Elections 2010 Wanavyuo, wamefikia wapi?

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
49
Kuna hili sakata la wanavyuo kushindwa kupiga kura kutokana na vyuo kuchelewa kufunguliwa, mpaka sasa sijapata habari zaidi ya ile walipokwenda kwa waziri mkuu, je kuna kinachoendelea? na kama ikishindikana itakuwaje?, je suala hili kuna mkono wa siasa au ni bahati mbaya?
 
Tanzania full uoga, kama wahadhili walishindwa je wanavyuo wataweza, hio ndio imetoka bwana, ila shame on Tz Gvt.Mambo haya huwezi fanya nchi kama Ug, SA na kwingineko ambako wananchi wake wanatambua haki yao ya kidemokrasia.
 
Hapa ndipo wananchi wengi wana pigwa na butwaa kubwa maaana hawa watu wa Tume ya Uchaguzi wanadai walitoa muda wa kutosha kwa watu kujirudia kujiandikisha na ndipo hapo walipo panga mipango kabambe ya kuhakikisha wanapunguza makali ya wanavyuo na kura zao.

kwani walijua fika kuwa vijana wengi wa kizazi kipya hiki kinataka mabadiliko na ndio kama Mama Salma Kikwete alivyosema kwenye mmoja ya magazeti yetu leo kuwa VIJANA WENGI WA SASA WANICHUKIA CCM NA WASUPPORT UPINZANI - kwani alisema hivyo ni kuwa vijana wengi hawajui mazuri ya CCM na kuwasihii wazazi wa vijana hawa wa kizazi hiki kuweelewesha mazuri ya CCM,

Sasa kweli Mke wa Rais ameweza kuona alama za nyakati nakulijua hilo na muda ulisha tokomea, hili ni dhahili kuwa watafiti wetu wa REDET na SYNOVATE wakajipange upya na watupe tathimini yao tena maaana tiali hapo ni kuwa kuna mabadiliko yanatokea ila kuna watu hawataki kukubali kuwa mabadiliko yako njiani na yanatokea.

Kisheria hawa wanachuo wamenyimwa haki zao za kimsingi na hili jambo hao NEC ndio kabisaaaa wamegoma kulitolea ufafanuzi, haya kwa ushauri mzuri Kama CCM inaona itapoteza kura zao kwa wanavyuo basi wakawalipie waje wapige kura kule waliko jiandikishia na kuwarudisha makwao na ndivyo hivyo kwa CHADEMA,CUF na vyama vingine kwani Uchaguzi ni siku mmoja tu na kesho yake wanarudi makwao
 
Tanzania full uoga, kama wahadhili walishindwa je wanavyuo wataweza, hio ndio imetoka bwana, ila shame on Tz Gvt.Mambo haya huwezi fanya nchi kama Ug, SA na kwingineko ambako wananchi wake wanatambua haki yao ya kidemokrasia.

Mkuru hapa bongo,

Wananchi wanajua kabisa haki zao ila kuna tatizo kubwa sana la serikali kutumia vyombo vya dolla kuwakanyagia kati watanzania na kuwadhurumu haki zao, kwani watu wakiandamana wanapigwa risasi za moto na kuwekwa ndani which mean sheria za nchi hii bado zimetungwa kulinda maaamuzi ya wakubwa au viongozi walioko madarakani wanapindisha sheria kwa manufaa yao.

Wajua police wetu wa kutuliza ghasia huwa hawana upeo wa kutuliza ghasia wao ni kufuata order tuu basi watu wameandamana kwa mfano bila kibali waache waandamane mpaka mwisho na unawapa ulinzi kabisa at the same time unawachomeka mashushushu humo kwa maaandamano ili wakuchukulie details zote ile maaandamana yatakapoisha utajua wapi pa kuanzia kuwakamata wahusika wakuu na kuwapeleka mahakamani kwa makosa haya na yale ili washitakiwe, ila wao huanza kurusha mabomu risasi za moto hapo si ndipo ghasia unaianzisha, na ndipo watanzania wanapo ogopa hapo

Navyo fahamu mtanzania sio mtu wa vurugu kabisa ila ni vigogo fulani wanajihami ili wasije shtukiwa kuwa wanaivuruga nchi

Wengi ingawa sio wote nimewasikia wakijitayarisha baada ya wiki hii kwisha kwenda kupiga kura. Hasa wa UDSM wamejitolea kutopoteza haki yao.
 
Wengi ingawa sio wote nimewasikia wakijitayarisha baada ya wiki hii kwisha kwenda kupiga kura. Hasa wa UDSM wamejitolea kutopoteza haki yao.

Nadhani itakuwa vyema kuwaomba wanavyuo wooote wazalendo popote hapo walipo kusaidia kuokoa haki yao walionyang'anywa na hii Sirikali. Wajitolee kufanya kampeni walipo na kusaidia katika kulinda kura,kwenye maeneo watakayo kuwepo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom