We ndo umepaniki, kuja kulalamikia mawigi ya mwanamke, kama ulikuwa hujui sio mara zote wanawake wanajiremba kwa ajili ya wanaume hiyo ni psychology ya wanawake... They are competitive among themselves.
Hata ningekuwa nimelivaa wewe halikuhusu, hata liwe la kijani teh teh
Mawigi yanawasaidia sana,wengi nywele zao vipilipili zimejaa mmba
Umefanya uamuzi wenye akili
Teh teh..Yani sometimes unakuta msichana anageuka kuangalia upande mwingine ila wig limebaki straight tu..halijafwata direction ya kichwa...
Hii kitu niliisikia kwa mwanasaikolojia mmoja, eti women do things for their fellow women to see not men, hivi kumbe ni kweli!!
Mbona unajazba sana,imegusa moyo wako nini? Jamaa katoa ushauri tu wala hajakwambia wewe.Samahani kwa kuingilia mazungumzo
Teh teh..Douta siogopi gharama coz hazinihusu..Mama ako anajisimamia mwenyewe kwenye hilo..Bora weaves..Ila mawig ndo siyapendi kabisaHahaha kwa raha zetyuuuu na Halloween zetu
Daddy sema vizuri hupendi weaves au gharama za weaves. Maana leo kila mtu hapendi weaves eti daah
Hivi ushawahi kuwasikia men wanaambiana " washkaji yule demu pochi lake kali"? Mara nyingi tunasifiana na kupondana wenyewe. Kuna wanaume hata kutofautisha nywele za kawaida na weaves hawawezi let alone kujua bei
Teh teh..Douta siogopi gharama coz hazinihusu..Mama ako anajisimamia mwenyewe kwenye hilo..Bora weaves..Ila mawig ndo siyapendi kabisa
Hiyo sio 'competition' kama unavyofikiri bali ni utoto na kutojitambua
Au ndio unaficha kipilipili chako? Ungejua!! Kipilipili ukikiacha kinakufanya uonekane una mvuto zaidi kuliko wigi
Ni kweli kabisa mae, umenikumbusha chuoni my friend alikuwa ana weave inayofanana na nywele zake kabisaaa alafu ilikuwa inashonwa kiustadi huwezi jua km sio nywele zake, alipolichoka akalitoa kaka mmoja kwa masikitiko akamuuliza "aisee nywele zako zilikuwa zinakupendeza mnooo, why umezinyoa?" Akamjibu tu kuwa aliamua, tulicheka tukijua kinachoendelea!
Teh teh..Mpaka mtu unajiuliza hii ni sura au painting boardTena hilo la make up ni kimeo. Mkorogo, kope za bluu, lips za kijani, wigi jekundu hadi anatisha
Na kuna wanaume wanayapenda sana tena wanayagaramikia wao, babu jf siku hizi ni nipe nikupe balaa tupu, tuvumilie tu wajukuu zako ndio zama zenyewe hizi.