Kama ulikuwa hujui

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,537
27,073
NGOJA NIKUKUMBUSHE KIDOGO

1. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 40, waliosoma sana na waliosoma kidogo, wote wanakuwa sawa tu, ni wakati huu majigambo ya certificates, diploma, degree, masters, PhD, hupotea kabisa. Ni katika umri huu, inawezekana mwenye elimu ndogo, akatengeneza pesa nyingi sana kuliko mwenye elimu kubwa. Waliosoma sana na waliosoma kidogo, wote wanakuwa sawa tu.

2. Kama ulikuwa haujui, ikifika umri wa miaka 50, mtu aliyesemekana kwamba alikuwa mrembo, na mtu aliyesemekana kwamba alikuwa ana sura mbaya, wote wanaanza kuwa sawa tu. Ni wakati huu, mikunjo usoni, vipara kichwani, mvi n.k, haviwezi kukwepeka tena.

3. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 60, watu wanakuwa wamestaafu kazi, aliyekuwa na cheo kikubwa na aliyekuwa na cheo kidogo, wote wanakuwa sawa tu. Ni wakati huu, hawa watu wanakuwa washikaji, wanaanza kukaa kijiwe kimoja, wanapiga story zenye idea zinazofanana, mara nyingi utawakuta makanisani au misikitini pamoja.

4. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 70, mwenye nyumba ndogo na mwenye nyumba kubwa, wote wanakuwa sawa tu, wote wanahitaji nafasi ndogo sana ya kukaa, kwa kuwa ni katika kipindi hiki, kuhamisha-hamisha vitu, inakuwa taabu sana. Mwenye ghorofa atapenda kukaa nyumba ya chini, kwa kuwa miguu yake inaanza kukosa nguvu. Ni wakati huu, watoto huwaachia nyumba na kwenda kuanza maisha yao, hivyo, nyumba huwa kubwa kuliko mahitaji.

5. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 80, walio na pesa na wasio na pesa, wote wanakuwa sawa tu, hata mwenye pesa anapotaka kutumia pesa zake, anakuwa hajui wapi pa kwenda, wote tajiri na masikini, hubaki nyumbani tu.

6. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 90, kulala usingizi na kuamka, vyote vinakuwa sawa tu, kwa kuwa hata ukiamka, unakuwa huna cha kufanya,hapa masikini na tajiri, wote wanasubiri kifo tu.

7. Kama ulikuwa hujui, ukifa wadudu wakitafuna masikini na tajiri wanakuwa sawa tu.

Katika maisha, kama wewe ulidhani ni mtu muhimu kuliko watu wengine, kwa sababu ya elimu, uzuri, nafasi yako kazini, nyumba, au kipato chako kuwa kikubwa. Basi ulikuwa hujui tu, wewe ni wa kawaida sana, hakuna mtu mwenye nafasi kubwa kuliko mwingine, ni suala la muda tu.

Nimekaa pale.✍🏾
 
Ngumu kumeza hii labda nipite hivi...
JamiiForums2142472440.jpg
 
Ndo yale ya Aliyesafiri na Trekta na Aliyesafiri kwa ndege wote wamefika.
Utajiri ni mzuri ingawa tajiri na masikini wote sawa.
 
Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 40, waliosoma sana wanakuwa na kazi nzuri kama wanasheria wasomi wahasibu madaktari wahandisi lecturers maprofesa n.k na wanatengeneza pesa ya kutosha, wakati huo wasiosoma wanahangaika na kubahatosha maisha! ni wakati huu majigambo ya certificates, diploma, degree, masters, PhD, huonekana kabisa kwa kuwa elimu yako hukuwezesha kupata kipato.

2. Kama ulikuwa haujui, ikifika umri wa miaka 50, mtu aliyesemekana kwamba alikuwa mrembo, na mtu aliyesemekana kwamba alikuwa ana sura mbaya, wanabaki hivyo hivyo! Hakuna cha umri wala nini.Mwangalie Jenifer Lopez kisha mlinganishe na bibi wa huko kijijini bado urembo utajidhihirisha!

3. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 60, watu wanakuwa wamestaafu kazi, aliyekuwa na cheo kikubwa na aliyekuwa na cheo kidogo, wote wanakuwa sawa tu kicheo lakini si katika mafanikio! Aliyekuwa na cheo ataonekana na heshima yake itabako palepale kulinganisha na ambaye hakuwa na cheo! Mwenye cheo alikuwa anaoata mshahara mnono mf Rais mstaafu kwa hiyo lazima amejenga mijengo,biashara n.k hivyo hawawezi kulingana! Ni wakati huu, hawa watu wanaweza kuwa washikaji au la! Wala hawawezi kukaa kijiwe kimoja, wala kupiga story zenye idea zinazofanana,Mfano Bakhresa aliyekuwa mwenyekiti bodi ya Bakhresa group eti akae na mzee nani huko kijijini wanywe kahawa 😂

4. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 70, mwenye nyumba ndogo na mwenye nyumba kubwa, wote wanabaki hivyo hivyo hawawezi kuwa sawa.Wengi wanabaki kuwa tegemezi kwa familia kwa hiyo wajukuu na watoto utakuta wanaachwa kwa babu na bibi yao! Wengine wana wageni wengi.Mfano wahindi hata ukizeeka unaishi kwenye nyumba ya baba yako.Matajiri wanakuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi nyumbani pamoja na ndugu jamaa na marafiki.

5. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 80, walio na pesa na wasio na pesa hawawezi kuwa sawa!, mwenye pesa atabaki kuwa mwenye pesa,anapotaka kutumia pesa zake, anaamua kupanda ndege kwenda Massachusets kufanyiwa massage! Usijidanganye kwamba kuna uzee wa kushindwa kutumia pesa!

7. Kama ulikuwa hujui, ukifa wadudu wakitafuna masikini na tajiri sio sawa kwani wanaotafuna tajiri wanafaidi minofu 😄
 
Back
Top Bottom