Wanawake Arumeru mashariki wampa onyo kali NAssari.

Jimbo la Arumeru mashariki lilikuwa takribani miaka 50 halina mbunge, kuna matatizo mengi ambayo bwana Nassary anahitaji muda kuya adress yote ila kwa maoni yangu ameanza vizuri kero ya maji almost inatatuka, ushuru wa kiuonevu umeondoka, shule madawati yanawekwa kwa fujo barabara korofi angalau zinajazwa vifusi sasa wanaolia kwa nn wasingelia miaka 50 iliypita wakati jimbo halina mbunge? Tuacheni unafiki na ushabiki hizi pilao za bure zisituharibie jimbo, kamanda nassary songa mbele tunakupa support kubwa!!
 
Ingekuwa kina mama wametembelewa na viongozi wa CHADEMA wanawake hao wangeitwa wanachadema, lakini wakitembelewa ni viongozi wa CCM wanaitwa wananchi/wanawake/wanaume na si wanaCCM sishangai maana kilichoandikwa ni cha wale ambao waliamini hawezi kuwaongoza ila Nassari nae amezidi Ashauriwe kuwa makini sasa hivi sio mtu wa mtaani analoongea linajulikana Tanzania nzima. awe makini viongozi na marafiki mumshauri huyu jamaa mbona hakuwa hivyo.
 
Nadhani ni ile kauli ya Mwenge wa CCM. Maana binafsi hata mimi sioni umuhimu wa huu Mwenge. Gharama ya kuuzungusha Nchi nzima haiwiani na miradi wanayozindua ambayo mingi yake sio endelevu na ingeweza kuzinduliwa na viongozi wengine wa mahala husika. Mwenge unaenda kufungua matundu ya choo cha shule... kweli! hao wakuu wa wilaya, wakurugenzi, madiwani, wabunge wa maeneo husika wanafanya kazi gani?
 
SSM mnahaha, kila kona mnanunua watu wa kuwapigia mbiu mara CUF, mara chama cha madatari hewa, mara akina mama arumeru, mara ma-editors wa baadhi ya media houuses, mara hili mara lile!!! Kubalini mmeshapoteza dira na dhima hamna tena.
 
kama wameongea na viongozi wa ccm ulitaka waseme nini tofauti na hayo? Siasa bhana, afu utakuta ni mama mmoja tu kachonga karatasi yake kaisoma afu mwandishi anasema wanawake wa arumeru. Waandishi na nyie punguzeni kuweka chumvi
 
Sasa wanawake wenyewe ni wa CCM na wanaongea na voingozi wa CCM, unatarajia watatoa kauli ya kumuunga mkono Nasari? Waache waendelee kutapatapa maana wao si wasemaji wa wanawake wote wa Arumeru Mashariki.
 
Kichwa cha habari kilipaswa kuandikwa " wanawake kadhaa wa ccm arumeru mashariki"


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Basi utawaona kina bagwell, zomba, tantawi, tume, e.t.c hapa ndo michango kibao... I wonder who pays them!!!! Au ndo ofisi ya pale upanga?
 
Sasa hao Wanawake Wasingetembelewa na VIONGOZI wa CCM Wasinge lalamika ? Au MPAKA viongozi wa CCM wafike...
 
Wanawake wa chama cha mapinduzi au wanawake wa Arusha? Ccm imeingiaje hapo? Nadhan ni ccm na siasa za maji taka, yaan wanawake wanachama na wakeleketwa wa ccm.
 
Hao ni wanawake wanachama wa ccm. Hao ni kawaida yao, tumewazoea, umbea ni jadi yao, wanahitaji kuhurumiwa na kila mjinga.
 
Kwa nini mwandishi anatumia uwingi wa wanawake wakati aliyesema hivyo ni mwanamke tena wa ccm. Hilo jimbo inaonekana bado linaiuma ccm. Wameru siyo wajinga kiasi cha kurudia makosa ya nyuma ya kuchagua chama kinachoelekea kaburini.
 
haa !wanaulilia mwenge ?

ila kwa sasa CDM wangeacha tuu mwenge uendelee hadi hapo 2015 wata kapo shika nchi
 
Sasa wanawake wa meru wanamlalamikia ccm juu ya mbunge wa chadema? Si wakamuambie wenyewe?
At least wanatambua kiti kilikuwa mali yao na hawakufanyia kazi ndo maana wakakigawa!
 
Hii itakuwa ni kwa hisani ya gazeti la uhuru, waache kuilaumu serikali iliyoko madarakani kwa miaka 50 "with emptiness", hafu wamlaumu dogo aliye mjengoni kwa miezi saba kweli? Propaganda nyingine bwana!!!!!
 
Back
Top Bottom