Wanawake na kudai talaka . . . . . . .

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,709
Ni kama wiki mbili hivi nimekuwa nikienda mahakamani kumsindikiza jamaa yangu mmoja aliekuwa anafuatilia mambo fulani pale mahakamani.

kila siku nilipokuwa naenda pale nilikuwa ninabahatika kusikiliza kesi kadhaa kabla ya muda wetu wa kuwa pale mahakamani kwisha,na hapo ndipo nikakutana nahili swali,
asilimia 80 ya kesi za kutaka kutengana kati ya wanandoa ambao wamepeleka kesi yao pale mahakamani ni wanawake ambao wanataka kuvunja ndoa hizo.Ni kwa nini?

Je wanawake wamechoka ndoa?
Je wanaume ndo sababu ya wanawake kudai talaka?Kamani hivi basi ni hatari sana.
Lakini nakumbuka kuna kesi moja mume alimuomba mkewe wakamalize tofauti zao kwa mchungaji na mkewe akamjibu kuwa "hata ungeleta wachungaji 10 hapa siwezi wasikiliza mi nataka talaka tu".

Huyu mwanamke na wengine wanaashiria nini?
Tatizo ni la wanaume au wanawake?
Kama ni la wanaume ni kwanini wanawake wasitumie busara kuyasuluhisha hukohuko nyumbani?
Kama ni tatizo ni wanawake je kutakuwa na ndoa siku za usoni kweli?
Nashindwa kuamini kuwa hapa ndo tulipo,nisaidie kujibu maswali hayo tafadhali
 
If the marriage is irretrievably broken the best course of action to take is to get a divorce and move on forward with your life.

It makes no doggone sense to hang onto a sinking ship. Just abandon it and keep it movin'.

Mhhhhhhh!!!!!!!
 
Naona sredi ya lara 1 imezua sredi mpya. So damn creative!

BTW hiyo 80% ilivopatikana...... I doubt! Labda mwanzisha sredi amehudhuria mashauri zaidi ya 100 mahakamani?

Ngoja niendelee kuwasoma.
 
Last edited by a moderator:
Shida kubwa inayozikumba mahakama ni hizi kesi za kipuuzi za watoto wadogo kuolewa na watu wazima tena ambao tayari wana wake wengine. Asilimia kubwa ya wanawake wanaodai talaka mahakamani madai yao ni kwamba wananyanyasika. Wakiulizwa wananyanyasikaje, hamna majibu
 
Naona sredi ya lara 1 imezua sredi mpya. So damn creative!

BTW hiyo 80% ilivopatikana...... I doubt! Labda mwanzisha sredi amehudhuria mashauri zaidi ya 100 mahakamani?

Ngoja niendelee kuwasoma.
Hii ni kwa mujibu wa kesi nilizohudhuria........
 
Dah hata mimi kuna moja naifahamu mume ni katili sana na mzinzi!! Mke alifungua kesi ya talaka mume akampigia magoti akilia 'mama fulani ukaumbuka kile kiapo cha ndoa... hakuna kuachana..' kweli mke alisamehe na maisha yakaendelea. Baada ya muda kusahaulika yule mume akaanza tema matimbwili yake na sasa mke alijenga nyumba yake kashabeba watoto na kuhamia!! Mume kabaki hana lolote na ile nyumba (matrimonial house) imepangishwa ili ada ya watoto ipatikane!! Sasa imagine mume na heshima zake leo hii anapanga na mke ana nyumba hawezi kanyaga pale. Ni firauni fulani hata ndugu wa mume wanamchukia ndugu yao maana mke ni mvumilivu mno. Kwa hiyo ukiona mwanamke anadai talaka kama hawara hahusiki jua amechoka!!! Hata akiwa na hawara kama nyumbani ni shwari talaka hakuna!! So wanaume kazi ipo.
 
wanaume ni wanyanyasaji wakubwa sana kwa wanawake utakuta mtu kajituliza jamaa ndio moto umepamba .wanawake mkitkla talaka mahakamani bila usumbufu semeni walikuwa wanataka kuwafira utapewa talaka yako fasta lol
 
Ni ukweli talaka zimeongezeka kwa sana.. Zamani waumini wa dini ya kikristo (ambao kwao talaka itoke pale tu itakapogundulika mmoja amezini nje) waliweza kuvumilia matatizo mengi ndani ya ndoa kwa kuwa dini iliwataka wacitengane.. Ciku hizi kutokana na utandawazi na mabadiliko na dunia kugeuka kama kijiji wengi wameacha kuishi kwa kufuata misingi ya vitabu vya dini vinavyosema.. (hapa namaanisha kwa wakristo bado maana nadhani acilimia kubwa ya kesi za talaka mahakamani zinawahusu wakristo maana waislam mara nyingi wanatumia bakwata pale panapotokea utata.. Ni wachache wanaoenda mpaka mahakamani)..

Uvumilivu ndani ya ndoa umekuwa mdogo sana ciku hizi.. Mie nimekua huku nikiona mengi ambayo mama yangu aliyavumilia ambayo sasa hivi hawa dada zangu niliozaliwa nao hawako tayari kuyavumilia..! Ninaamini aliokumbana nayo mama yangu kwa hawa mabinti wa leo zamani ndoa ingekuwa imeshavunjika..!

Ila wanawake kutokana na uhuru wanaoendelea kuudai unachangia kuondoa uvumilivu na maridhiano ndani ya ndoa..
 
Mi nahisi lazima kuna tatizo..!!

Mwanamke mpaka afikie suala ka kwenda kudai talaka mahakamani ujue ameshamvumilia sana huyo bwana imeshindikana ndio maana anaona ni bora tuu watengane..!!

Kwa wanaume wenyewe sio kwamba ni wavumilivu ndio maana hawadai talaka, la hasha.. Wenyewe mwanamke akisumbua tuu kidogo home ni rahisi kujitafutia liwazo la small house na maisha yakaendelea, kitu ambacho kwa wanawake sio rahisi sana..!!
 
Neylu una uhakika wanawake hawana mahusiano nje ya ndoa zao?
 
Last edited by a moderator:
Mwanamke kudai talaka ni kawaida kama hatimiziwi mahitaji yake, msisahau sex ni 1st priority :biggrin1:
 
Back
Top Bottom