Wanawake mnatufanya kuwa wabinafsi

Wanawake mnatufanya kuwa wabinafsi

yuzazifu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2018
Posts
5,108
Reaction score
9,469
Natumai hamjambo wananzengo

Wakuu kuna hili suala la kuwashirikisha wake zetu katika kupangilia matumizi ya kipato cha familia, mara nyingi tunapopangilia huwa tunawakabidhi pesa za mipango husika ajili ya kutimiza malengo ya familia.

Ajabu pesa hizo hubadilishiwa matumizi bila hata kujuzwa sie yaani unajuzwa baada ya pesa kutumika, utasikia mume wangu samahani alipita chinga nikatumia pesa kiasi kununua kadha kadha.. mara mama juma aliniazima pesa kadhaa na hataki nilipa na nk.

Ukweli mambo haya hutukwaza sana na kuamua kuchukua maamuzi ya kua wabinafsi tukibaki kutoa matumizi pekee bila kuwashirikisha kitu ambacho huwafanya muanze kutulaumu bila kujua huo ubinafsi chanzo chake ni nyie wenyewe, naomba kuwasilisha.
 
Wewe toa, atatumiaje achana nalo, ili mradi ukirudi msosi upo unaoendana na pesa uliyotoa
 
Wewe toa, atatumiaje achana nalo, ili mradi ukirudi msosi upo unaoendana na pesa uliyotoa
itakua hujaoa wewe, pesa za matumizi na malengo ni tofauti mkuu, tatizo linakuja anapotumia pesa ya malengo kinyume na mpangilio
 
Kama humpi pesa za matumizi yake binafsi kubali matokeo kama hayo. Both team to score
pesa za matumizi binafsi anapata sema ni vile wanawake wanapenda show off kwa majirani kitu ambacho hupelekea kufanya mambo nje ya uwezo wao hata wakavuruga mipango
 
pesa za matumizi binafsi anapata sema ni vile wanawake wanapenda show off kwa majirani kitu ambacho hupelekea kufanya mambo nje ya uwezo wao hata wakavuruga mipango

Wanawake kawaida yao hata me nilikua naona mzee alilalama nikuwachukulia tu
 
Back
Top Bottom