Nguva Jike
JF-Expert Member
- Jan 22, 2018
- 1,298
- 1,875
Natumai mmeamka salama Tanzania yote!
Nimegundua mchezo hatari unaoleta mkanyagano na kung'atana katika mahisiano.
Mwezi uliopita niligombana na shemeji yenu kiasi cha kunyofoana nguo kabisa.Sikupata jibu kwanini tuligombana kiasi kile kwakuwa huwa hatugombani kijinga jinga.
Jana asubuhi akaja mtoto wa kike kagonga getini nikamfungulia akasema ametumwa moto na mama yake eti kibiriti chao kimelowa.Nikamwambia ingia jikoni kachukue.
Alivyotoka tu kuchukua moto mume wangu akaja nje huku anawaka maji yako wapi nikaoge sijajibu karusha kofi Mara teke nikaanguka chini nilikuwa na kanga tu uchi ukaonekana house boy alishuhudia.
Nikajiuliza hii balaa gani siku ya pili.Nikaingia jikoni nakuta harufu isiyo ya kawaida kuchunguza naona kipande cha ngozi kinaungua jikoni.Nikakitoa nikakizima moyo ukatulia.
Nikaenda mpaka kwao yule mtoto aliyekuja kuchukua moto.Nikamuita akaja nikamuuliza wewe jikoni uliweka nini akakana.Nilivyo mbana akasema nilipewa na mama nikiweke kiungue baada ya kuchukua moto.
Nikapitia Kwa mganga wa jirani nikamuonesha ile ngozi akasema ngozi hiyo mbaya ni ya kufarakanisha nyumba nzima.Nilipo mwambia mume wangu hakuamini alivyo mfuata yule jirani polisi walikuja gombea ugomvi huo.Polisi walimhoji yule jirani akakiri kweli alimtuma.
Ndugu zangu kuweni makini sana jikoni na majumbani kwenu Kwa wageni wasio wema.