Wanawake mna majaribu sana mjue...

Wanawake mna majaribu sana mjue...

Samcezar

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
13,096
Reaction score
22,826
Naomba nitoe ya moyoni.

Hivi mtu unakuwa na kazi yako ya kando, ina mtoto, huwa unapata shida kuwasiliana nayo kwenye whatsapp videos na hata social networking nyingine.

Sababu ni kuwa simu yake ya Samsung anayotumia ni zaidi ya kimeo, imefungwa na gundi tape. Kioo kina crack na ina michubuko haifai hata kumpa mtoto achezee maana inaweza muumiza.

Mwanaume unaamua ngoja uingie tu mfukoni, unakwenda dukani unachukua Simu mpya kabisa unamletea muhusika. Anafurahi sana anaipokea kwa furaha na unamsetia upya safi kabisa anaanza itumia wiki ya kwanza mnawasiliana vema sana na unapata raha ya mawasiliano.

Baada ya wiki anakupigia simu haumsikii vizuri sauti yake inatoka kwa mbali. Anakwambia simu mtoto alitumbukiza kwenye maji. Unamuelekeza bodaboda akaichukue aipeleke kwa fundi town ikatengenezwe. Baada ya kupelekwa kwa fundi na kusafishwa na kuwa sawa unamrudishia anakushukuru sana na mnaendelea kuwasiliana vizuri.

Baada ya wiki tatu simu unampata kwa shida, simu muda mwingine inaita sana. Kuja kufuatilia anakwambia kuwa chaji anayotumia inacheza na haingizi moto vizuri so muda mwingine anachaji kwa rafiki yake chumba cha jirani.

Unaamua siku unakwenda kumuona, unambebea chaja mpya, kufika unagundua chaja anayotumia sio chaja original uliyonunua na simu, bali ni chaja ya simu za mchina yaani Itel. Unamuuliza kwani chaja ya simu ipo wapi anasema kuna rafiki yake aliiazima hajamrudishia anasema imepotea.

Sawa haujali unampatia hii mpya uanataka kumuwekea unagundua simu imevunjwa screen kioo kina mistari ya nyufa. Unaamua kukaa kimya. Unamuwekea chaji mambo mengine yanaendelea.

Muda unakwenda siku kadhaa baadae. Haumpati, hewani kabisa siku nzima na hata online hayupo last seen ni two days......anakuja kukupigia jioni anakwambia anatumia kisimu cha tochi.

Siku unaenda unakuta anatumia kisimu cha tecno cha tochi na ni kibovu balaa. Simu uliyomnunulia anakuonyesha anasema haiingizi chaji na pini ya chaja imepinda sababu ilipinda alipoikalia kwenye kochi wakati inachaji so ikakorofisha kabisa haiingizi chaji.

Unaamua uipeleke kwa fundi mwenyewe, unaipeleka inatengenezwa maana kile kisehemu cha chaji kilivunjwa kwa kupindwa na pini ya chaja wakati imechomekwa. So fundi anatengeneza na likakujia wazo kuwa akupe pesa umuachie simu maana bado mpya kabisa.

Fundi anakubali anakupa pesa. Unaamua kumchukulia infinix maana ndio jiwe na atawezana nayo.

Unakwenda kuchukua unampatia bila kumwambia chochote. Anaichukua na kuanza itumia. Anafurahia sana simu mpya.

Baada ya mwezi m'moja wa utulivu, anakupigia simu unamwambia unataka kumuonyesha kitu so unapigia video call anakwambia ni wiki sasa hivi touch inasumbua akitaka kubonyeza back. Unamwambia angoje utakwenda kuiona.

Siku unaenda unakuta kioo tayari kimeshachezea manyufa ya maana.


Basi Mwanaume unaamua kuuchuna kama haujaona stroy zinapigwa unaaga unasepa.

Hivi wanawake waharibifu wa namna hii wasioheshimu pesa mtu unayowekea katika kumpa mahitaji yake huwa mnawafanyaje?!
 
