Wanawake: Kama unampenda mumeo, mpende na mama mkwe

Wanawake: Kama unampenda mumeo, mpende na mama mkwe

Ninakubaliana na wewe wapo wamama wakwe kama hao. Lakini mimi naona mume ndiye mwenye jukumu la kuweka sawa mahusiano ya mama yake na mkewe. Ukiona mama ma mka mwama hawana mahusiano mazuri (ile live kabisa) ujue huyo MUME NI DHAIFU!

Kuna kesi nyingine naona hata wanaume zinawashinda teh kuna bi dada siku moja alichambana na ma mkwe wake yani wanatukanana matusi muda huo mme yupo chumbani na mke ma mkwe kakaa sebleni wanatukanana, ila jamaa kapiga kimya anawasikiliza.... Ma mkwe anamwambia yule dada "Kama mji umekushinda nipishe mie nikae", ma mkwe alikuja kumuona mjukuu kazaliwa akamwambia "na huyo mtoto akikua labda so mie" sijui what happened yule mtoto alikua anaumwa yani siku mbili mzima siku tano mgonjwa hadi akafariki
 
hapo ndo mwanzo wa kushikana uchawi...ndo hapo ntakapojifanya shetani limenipanda.. toa kichapo kiana.. baadae naomba msamaha nilikua cjui nitendalo..ila msg sent
 
Mhhhh!!!! Acheni tu! Bado aanze kuhisi mwanae amepata pesa!!! Mhhhh ukivaa makenze ni shiiiidah!!
 
hapo ndo mwanzo wa kushikana uchawi...ndo hapo ntakapojifanya shetani limenipanda.. toa kichapo kiana.. baadae naomba msamaha nilikua cjui nitendalo..ila msg sent

Kwakweli yale mtoto hata kama ndo ilipangwa iwe hivo, yule dada anaamini ma mkwe anahusika.....yani ye na ma mkwe wake ni maji na mafuta
 
Sababu za kumchukia ma mkwe huwa wanasema ni zipi?

Sababu kubwa ni Mungu mwenyewe alivyowaumba wanawake,wanawake wana asili ya kupenda kupambana wao kwa wao!kama unataka kulaumu yeyote katika hilo mlaumu Mungu aliyewaumba hivyo kama utaweza kumlaumu Mungu

Wanawake hata nyumbani kwao wanapambana na mama zao kuishinda mioyo ya baba zao lakini pia kama shida ni ukwe au tabia za wamama mbona almost husikii mwanaume anavutana na mama mkwe wake???unadhani mama wakwe wa wanaume ni malaika kwao???Ni vile wanaume hatuna asili ya kuvutana na wanawake ndio maana unaona mambo kwa upande wa wanaume yapo shwari.

Kwa hiyo kupenda huku kuvutana kwa wanawake ndio kunaleta mambo yote hayo,mama atataka kuthibitisha kwamba yeye ndio kamleta duniani umemkuta tu,na mdada nae atataka kumthibitishia mkwewe kwamba ye ndio mambo yote kwa maisha yaliyobakia ya mwanae!

Lakini katika haya niliyosema si kwa kila mahusiano,wenye bahati tunafurahia mahusiano mazuri kati ya mke na mama!
 
Mama mkwe sometime sio kabisa.
Kaka yangu kaoa ila mama huwa anaona kama yule binti anamtesea mwanae kumbe walaa limwanaume ndio linamtesa mtoto wa watu... but mama haachi kukaa upande wa mwanae.
OVYO. nimetumia mfano halisi sitaki panic

Hutaki longolongo. Ukweli bin ukweli hata kama ni upande wako. Wachache wa aina yako. Big up!

Niliwahi kumwambia mama yangu mdogo kwamba treatment kwa mkwe wake sio fair. Alikubali na akakubali kuondoka kurudi kijijini.
 
