Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,300
- 33,919
Hii tabia ya wanawake ya kuzaa na mtu halafu kukataa kumpa mtu huyo mtoto wake, na badala yake kumchukua mtoto huyo na kumpa jina la ukoo wa mwanamke huyo ni ya hatari sana. Mtoto anapokuwa mkubwa anajikuta kwenye mtatiziko wa kisaikolojia kuelewa hasa kimetokea nini yeye kufanana jina la ukoo na wajomba na mama zake. Jee mama yake alizaa na ndugu yake?
Kama umezaa na mtu mwache mtoto kama anataka kufuata jina ama imani ya baba yake afuate na siyo kusema eti hana baba ama baba yake hafai kuitwa baba. Mtu kazaa na Muislamu lakini analazimisha mtoto wake awe mkristo ama mkristo awe muislamu.