Huwa unanikera tabia ya mtu mmoja kuifanya ya jamii yote, unaonekana una tatizo kimtizamo,

Hiyo ni tabia tu ya hicho kidemu chako,Kuna wengine tunajua kutunza Tena kitu ninunuliwe na mwenzi wangu nitakitunza mpk muda wake wa mwisho, na huwa vitu hivyo sigawi hata kikiharibika kinatunzwa.
 
Kiufupi tu naishia hapo sinunui kitu cha kuharibika tena maana huyo Ni mufilisi tena akifanya mchezo anachezea kadi myekundu fasta
 
Mbona unasumbuka nae sana kwenye swala la simu, acha atumie vitochi maana huyo ulimwengu wa smartphone hauwezi
 
Huwa unanikera tabia ya mtu mmoja kuifanya ya jamii yote, unaonekana una tatizo kimtizamo,

Hiyo ni tabia tu ya hicho kidemu chako,Kuna wengine tunajua kutunza Tena kitu ninunuliwe na mwenzi wangu nitakitunza mpk muda wake wa mwisho, na huwa vitu hivyo sigawi hata kikiharibika kinatunzwa.
Punguza hasira mama ametumia kauli akisema mademu wa aina hiyo wanafanywaje hivyo hajasema wanawake wote mpo hivyo mkuu punguza nyongo dawa iende kwa wenyewe labda watapona!!
 
Mwanamke ukimdekeza kuna siku atakushika makalio shauri yako, endelea kulia lia hapa badala ya kuwa Bold .
 
Huwa unanikera tabia ya mtu mmoja kuifanya ya jamii yote, unaonekana una tatizo kimtizamo,

Hiyo ni tabia tu ya hicho kidemu chako,Kuna wengine tunajua kutunza Tena kitu ninunuliwe na mwenzi wangu nitakitunza mpk muda wake wa mwisho, na huwa vitu hivyo sigawi hata kikiharibika kinatunzwa.
Na mbaya zaidi hajagundua kuwa tatzo ni yeye amekamatika na anaendeshwa
 
Huwa Tunaenda kwa waganga wanatutoa malimbwata tuliyolishwa maana ni ngumu sana kuwatendea hao viumbe hayo bila kinogesho! So changamka haraka ndugu yatakukuta makubwa..
Kwakweli ngoja tu nijikague
 
Huwa unanikera tabia ya mtu mmoja kuifanya ya jamii yote, unaonekana una tatizo kimtizamo,

Hiyo ni tabia tu ya hicho kidemu chako,Kuna wengine tunajua kutunza Tena kitu ninunuliwe na mwenzi wangu nitakitunza mpk muda wake wa mwisho, na huwa vitu hivyo sigawi hata kikiharibika kinatunzwa.
Nyie ndio wanawake wa kuoa kabisa... Mwanamke akiwa anatunza mali ninazomnunulia huwa napata nguvu za kiume sana kwake.... Naweza mpa chochote, hata mimba nampa.
 
Ukitaka mkeo adumu na simu basi usimzalishe, watoto ndio hua chanzo cha simu za wake kuharibika
Anawapa za nini?! Mimi simu hata niweke hapo mezani hakuna mtoto atagusa biti nitakalotangaza hapo ndani.... Wanachezea simu imekuwa toi.
 
Punguza hasira mama ametumia kauli akisema mademu wa aina hiyo wanafanywaje hivyo hajasema wanawake wote mpo hivyo mkuu punguza nyongo dawa iende kwa wenyewe labda watapona!!
Mtoto kaongea kwa hasira sana ila nikamuelewa kipande aliposema kuwa yeye ni mtunzaji...
 
Nyie ndio wanawake wa kuoa kabisa... Mwanamke akiwa anatunza mali ninazomnunulia huwa napata nguvu za kiume sana kwake.... Naweza mpa chochote, hata mimba nampa.
Kila la heri ukampate anaejua kuthamini jasho la mwanaume wake
 
Back
Top Bottom