Wanawake hawahitaji vingi, ni nyama ya ulimi tu basi

kinyamkela mahaba

JF-Expert Member
May 4, 2022
1,181
1,574
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni takribani mwezi tangu nimeanza ku interact na huyu mwanamke kwa namna moja ama nyingine. Siku ya kwanza alinikuta mgahawani nakunywa supu ya utumbo, nikamkaribisha akakataa, kabla ya hapo pia nilikua navutiwa naye.

Siku ya 2 nikakutana naye club maeneo flani, nikawa nakula muhindi wa kuchoma nikampa hi nikamkaribisha akasema ameshiba. Na juzi juzi akanikuta nakunywa uji wa ulezi mgahawani alikuwa anapita, akaanza kunichekea chekea tu na viaibu aibu vya kike, nikajua hapa tayari.

Nikamnunulia uji ila na yeye akamuambia mama muuza anywe kwa niaba yake. Huyu babayake anajiweza na wana miezi 8 tangu wahamie mtaani kwangu. Ni royal family siyo kidogo.

Tukakutana club kwa mara ya 2 akanikuta na dance nimeweka chupa ya bia kichwani pasipo kuanguka, alifurahi sana. Kiwizi wizi nikaomba namba akachukua yangu.

Kesho yake tukakutana akanichekea chekea nikajua mambo byeee. Mtoto kanasa. Na akaniambia jana nilipendeza kwa code zangu. Nilinyonga tai, pensi, raba na cap ya mike kama Ronaldo vile acha tu.

Kweli issue ni nyama ya ulimi tu, nani alijua kama manzi kama huyu atajigonga kwangu??

Nyama ya ulimi jamani

NB; msisahau ucheshi
 
Duuuh
 
We kamilisha kazi ndio uje hapa na maelezo kamili, sio unakuja kutuambia vimatukio na hata hajawahi kukuambia kitu oote
 
Back
Top Bottom