Wanawake Arumeru mashariki wampa onyo kali NAssari.

Wanawake Arumeru mashariki wampa onyo kali NAssari.

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
15,340
Reaction score
1,573
Wanawake Arumeru Mashariki wampa onyo Mbunge wao, Nassari la sivyo atajajuta

20/09/2012




Na Queen Lema, ARUSHA -- Wanawake wa eneo la Kisambare, Usariver, wilyani Meru mkoani Arusha wamesema kuwa kamwe hawatavumilia kauli za mbunge wa jimbo hilo, Joshua Nasari badala yake watalazimika kuingia barabarani kumpinga hadharani Mbunge huyo kwani kauli zake hazijengi hoja za kutetea shida za wananchi na badala yake zinachochea malumbano pamoja na migogoro huku wanawake wa Vijijini wakiwa wanakabiliwa na shida mbalimbali

Wanawake hao waliyasema hayo jana Wilyani humo wakati wakizungumza na Viongozi mbalimbali ambao waliwatembelea Kijijini humo sanjari na kuongea na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.

Walisema kauli za Mbunge wao siyo za kujenga bali ni kubomoa na kuchochea malumbano makubwa ambapo kwa sasa alipaswa kuwa anaongelea jinsi ya kutatua changamoto mbalimbali zilizomo kwenye jamii.

Wakasema Mbunge huyo anapaswa kujua na kutambua kuwa alipewa jimbo hilo kwa hasira kutokana na kukithiri kwa changamoto lukuki ambazo zimo kwenye jamii hasa za Wameru na kwa hali hiyo huu ndio muda muafaka wa Mbunge huyo kuhakikisha kuwa anatatua kero na wala sio kutoa matammko ambayo hayana tija na jamii.

Waliongeza kuwa kauli hizo zimekuwa na madhara makubwa sana hasa kwa vijana kwa kuwa mpaka sasa wapo baadhi yao wanaofanya makosa na kuvuruga amani, kwa visingizo vya Mbunge huyo, "tunachotaka kujua ni kuwa tunatatuliwa kero zetu lakini badala mbunge afikirie suala zima la maendeleo yeye anafikiria kuzima mwenge wakati sisi hatuna shida na mwenge na mwenge unapita lakini shida zetu hasa sisi wakina mama wa Nkoakirika hatujui hata majira ya saa sasa tueleweje kwani tukimbia CCM kutokan a na changamoto lakini hii ya sasa ni kali na kama huyu mbunge ataendelea hivi basi ipo siku matatizo makubwa sana yatatokea" waliongea akina mama hao huku wakilia.

Mbali na hayo, waliongeza kuwa nao viongozi wa siasa watakiwa kukumbuka ahadi mbalimbali ambazo wamezitoa kwa jamii hasa nyakati za kampeni kwani baadhi ya viongozi, hasa wa Mkoa wa Arusha wakishapata nafasi ya kuongoza basi wanakuwa na matamko ambayo hayana tija na badala yake yanasabahbisha baadhi ya vijana kukamatwa ovyo na Polisi.

Awali Katibu wa CCM Wilaya ya Meru, Langaeli Akyoo alikiri kuwa CCM ilikuwa na kasoro hali ambayo iliwafanya wananchama wake kukopesha jimbo la Arumeru Mashariki lakini kwa sasa chama hicho kimejipanga hata kwa Watendaji wa huduma zote za kijamii kuhakikisha kuwa wanatekeleza sera za wananchi.

Bw. Akyoo alisema, hasira ambazo ndio chanzo pekee cha wananchi kutoa kura kwa upinzani kwa sasa zitapunguzwa kwa kiwango cha juu huku jamii hasa za vijijini zenye mahitaji maalumu nazo zikiweza kupatiwa ufumbuzi wa matatizo yao kwani uwezekano wa kuwasaidia bado ni mkubwa sana.



Source:
wavuti - wavuti
 
Mwacheni avimbe kichwa wembe utampitia 2015.
 
Duh, hii kweli kali! Au ndo Mgema akisifiwa sana?
 
Hao kina mama ni wa chama gani?Mbona mm nakaa usa River sijasikia
hilo?Hatudanganyiki.
 
Hatoweza kutimiza ahadi yake kwa sababu viongozi wengi sana hua wanajinufaisha wao kwanza halafu ndio wawakumbuke wanaowaongoza..
 
