Wanawake: Kama unampenda mumeo, mpende na mama mkwe

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,269
Reaction score
25,309
Habari wakuu,

Kumekua na tabia kwa baadhi ya wanawake ya kupenda waume zao na kuwachukia wazazi wa kike wa wawaume zao.

Hii tabia imekithiri katika baadhi ya ndoa nyingi, wanawake hao wamekua wabinafsi sana, hawataki kuendeleza mahusiano ya mume wake na familia ya mumewe.

Mfano, unakuta mtoto huyo wa kiume ni tegemeo la nyumbani kwao au wakati mwingine sio tegemeo ila lazima atume kiasi flani cha matumizi nyumbani kwao, lakini mkewe akiona hivyo anazuia hataki pesa zitumwe kwa mama mkwe.

Wakati mwingine mama huyo anaumwa na anahitaji kuja kutibiwa kwa mwanae, lakini mwanamke anakasirika na kumwambia mumewe asije kupata matibabu nyumbani kwao.

Wanawake wengine wamekua wakigombana na mama wa waume zao bila hata aibu, lakini eti akiwa na mumewe anampenda. Wanawake wenzangu tujifunze kuwaheshimu mama wa waume zetu na tuwapende kama mama zetu.

Kama unampenda mumeo, mpende na mama mkwe

MUNGU AWABARIKI WOTE
 
Ahsante kwakutukumbusha shosti, mie nashindwa kuelewa vp mwanamme anaweza kumwambia mamake eti kaa huko huko utibiwe wakati matibabu mazuri yapo mjini? hawajui Hakuna kama mama? na ukimuona mwanamke hampendi mkewe ujue hata huyo mume hampendi na hana akili timamu....
 
Si kila wakati mke ni kulaumiwa kuhusu uhusiano na mama mkwe wake. Naona raha sana kama mke akipatana na mama yangu. Lakini lazima tukubali kuwa kuna akina mama mkwe ambao ni very intrusive kwenye ndoa za watoto wao. Wanamwona mke wa mtoto wao kama mfanyakazi, kidampa fulani wa kuamrishwa tu. That is unfair.

Mwenye uwezo wa kuweka mambo sawa ni mwanaume. Lazima awe na uwezo wa kupima kwamba mama yake kavuka mpaka na kumweka sawa.

Mara nyingi mama akimheshimu mkwe wake mambo huenda sawa japo wapo wanawake hata mama mkwe afanye nini yeye ni uadui tu. Kila ndoa na mambo yake. Kila ndoa ina DNA yake!
 
Kuna dada aliwahi kusema "wakwe wengine roho zao zimening'inia kama kamasi hata uwatendee nini hawabebeki" uhusiano wa mtu na mkwe wake sio swala la kuangalia upande mmoja
 
wewe umegusa ikulu... uhusiano kati ya mtu na mkwe wake ni relationship kama zingine, kuna saa hazi work! unachoweza kufanya ni kumheshimu tu kama mama yako, sio lazima umpende kama sio realistic! huwezi kupenda simply because unampenda mumeo, hayo mawili ni tofauti.
 
Kuna dada aliwahi kusema "wakwe wengine roho zao zimening'inia kama kamasi hata uwatendee nini hawabebeki" uhusiano wa mtu na mkwe wake sio swala la kuangalia upande mmoja

Ndiyo maana kila ndoa na DNA yake ! Binadamu wapo wa kila aina.
 
Nakubaliana na mtoa mada kuhusu umuhimu wa kumheshimu mama mkwe. Lakini kumpenda sio lazima kama nilivyosema hapo juu. Jamani kuna mama wakwe wabaya. Naweza kutoa mfano, utakuta umejifungua ma mkwe anakuja kukuhudumia kama mzazi. Mama mkwe hafanyi chochoteeeeee hata ile kumwambia mfanyakazi akusaidie kitu, yeye kazi kukaa kuangalia tv na kukutuma wewe mzazi wa siku 5 ukampikie chapati za kusukuma anajisikia kula leo, na hataki msichana wa kazi azipike. Mama mkwe anakataza usipikiwe supu, eti mzazi hapaswi kula nyama! utakuta unapikiwa ugali na nyanya chungu. Mama mkwe anapita chumbani kwako kisha anakuelekeza pale kabati lilipokaa halipendezi utoe upeleke wapi sijui... seriously? Mama mkwe anakuingilia cha kupika, anafukuza wafanyakazi basi ili mradi! Ukimkuta mkwe mswahili utajuta, hana mipaka na wewe ni mtumishi wao! Yataka moyo hawa watu, labda hujakutana nao ndo maana unasema hivyo! Unaweza ukaichukia ndoa usipoweza kupambanua kuwa huyo ni mkwe tu, hajakuoa!
 
