Tumekusikia,tunaomba na nyie muache kutumia mihela na muda mwingi bar,kwenye nyumba ndogo zenu,muwe na vipaumbele kwenye maisha na kwa wale wenye ndoa,wajitahidi kuipa familia muda zaidi. Ndoa inajengwa na inaweza bomolewa na pande zote mbili. Ni hayo tu.
Na ndipo uhovyo wao unapodhihirika!
Hivi kwenye ndoa nako kuna ngono?Nauliza tu!!
Nwy wakulaumiwa ni hao wanaume kwa kukimbilia kuona na watu ambao hawakidhi yale wanayohitaji yoka kwa mke. Tangu uchumba we mtu hajakushauri ununue pazia jipya badala ya kwenda club mara nne kwa wiki unategemea nini? Mtu hajawahi hata kukushauri/ambia unaweza zaidi ya unayofanya unategemea nini kwake?
What you see is what you get. Ukiwa na mchumba/mpenzi anaejali leo tu jua hata kwenye ndoa atakua hivyo hivyo. Hawezi badilika na kuanza kufikiria kesho kisa tu umemuoa maana hiyo ni tabia ya mtu, tabia inayokua imemjenga na sio sawa na kujifunza kusonga ugali au kupiga nyumba deki.
Kuweka dada wa kazi hilo ni la wengi. . . mi hua nashangaa watu wengine wanaishi wawili tu hawana hata mtoto bado na bado eti wanaajiri dada wa kazi anaefanya kila kitu. Wakati wenyewe wanaweza wakafanya shughuli ndogo ndogo za kila siku kwa ushirikiano alafu labda weekend ndio wawe na.mtuwa kuja kusaidia usafi mkubwa au kufua. Ila sasa hii ili iwezekane mwanaume nae inabidi ashirike. . . na hapo ndio kaka zetu wengi msipoweza. Mkiombwa kusaidia mnasema "bora nikutafutie dada wa kazi" alafu mwenxio nae akiwa kama wewe akafikiaria na mimi "ngoja nimwachie kila kitu dada wa kazi " mnalalamika.
Kuweni mabadiliko mnayotaka kuyaona badala ya kudemand tu.
Umefafanua kidogo vizuri Lizzy,lakini faham kuwa kama mwanamke anajijua na anajua nguvu yake kwenye mahusiano au ndoa,anaweza kufanya mabadiliko makubwa sana,nguvu na fujo za wanaume kwa mwanamke anaejua yeye ni nani nikama mkate mbele ya chai.Wapo wanawake ambao wamegundua hili na wamelitumia kwa njia chanya na wameyabadili maisha ya familia zao,na wapo wengine wametumia kwa njia hasi,wamejinufaisha,ukikuta familia ina mama wa hovyo na kuna maendeleo jua huyo mke akijirekebisha familia hiyo itakua na maendeleo maradufu!
Duh!Tatizo Lizzy wanawake wengi ni fake,wanafake mpaka tabia,kwenye uchumba anajidai anajua sana malengo,kumbe hovyo!Halafu kumbuka kuwa mwanaume anapochoka mara nyingi anatakiwa atulizwe na apewe maneno ya kumrejeshea nguvu,haijalishi mwanamke yuko vipi,tatizo linakuja pale atakapopewa nyoka wakati yeye aliomba samaki!
yote hayo mnasababisha nyie nyie wanawake fake,ndio maana tunaenda kutafuta tulizo huko!!!Tumekusikia,tunaomba na nyie muache kutumia mihela na muda mwingi bar,kwenye nyumba ndogo zenu,muwe na vipaumbele kwenye maisha na kwa wale wenye ndoa,wajitahidi kuipa familia muda zaidi. Ndoa inajengwa na inaweza bomolewa na pande zote mbili. Ni hayo tu.
Hii ni freudian Defense mechanism ya "Rationalization"Inafahamika kuwa linapokuja suala la uimara na ubovu wa ndoa,kufu au kudumu kwa ndoa wanawake mara nyingi ndo wanakua na nguvu sana,sisi wanaume hapa hatuna ubavu.Hivyo basi mwanamke akiwa fake/mjinga nk, na ndoa au mahusiano huwa hivyohivyo.Siku hizi wanawake wengi ni hovyo ndo maana na mahusiano/ndoa nazo ni za hovyo,siku hizi wanawake hawataki majukum ya kike,wanajua ndoa ni kuzaa na kuwatupia watoto ma HG.Hawajui namna ya kumhudumia mume,huduma wanayoijua wao ni ngono tu,hawawezi hata kumshauri mume namna ya kubajeti matumizi ili angalau wapate ka jumba hata ka vyumba viwili,wao wanajua kubana hela ili wakanunue mawigi,skin jeans,vimin nk,kama ni mfanyakazi mshahara unaishia hukohuko na machinga watajazana nyumbani kwako kukudai hela ya rangi za kucha,khanga na upuuzi mwingi tu!Hawa ndo wanawake watakaotusaidia kusonga mbele kimaendeleo kweli?Ama kweli kwa mtindo huu ndoa nyingi zitakua za hovyo ka sababu ya uhovyo wa wanawake wa leo.WANAUME kazi tunayo!