Wanawake, kwanini mnaacha vitu vyenu mkitutembelea?

Girland

JF-Expert Member
Jan 24, 2016
1,826
2,843
Aliyesema tuishi na mwanamke kwa akili hakukosea, Hawa viumbe wana mbinu nyingi za kivita Leo nawaletea hii moja iko hivii

Kuna mbinu imezuka mtu anakutembelea akitoka anaacha chochote, Hereni /khanga /Kyupi 😀😀

JAMAA YANGU ALALAMIKA, baada ya kuzagamuana na mrembo X, hakujua Kama aliacha hereni zake ndani kwake! Siku alivyokuja "main mazahausi tubii" akaanza kufanya usafi, timbwili likaanza. Alikutwa na ushahidi 😀😀😀

MIMI NILIKOSWAKOSWA, siku moja nilishangaa kukuta nguo isiyo yangu, kwenye kabati nikashangaa! Kumuuliza mhusika anasema kwani kuna shida?

AU ni njia ya ulinzi kwamba Y akiacha vitu vyake hategemei, mwanaume wake kuja na mwingine?

Eti ladies wa MMU mnaacha kwanini vitu mkitutembelea?mnavisahau au vipi? 😀 mshawahi kusikia hilo? Na wazee wa masihara mshawahi kuachiwa vitu
 
Kuna wale wanaoacha sehemu usiyoijua. Halafu mwingine akija anaanzia hapo usipopajua na anagundua kuna mwenzake.

Ukiulizwa una mwanamke mwingine, jibu kwa akili. Kwasababu hakuna swali analouliza mwanamke bila kuwa na majibu.
 
Mie naendaga kwa Wifi enu nilimpangia huko. Kuna vitu vyangu nimeviset najua akija baharia mwingine lazima vihamishwe.

Kuna Suti zangu nimezitundika sehemu na juu kabatini nimeweka beg (briefcase) sasa nikienda huwa nakagua vumbi. Nikikuta hakuna Alama za vidole kwenye vumbi najua hakuna ngedere aliyekuja.

Na naendaga bila taarifa.
 
Tunaweka ulinzi shirikishi!
Kuna mmoja aliacha khanga kwa mwanaume, sasa demu wake na jamaa alivyokuja akamuuliza hii khanga ya nani?
Jamaa akajibu, “Ya kwangu navaa nikiwa nasikiliza taarabu” 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom