BARAZA la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Kilimanjaro (Bawacha), limemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa, kuacha siasa na badala yake awaamuru polisi kuwakamata na kuwafikisha mahakamani watu wanaodaiwa kumtishia maisha mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema.
Wiki iliyopita, Tendwa alikaririwa na vyombo vya habari akimuonya Lema kutokanyaga kwenye kampeni za uchaguzi mdogo katika jimbo la Arumeru Mashariki, kwani angefanyiwa vurugu.
Tendwa alidia Lema alitoa matamshi ambayo yalionekana kuwakera wazee wa kimila wa kabila la Wameru (Washila) katika mazishi ya marehemu Jeremiah Sumari na hivyo wakamtaka akawaombe radhi kwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Kilimanjaro, Lucy Owenya, alisema kauli hiyo ya Tendwa ni ya kushangaza hasa ikizingatiwa imetolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye ndiye mlezi wa vyama vyote nchini na tena ni mwanasheria aliyebobea.
Owenya alimtaka Tendwa kuwaarifu polisi kuwapo kwa watu wanaodaiwa kumtishia Lema kama anao ushahidi, ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Alisema CHADEMA ni chama chenye usajili wa kudumu na kina haki kisheria kushiriki uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki bila kutishiwa na mtu au taasisi yoyote kinyume cha sheria; na kuongeza kuwa kauli ya Tendwa inalenga kukidhoofisha chama hicho.
Owenya ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum, aliongeza kuwa kutishia kuua kwa maneno ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria, hivyo Tendwa anawajibika kuwalinda viongozi wote wa vyama vya siasa kutokana na vitisho vya aina yoyote kwa kuwaripoti polisi mara moja kwa kuwa ana ushahidi na wazee hao waliotishia kumuua Lema.
Wakati huo huo, Bawacha imelaani mauaji ya raia watatu waliouawa na askari wa jeshi la polisi mjini Songea, mkoani Ruvuma, hivi karibuni na kudai kuwa vitendo hivyo visipodhibitiwa vitachochea uvunjifu wa amani kwani wananchi watakosa uvumilivu.