Murete
JF-Expert Member
- Apr 11, 2016
- 246
- 102
Salaam mama zangu, dada zangu, wenzangu na wadogo zangu!
Tumshukuru Mungu kwa kuiona tena siku hii.
Nimerudi na uzii huu nia yangu ni kupata uzoefu (experience) kutoka kwenu kuhusiana na maswala ya ndoa baada ya kuolewa. Kwanza nianze kwa kuwapongeza wote mlio kwenye ndoa zenu. Wale ambao ndoa zimeisha kwa uwazi au kificho niwape pole. Naamini JF MMU ni kisima cha mawazo mapana na ya hekima. Hapa naomba mnipe hekima zenu ambazo zinaweza kuelemisha pia wadada wenzangu wanaotarajia kuolewa. Ni dhahiri ya kwamba mwanamke anaweza kuolewa akiamua tu.
Sasa natatizwa na mambo muhimu na ningependa kusikia kutoka kwenu. Je, maisha yanakuwaje ukiolewa na:-
1. Mwanaume uliyempenda kwa dhati
2. Mwanaume usiyempenda ila yeye alikupenda
3. Mwanaume mliyependana toka urafiki na uchumba
4. Mwanaume asiyekupenda ila akakuoa kwa sababu ya mimba, familia n.k
5. Mwanaume kwa sababu ya mali.
Kwenye jamii yetu haya yanatokea sana na kuna madhara na faida zake baada ya ndoa. Tafadhali hebu tupeni uzoefu wa mahusiano huko ndani ya ndoa yanakuwaje kutokana na aina ya ndoa. Wengine mtauliza kwanini nauliza kuolewa na mwanaume ila siku hizi kuna ndoa za jinsia moja.
Wanaume mnaweza kuchangia pia, tungependa kusikia toka kwenu. Ili uzi huu uwaelimishe wadada wanaotegemea kuingia kwenye ndoa sitegemei kejeli, dharau na matusi. Hapa kila mtu yuko nyuma ya computer, hakuna anayejua nani anaandika kwa hio maoni yako halisi ni muhimu kwa kujifunza. Tafadhali tupeane maoni ya kweli (genuine) kwenye swala hili.
Karibuni tuchangie. Asanteni