Kumbe ni maoni ya wanachama wa CCM ambao hawakumpa kura.....then hiyo sample inachukua % ngapi ya wapiga kura wote?Too low!
 
Kichwa cha habari kilipaswa kuandikwa " wanawake kadhaa wa ccm arumeru mashariki"


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Dodo asijisahau. Kuna masuala mengine anapaswa kuwashirikisha viongozi wake kwa ajili ya ushauri, vinginevyo kila mara viongozi wa CHADEMA watakuwa wanamwombea msamaha.
 
Wanawake wa Arumeru, au ni wana-ccm wa jinsi ya kike Arumeru?

Kama kawaida, wanaongea kuhusu 'amani na utulivu.' Ningeomba maoni ya hao wamama kuhusu mjane wa Daudi Mwangosi na wanasema nini kuhusu polisi kuicha familia ya Daudi Mwangosi bila bread winner?
 
Kichwa cha habari kilipaswa kuandikwa " wanawake kadhaa wa ccm arumeru mashariki"


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

kwanza wanawake hao hawakumchagua Nassar, japokuwa awe makini na kauli zake. Lakinikwa hili la mwenge, kuna hoja ya msingi. mfano, pesa ya kukimbiza mwenge kwa jimbo la arumeru inatosha kununua vitanda vingapi vya akina mama wajawazito na magodoro yake? huoni kuwa kudi mwenge kuzimwa, ni kutoa fursa kwa baadhi ya mambo kufanyika yaliyokuwa yakishindikana kwa sababu ya gharama za mwenge?
 
nasari achukue hii changamoto na ajirekebishe.sio mwanzo mzuri kwake
 
Wanawake wa Arumeru, au ni wana-ccm wa jinsi ya kike Arumeru?

Kama kawaida, wanaongea kuhusu 'amani na utulivu.' Ningeomba maoni ya hao wamama kuhusu mjane wa Daudi Mwangosi na wanasema nini kuhusu polisi kuicha familia ya Daudi Mwangosi bila bread winner?

kaskazini ijitenge - Nassari akiwa arumeru jimboni
 
[/COLOR]]kwanza wanawake hao hawakumchagua Nassar, japokuwa awe makini na kauli zake. Lakinikwa hili la mwenge, kuna hoja ya msingi. mfano, pesa ya kukimbiza mwenge kwa jimbo la arumeru inatosha kununua vitanda vingapi vya akina mama wajawazito na magodoro yake? huoni kuwa kudi mwenge kuzimwa, ni kutoa fursa kwa baadhi ya mambo kufanyika yaliyokuwa yakishindikana kwa sababu ya gharama za mwenge?

kwenye red apo.Ni dhambi ya ubaguzi hiyo ndio maana mnasema kaskazini ijitenge.
 
[FONT=courier
Wanawake hao waliyasema hayo jana Wilyani humo wakati wakizungumza na Viongozi mbalimbali ambao waliwatembelea Kijijini humo sanjari na kuongea na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.

/COLOR][/UR



Hawa wanawake wa "Arumeru" watueleze haya;

1. Kauli na majibu gani hayo wanayo yasema?

2. Walishindwaje kumwambia Mh. Nassari hayo huku
wako naye hao Arusha hadi wakayaseme kwa
"VIONGOZI waliowatembelea"? tena ana kesi hapo hapo
Arusha?

3. Halafu kwanini waongee na wanachama wa CCM
pekee??!



Ushauri: Enyi wanawake wa "ARUMERU" dont make threats that you cant deliver..kama kuingia mitaani ndiyo suluhisho la hayo matatizo yenu ya "kauli" ambazo hata mnashondwa kuzitaja...ingieni tu, hamna hata haja ya kutoa vitisho.!! mambo ya "mipasho" yaacheni huko huko "mnakopashana" mkiwatembelea hao "viongozi sanjari na kuongea na wanachama wa CCM"
 
Magamba wameshikwa haswa..

Sijui ni maendeleo gani wanayataka? Maana Mh. Mbunge anatenda kwa maneno na vitendo.

MAJI NI UHAI...Leganga na Shule ya Muungano


WATAPAMBANA, LAKINI HAWATASHINDA..WATASHINDANA, LAKINI HAWATASHINDA
 
Nimekaa nasoma siona hata hiyo kauli ya Nassary wanaoipinga, waandishi wa habari bana!
 
Back
Top Bottom