Wanawake kuweni wakweli na wanaume toeni ushuhuda

Wanawake kuweni wakweli na wanaume toeni ushuhuda

Ujanani.. tee age Nilishampenda mtu nilikuwa napenda kumuangalia tu, akiingiza neno nakimbia. Na wenye macho mazuri walikuwa wananimaliza sana
 
Najiuliza ikitokea siku wanawake wakaamua rasmi kuanza kututongoza wanaume sijui itakuaje,nahisi nitaitwa baba Huruma maana sijui kama nitaweza kuwatolea nje na aibu hizi.Unaanzaje kuikataa papuchi labda?
 
Daaah kuna mdada alanifuata live akaniambia ya moyoni alafu bila hiana nikamjibu very simple kwamba Sipo tayari kuingia kwenye relationship akaniambia naomba siku ukihitaji kuingia kwenye rlationship nimuambie.

Akaja tena baada ya miezi minne, nakumbuka that Day alilia sana akaniambia J najuta kukufahamu najibu kupoteza hisia but nashindwa.... Sito kusumbua tena.

Tulikuwa beach fulani baada ya yale maneno nilimwambia usijali utapata mwingine aliinuka akaondoka hakunitafuta tena.

Kwa niliyo pitia sasa i wish nikutane na mdada wa hivyo maana alionyesha kunipenda kwa moyo wake wote na sijui kwanini nili mkataa.

Mara ya mwisho alinitumia e-mail akaniambia yupo Canada akaniambia nimsalimie wifi yake nilijikuta machozi yanatoka hiyo iikuwa baada ya miaka 4....nilimtumia txt ya kumuomba mawasiliano mengine hakunipa mpaka leo hii.
 
Back
Top Bottom