Wanawake Kenya wajifunza karate ili kupambana na unyanyasaji wa kijinsia

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Vitendo vya unyanyasaji wa kijinsi ambavyo vinajitokeaza katika maeneo mbalimbali nchini Kenya vimewashawishi wanwake wa eneo la Korogocho lililopo Nairobi Kenya kutafuta njia mbadala ya kuzuia vitendo hivyo.

Wazee wa jinsia kike katika eneo hilo wameunda kikundi ambacho kitakuwa kikifanya mazoezi ya pamoja ya karate ili kuweka miili yao fiti ili hata wanaume wanapowafata kwa lengo la kuwaingilia kimwili bila ridhaa yao waweze kuwadhibiti.

Akielezea hali ilivyokuwa awali kabla ya kuweka kikundi hicho, Beatrice Nyariara alisema kwa kipindi kirefu wanawake wa eneo hilo wamekuwa wakinyanyaswa na wanaume na hasa vijana lakini sasa mambo ni tofauti tangu walipoanzisha kikundi.

“Hali sio salama sababu kabla hatujaanzisha kikundi kwa wazee kama mimi, wanawake wengi wazee walikuwa wakibakwa na vijana wadogo. Wanatumia madawa ya kulevya, pombe na wakirudi nyumbani hawajui kutofautisha wazee na mabinti wa kike,” alisema Beatrice.

Chanzo: Mo Dewji Blog
 
wanaongoza east africa kwa kupiga wanaume hao
 
Back
Top Bottom