Wanawake mlioolewa na wanaume mliowazidi elimu, hali ya ndoa zenu ikoje?

Scorpio Me

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
6,119
7,933
Mambo zenu JF...

Kumekuwa na threads nyingi sana za kutafuta wapenzi but hiki kigezo cha elimu naona kinakuja juu sana especial kwa sisi wadada...
I know kuna wale wanaopinga kuwa elimu doesnt matter so long as mmependana...

Personally mwanaume anaponizidi kila kitu nafeel secured, kuanzia elimu, kipato, IQ...etc.....Nyie wadada ambao mko katika mahusiano or mmeolewa na wanaume mliowazidi elimu mahusiano yenu yakoje?

Wanaume mliozidiwa na wadada kielimu katika mahusiano hiyo gap ya elimu haijawaletea effect yoyote?

NB: Elimu nayoongelea ni ile mwanaume diploma mwanamke degree au mwanaume degree mwanamke masters etc...

Sio ile ya kupishana we uliishia la saba mimi la sita.
Leteni ushuhuda hapa.
 
Madam mahusiano is all about discipline baasi...
Ingekuwa mapenzi yanakuwa strong kwa kigezo cha elimu basi leo hii ndoa za maprofesa zingekuwa za mifano ya kuigwa!
Kuna binti mmoja namjua ni Captain wa JWTZ ila kaolewa na kijana ambaye ni kondakta wa dala dala na maisha yanaendelea vizuri,kikubwa ni kuheshimiana na kutambua kwamba ndoa na mahusiano ni taasisi inayojitegemea na yenye idara zake nyingi tu!
 
Wanawake waliosoma sana huwa jeuri sana kumzidi mume, hata kumsikiliza mumewe inakua ni kwa kiasi kidogo sana.

Wengi tendo la ndoa wanakuwa wananyima pia kwa kisingizio eti kachoka na mishe mishe za Kazini. Alafu ndo vile, ukimkoromea kidogo na kutaka kumzabua anatishia kwenda Kukushtaki. Shenzi kabisa.
 
Wanawake waliosoma sana huwa jeuri sana kumzidi mume, hata kumsikiliza mumewe inakua ni kwa kiasi kidogo sana.

Wengi tendo la ndoa wanakuwa wananyima pia kwa kisingizio eti kachoka na mishe mishe za Kazini. Alafu ndo vile, ukimkoromea kidogo na kutaka kumzabua anatishia kwenda Kukushtaki. Shenzi kabisa.
kweli raha kupitwa na mwanaume kila kitu
 
Mwanamke ukiwa na elimu kubwa kuliko mumeo/mpenzio mnaweza kuishi na mkaendelea vema kabisa ila tatizo wakaka huwa na wasiwasi au kujishtukia fulani. Mimi nilishapitia huku, ukimwambia kitu (kwa mfano unamrekebisha) hata kwa upole na upendo anasema unajiona kwa sababu umesoma. Ila wapo waelewa unaoweza ishi nao vizuri tu ili mradi upendo na heshima viwepo. Hiyo ndio misingi.
 
Back
Top Bottom