri kabisa.
Wengine mnaingia huko kwenye vicoba hamna hata shughuli au biashara mnategemea peza za matumizi za waume zenu, inakuwaje uingie huko kwenye mikopo au vicoba halafu huna kitu cha kukuingizia pesa?
Kuna huyo mama kapata mgeni wanaishia kumuomba mgeni mara hiki mara hiki kisa tu pesa kapeleka kwenye vicoba, umeme unaisha inabidi mgeni anunue, wengine hadi ada za watoto mnapeleka huko.
Hivi hivyo vicoba imekuwa fasheni kiasi kwamba usipokuwemo ni vibaya mno, basi kuwa kibiashara ili usihangaishe watoto ukipeleka marejesho unatoa pesa kwenye biashara yako.
Kuna mwingine nae hapa kaniomba pesa sijui arejeshe huko kwenye vicoba vyao nimemwambia sina, mtu hana biashara unajiingizaje huko.
Mnakosea sana kuwa na kitu cha kukuingizia pesa ndio ufanye hivyo vicoba vyako na uchukue mikopo, mnachukua mikopo ya Brac roho zinakuwa juu juu hamna hata raha wala furaha.
Kina baba shtukeni pesa za matumizi zinapelekwa vicoba na kurejeshwa kwenye mikopo, watoto wanakuwa hawali vizuri.