Wanawake acheni malingo katika maisha

mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
5,262
12,838
Katika maisha yetu ya Dunia hi kiumbe kike ni hatari akiwa anakuzidi elimu, urembo, pesa nk wanatesa wenzao kupitiliza ila naomba wakumbuke haya:

1. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 40, waliosoma sana na waliosoma kidogo, wote wanakuwa sawa tu, ni wakati huu majigambo ya certificates, diploma, degree, masters, PhD, hupotea kabisa. Ni katika umri huu, inawezekana mwenye elimu ndogo, akatengeneza pesa nyingi sana kuliko mwenye elimu kubwa. Waliosoma sana na waliosoma kidogo, wote wanakuwa sawa tu.

2. Kama ulikuwa haujui, ikifika umri wa miaka 50, mtu aliyesemekana kwamba alikuwa mrembo, na mtu aliyesemekana kwamba alikuwa ana sura mbaya, wote wanaanza kuwa sawa tu. Ni wakati huu, mikunjo usoni, vipara kichwani, mvi n.k, haviwezi kukwepeka tena.

3. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 60, watu wanakuwa wamestaafu kazi, aliyekuwa na cheo kikubwa na aliyekuwa na cheo kidogo, wote wanakuwa sawa tu. Ni wakati huu, hawa watu wanakuwa washikaji, wanaanza kukaa kijiwe kimoja, wanapiga story zenye idea zinazofanana, mara nyingi utawakuta makanisani au misikitini pamoja.

4. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 70, mwenye nyumba ndogo na mwenye nyumba kubwa, wote wanakuwa sawa tu, wote wanahitaji nafasi ndogo sana ya kukaa, kwa kuwa ni katika kipindi hiki, kuhamisha-hamisha vitu, inakuwa taabu sana. Mwenye ghorofa atapenda kukaa nyumba ya chini, kwa kuwa miguu yake inaanza kukosa nguvu. Ni wakati huu, watoto huwaachia nyumba na kwenda kuanza maisha yao, hivyo, nyumba huwa kubwa kuliko mahitaji.

5. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 80, walio na pesa na wasio na pesa, wote wanakuwa sawa tu, hata mwenye pesa anapotaka kutumia pesa zake, anakuwa hajui wapi pa kwenda, wote tajiri na masikini, hubaki nyumbani tu.

6. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 90, kulala usingizi na kuamka, vyote vinakuwa sawa tu, kwa kuwa hata ukiamka, unakuwa huna cha kufanya.

7. Kama ulikuwa hujui, baada ya miaka 90, masikini na tajiri, wote wanasubiri kifo tu.

Katika maisha, kama wewe ulidhani ni mtu muhimu kuliko watu wengine, kwa sababu either ya elimu yako, uzuri wako, nafasi yako kazini, nyumba yako kubwa na nzuri unayoishi, pesa au kipato chako kuwa kikubwa. Basi ulikuwa hujui tu, ila wee ni wa kawaida sana, hakuna mtu mwenye nafasi kubwa kuliko mwingine, ni suala la muda tu, hivyo tuishi kwa adabu.
 
Mara zote nasema wanawake wanapitia kipindi kigumu kwa sasa.

Sasa kuna sehemu anasema ukifika miaka 50 unakuwa na mikunjo usoni na kupata kipara. Sijawahi kuona kipara cha kike.
Kumbe amesema hivyo!! Hata sijasoma.

Mkuu unadhani wanawake wanapitia kipindi kigumu?!! We soma mitandaoni utajua ni jinsia gani wanapitia kipindi kigumu, hivyo wameamua hasira na stress zao kumalizia kwa wanawake.

Tunawaelewa, hivyo tunajitahidi kuwa nanyi karibu ili tusije kuwapoteza maana hali ni mbaya.
 
Imekuwa vita sasa kati ya me na ke naona kila upande unarusha mishale kwa mwingine.

NB: rudisha ile avatar yako ya kichawi.
Kumbe amesema hivyo!! Hata sijasoma.

Mkuu unadhani wanawaka wanapitia kipindi kigumu?!! We soma mitandaoni utajua ni jinsia gani wanapitia kipindi kigumu, hivyo wameamua hasira na stress zao kumalizia kwa wanawake.

Tunawaelewa, hivyo tunajitahidi kuwa nanyi karibu ili tusije kuwapoteza maana hali ni mbaya.
 
Sema wenzetu wa mtandao huu wana stress sana
Kumbe amesema hivyo!! Hata sijasoma.

Mkuu unadhani wanawaka wanapitia kipindi kigumu?!! We soma mitandaoni utajua ni jinsia gani wanapitia kipindi kigumu, hivyo wameamua hasira na stress zao kumalizia kwa wanawake.

Tunawaelewa, hivyo tunajitahidi kuwa nanyi karibu ili tusije kuwapoteza maana hali ni mbaya.
 
Mara zote nasema wanawake wanapitia kipindi kigumu kwa sasa.

Sasa kuna sehemu anasema ukifika miaka 50 unakuwa na mikunjo usoni na kupata kipara. Sijawahi kuona kipara cha kike.
Ni kwamba ametafuta mada ya kuwaponda wanawake amekosa, kaamua kucopy na kupaste hiyo ambayo ni general kwa jinsia zote
 
Back
Top Bottom