Kuna binti aliletwa home miaka fulani kutambulishwa na Cazn angu mmmh hadi nkahisi huruma ma mkwe kamdiss akamalizia "Mke mwenyewe ana maziwa makubwa" bahati nzuri tu hawakuoana yule binti hata kama angeolewa maisha yake na ma mkwe na mawifi yangekua magumu labda kama wangehamia mbali.....siwezi kujudge uhusiano huo asee huwa kuna mambo mengi hapo kati
 
Huyo ma mkwe next time marufuku kuja kuuguza mzazi, kama anakuja aje tu kutembea ila wa kumuangalia mzazi awepo, afu duuuh ma mkwe anaingiaje chumbani kwa wanae?
 
Aisee kuna mdada alikuwa ananihadithia vituko vya mkwewe mie nilichoka kabisaaaa! kama movie! Mdada karibia apate wenda wazimu, mama mkwe, mawifi wamemkalia kooni. Aliomba safari kazini akaenda mkoani kwanza ndo wale jamaa wakaondoka pale home maanake...
 
Kuna binti aliletwa home miaka fulani kutambulishwa na Cazn angu mmmh hadi nkahisi huruma ma mkwe kamdiss akamalizia "Mke mwenyewe ana maziwa makubwa" bahati nzuri tu hawakuoana yule binti hata kama angeolewa maisha yake na ma mkwe na mawifi yangekua magumu labda kama wangehamia mbali.....siwezi kujudge uhusiano huo asee huwa kuna mambo mengi hapo kati

Lakini your cousin alikuwa na nafasi ya kumuweka mama yake kwenye nafasi yake (cutting her to size) na mambo yakaendelea. Labda hakuwa na nia dhabiti. Angemwambia hayo maziwa makubwa ndiyo raha yangu. Akiruhusu kuingiliwa mara moja kwenye maamuzi yake, watajenga tabia and it will never stop.
 
Nakubaliana na mtoa mada kuhusu umuhimu wa kumheshimu mama mkwe. Lakini kumpenda sio lazima kama nilivyosema hapo juu. Jamani kuna mama wakwe wabaya. Naweza kutoa mfano, utakuta umejifungua ma mkwe anakuja kukuhudumia kama mzazi. Mama mkwe hafanyi chochoteeeeee hata ile kumwambia mfanyakazi akusaidie kitu, yeye kazi kukaa kuangalia tv na kukutuma wewe mzazi wa siku 5 ukampikie chapati za kusukuma anajisikia kula leo, na hataki msichana wa kazi azipike. Mama mkwe anakataza usipikiwe supu, eti mzazi hapaswi kula nyama! utakuta unapikiwa ugali na nyanya chungu. Mama mkwe anapita chumbani kwako kisha anakuelekeza pale kabati lilipokaa halipendezi utoe upeleke wapi sijui... seriously? Mama mkwe anakuingilia cha kupika, anafukuza wafanyakazi basi ili mradi! Ukimkuta mkwe mswahili utajuta, hana mipaka na wewe ni mtumishi wao! Yataka moyo hawa watu, labda hujakutana nao ndo maana unasema hivyo! Unaweza ukaichukia ndoa usipoweza kupambanua kuwa huyo ni mkwe tu, hajakuoa!

Ninakubaliana na wewe wapo wamama wakwe kama hao. Lakini mimi naona mume ndiye mwenye jukumu la kuweka sawa mahusiano ya mama yake na mkewe. Ukiona mama ma mka mwama hawana mahusiano mazuri (ile live kabisa) ujue huyo MUME NI DHAIFU!
 
Aisee kuna mdada alikuwa ananihadithia vituko vya mkwewe mie nilichoka kabisaaaa! kama movie! Mdada karibia apate wenda wazimu, mama mkwe, mawifi wamemkalia kooni. Aliomba safari kazini akaenda mkoani kwanza ndo wale jamaa wakaondoka pale home maanake...

Watu wa hivo ni heri kuwapisha kwakweli, unawaachia mji
 
Lakini your cousin alikuwa na nafasi ya kumuweka mama yake kwenye nafasi yake (cutting her to size) na mambo yakaendelea. Labda hakuwa na nia dhabiti. Angemwambia hayo maziwa makubwa ndiyo raha yangu. Akiruhusu kuingiliwa mara moja kwenye maamuzi yake, watajenga tabia and it will never stop.

Bora tu wakiachana, watu wanajudge hadi size ya nyonyo ni shida, hao hata ukiwafanyia nini kwao ni kibaya tu
 
Mama mkwe sometime sio kabisa.
Kaka yangu kaoa ila mama huwa anaona kama yule binti anamtesea mwanae kumbe walaa limwanaume ndio linamtesa mtoto wa watu... but mama haachi kukaa upande wa mwanae.
ONYO. nimetumia mfano halisi sitaki panic
 
Back
Top Bottom