Sababu kubwa ni Mungu mwenyewe alivyowaumba wanawake,wanawake wana asili ya kupenda kupambana wao kwa wao!kama unataka kulaumu yeyote katika hilo mlaumu Mungu aliyewaumba hivyo kama utaweza kumlaumu Mungu

Wanawake hata nyumbani kwao wanapambana na mama zao kuishinda mioyo ya baba zao lakini pia kama shida ni ukwe au tabia za wamama mbona almost husikii mwanaume anavutana na mama mkwe wake???unadhani mama wakwe wa wanaume ni malaika kwao???Ni vile wanaume hatuna asili ya kuvutana na wanawake ndio maana unaona mambo kwa upande wa wanaume yapo shwari.

Kwa hiyo kupenda huku kuvutana kwa wanawake ndio kunaleta mambo yote hayo,mama atataka kuthibitisha kwamba yeye ndio kamleta duniani umemkuta tu,na mdada nae atataka kumthibitishia mkwewe kwamba ye ndio mambo yote kwa maisha yaliyobakia ya mwanae!

Lakini katika haya niliyosema si kwa kila mahusiano,wenye bahati tunafurahia mahusiano mazuri kati ya mke na mama!

Nyie reaction zenu ni kimya kimya, ma mkwe akiumwa unapiga kimya, akipata shida unapiga kimya..... Teh ndo tofauti yetu hiyo
 
Kuna mmoja kajalalamika hapa juz tu, kwamba mkewe anampenda sana mama yake kuliko yy,

Lkn zaidi ya yote hawa mama wakwe walio wengi wana tabu sana
 
Mama mkwe sometime sio kabisa.
Kaka yangu kaoa ila mama huwa anaona kama yule binti anamtesea mwanae kumbe walaa limwanaume ndio linamtesa mtoto wa watu... but mama haachi kukaa upande wa mwanae.
OVYO. nimetumia mfano halisi sitaki panic

Bora umekuwa mkweli na hujaegemea kwa kaka yako, wamama wanashida sana mama mkubwa wangu yuko hi yo hivyo kwa mkwewe, naonaga huruma sana kwa wifi yangu
 
Mmh yani mabinti tuna kazi jamani mwee. Kidume hadi ukiguse kwa mtima kikuulize " will you marry me " si kazi ndogo. Unatoka hapo fyuuu kwa mama mkwe, ghafla tu unaambiwa hatukutaki mweee. Na wakwe ukipelekwa unachunguzwa jamani, kuanzia miguu, macho, pua, unavyokata Tonge, unavyotafuna je ukimeza unatoa jicho teh. Ukikubaliwa kama umeshinda vile vita vya 4 vya dunia.

Naonaga vibinti vinavyojitahidi kupetipeti mama wakwe kupalilia uchumba. Utasikia mama anaumwa naenda kumpikia Mmh, hapo kajibebesha mijizawadi hata mama ake mzazi hajawahi kumpelekea pyee ( unofficial utambulisho tu hapo ). Hukawii kuja kusikia ghafla wakwe wanasema " kabila letu na lenu hawaoanagi ". Mmh mama vitenge ulivyoletewa na binti wa kabila lingine havijakudhuru kwani?

Tatizo lingine nahisi pande zote mbili tumeshajiwekea ile mentality " mama mkwe, mawifi na mka mwana hawaivagi ". Kwa hiyo tunajikuta tunaishi kwa kuviziana. Unasubiri akosee tu upate justification ya kumkomoa na wewe. Kumbe sometimes ni makosa ya kawaida tu ya kibinadamu, kama ilivyo kuwa kila mtu ana mapungufu yake. Ni kuvumiliana tu

