Wanawake mtajiuga kwa presha...must read

Wanawake mtajiuga kwa presha...must read

MstahikiMeya

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2014
Posts
1,633
Reaction score
561
Mdada mmoja alitaka kujua kiasi gani anapendwa na mume wake, hivyo akataka kujua mumewe atafanya nini endapo ataamua kuondoka na kumuacha! Mwanamke huyo akaamua kuandika barua inayosema "Samahani mume wangu, nimeamua kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya
mbali na wewe" Barua hiyo akaiweka juu ya meza iliyokuwa chumbani.
Baadaye jioni, muda wa Mumewe
kurudi mwanamke huyo akajificha chini ya uvungu wa kitanda mule chumbani Mume alipoingia chumbani akakuta ile barua juu ya meza, akaisoma kisha, akaandika maneno fulani kwenye ile ile barua, harafu akaanza kuimbaimba kwa furaha huku akipiga miluzi na akiwa anavua nguo.
Akapiga simu na akasikika akisema hivi "hello mpenzi, nina raha sana leo.. yule mwanamke nuksi amesalenda mwenyewe kaondoka na kutuachia uwanja, jiandae nakuja" Muda huo huo Mume akaondoka.
Mwanamke alipokuwa uvunguni akawa anatoka lakini amenyong'onyea na amelowa mashavu kwa machozi.
Akasogea pale ilipo barua na akataka kujua mumewe aliandika kitu gani kwenye ile barua.
Akakuta maneno haya "nimeona miguu yako uvunguni, tafadhali andaa chakula nina njaa sana mumeo, ila nimetoka kidogo nafuata maziwa nilisahau kupitia.

Nakupenda mke
wangu"

MSPENDE KUJARIBU VITU VISIVYO JARIBIKA
 
Uwiiiiii!!!!
Hata hiyo nguvu ya kutoka uvunguni alikuwa nayo kweli?
 
hahahahaha weekend yangu itaisha vyema nimecheka sana..nahisi huko uvunguni nisinheweza kutoka duu..
 
Mi nilikuwa nshaanza kuishiwa nguvu ila mwishoni nguvu zimenirudia daaaahhh.
 
Back
Top Bottom