wanawake kauli mbiu zenu bado zinasisitiza utegemezi

wanawake kauli mbiu zenu bado zinasisitiza utegemezi

fige

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2010
Posts
375
Reaction score
61
Ni kazi ngumu kwelikweli kujikomboa huku ukitegemea misaada.Jambo hili limedumaza sana maendeleo ya nchi zetu changa na hivyohivyo wanawake.

Hii kauli mbiu ya wanawake isemayo WANAWAKE WAKIWEZESHWA WANAWEZA kwa mtazamo wangu inaendeleza dhana ya utegemezi.

Nawashauri wanawake kujijenga kwenye kujiamini kwamba wanaweza kuliko kutegemea kuwezeshwa,siku zote akuwezeshaye lazima atatafuta faida binafsi kuliko faida yako wewe, kitu ambacho ki
taendelea kuwafanya wanyonge.

Napendekeza wakati mwingine mje na kauli mbiu inayoonesha dhamira ya kujiamini juu ya uwezo mlio nao, mbona mnaweza hata kabla ya kuwezeshwa !

Nawasilisha
 
Nategemea challenge toka kwa akina mama, kama niko wrong nakubali kupewa sababu ya kauli mbiu yenu.
 
Back
Top Bottom