Afu wakwe, mawifi it's time waelewe kuwa kijana akioa kuna Vitu vinabadilika jamani. Sasa hivi ana familia yake, majukumu yanaongezeka na kuna priority nyingine tena. Kwa hiyo akisema " nimekwama kidogo " subiri wiki ijayo muwe mnaelewa. Maana hamkawii kusema " kamlisha limbwata kijana wetu " eeh. Tena usiombe mumeo ndo awe Reginald Mengi wa ukoo weee. Apunguze tu kiasi cha hela nyumbani kwao, utajutra

Ingawa Kuna vibinti navyo Eeeeeh havifai hata kwa kuchemshia maji. Yani vina visa vya madenge tu muda wote. Havitaki mume asaidie ndugu zake na hata hao ndugu wakija hapo home watalishwa pitiku na ugali kila siku hadi wajute. Ndugu wakifika gubu tu, full kujinunisha kama kifutu

Mwisho wa siku msimamo wa kijana ndo unaweza ukaiokoa ndoa yake na mahusiano yake na familia yake. Kijana akianza tu kuyumbishwa, basi familia inakufa kabisa. Jamani Tupendane, Tuvumiliane na tuheshimiane.
 
Kuna binti aliletwa home miaka fulani kutambulishwa na Cazn angu mmmh hadi nkahisi huruma ma mkwe kamdiss akamalizia "Mke mwenyewe ana maziwa makubwa" bahati nzuri tu hawakuoana yule binti hata kama angeolewa maisha yake na ma mkwe na mawifi yangekua magumu labda kama wangehamia mbali.....siwezi kujudge uhusiano huo asee huwa kuna mambo mengi hapo kati
Mpendwa huyo binti mwenye maziwa makubwa yupo wapi?..Unaweza kunipa contact zake
 
Nyie reaction zenu ni kimya kimya, ma mkwe akiumwa unapiga kimya, akipata shida unapiga kimya..... Teh ndo tofauti yetu hiyo

vyovyote iwavyo,ndivyo tulivyoumbwa na Mungu mwenyewe,hivyo kamwe silaumu mtu,maana hata kama mtu hataki anajikuta tu kafanya hivyo,hata wewe ukiteswa na mama mkwe wako baadae unajikuta tu unamburuza mkweo kwa mwanao wa kiume wakati wewe ulichukia ulivyokuwa unateswa,yaani unajikuta tu kumbe ndio nature hiyo!acha maisha yaendelee
 
Hizi ni baadhi ya athari za kutojuana vizuri kabla ya ndoa...Btw sometimes ni vyema kuwekeana misingi ya ndoa yenu mapema kabla ya kuanza hiyo safari(a lifetime journey)
 
Huyo ma mkwe next time marufuku kuja kuuguza mzazi, kama anakuja aje tu kutembea ila wa kumuangalia mzazi awepo, afu duuuh ma mkwe anaingiaje chumbani kwa wanae?

Wewe mwenyewe mamamkwe mtarajiwa..
 
Kuna binti aliletwa home miaka fulani kutambulishwa na Cazn angu mmmh hadi nkahisi huruma ma mkwe kamdiss akamalizia "Mke mwenyewe ana maziwa makubwa" bahati nzuri tu hawakuoana yule binti hata kama angeolewa maisha yake na ma mkwe na mawifi yangekua magumu labda kama wangehamia mbali.....siwezi kujudge uhusiano huo asee huwa kuna mambo mengi hapo kati

Mmh mimi kuna shoga angu alichambwa na mama mkwe na wifi ake. Ni kazuri kale kabinti lakini kalivyochambwa Eeeh. Wifi akapiga "hivi yale masikio sijui tutamrembaje siku ya harusi ", mara andunje, mara nyonyo Mmh. Seriously ndo Vitu vya kumjudge mtu?
 
Mpendwa huyo binti mwenye maziwa makubwa yupo wapi?..Unaweza kunipa contact zake

Mpendwa kwa kuchangamkia tu fursa uko njema, nnachojiuliza hizi fursa unafanikiwaga au harakati za pimbi tu? Lol yule binti sijui hata yuko wapi
 
Back
Top Bottom