Wanawake na message zenu mitanadaoni...!!!

Wanawake na message zenu mitanadaoni...!!!

Hamna kitu nachukia kama mtu anayeweka profile picture ya "vijembe" au whatsup status. Hata kama hanichambi Mimi.
Nikiwa nime save namba yako siku nikaona umeandika maneno ya ajabu ajabu, kama vile majungu majungu huwa naifuta ili nisione.
Ni ushamba na utoto na ulimbukeni.
Halafu subiri...! Inamaana na katika hili umeona wanawake tuu ndiyo huwa wanaweka hizo status za kijinga? Wanaume hawaweki? Au umemaanisha za wanawake tuu ndiyo zinakera? Za wanaume ni asali????????
Aisee basi uko tofauti na wenzio wengi....
Mara chache au hamna kabisa wanaume wanaochambana kwa style hiyo aisee...
 
Halafu mara nyingi wanaowekaga hizo status za kutupiana vijembe whatsapp wengi wao ni wale ambao wanaandikaga maneno kama mm, ww, ss, xx, umekura, umerara, umeludi, umelizika, et al

Kwanza mimi mtu akiandika maneno kama hayo kuna namna ambavyo huwa namchukulia hata kama kiuhalisia hayuko hivyo ninavyomchukulia na akitamka maneno kama hivyo (hayo manne ya mwisho) ndo kabisaaaaa

Punguza kurusha mawe Gizani, Mungu anakuona
 
Yaani kiukweli wanaoandikaga hivyo wanazingua sana

Ndio uhuru wa maoni na uwasilishaji, inaudhi yet mambo ya wakati,

Ya ujana na vijana muda wote pasua kichwa

Kwa conservatives ni mitihani mkubwa.
 
Back
Top Bottom