Wanaume wenzangu tusifanye hivi

Official Amo

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
990
1,216
Unapoamua kuzaa na mwanamke, basi inatakiwa uwe tayari kwa majukumu ya kumlea mtoto ambae Mungu amewa jaalia kumpata.

Ukweli ni kwamba suala la malezi sio suala la kitoto, linahitaji sacrifice ya kutosha, kwa hiyo kitendo cha kuwakimbia wanawake na kuwaacha na viumbe huwa inakuwa ni jambo zito kidogo kwao.

Hali wanayopitia inakuwa ni ngumu sana na wanakuwa wanapitia changamoto nyingi sana, hii inapelekea kuwaza mambo mengi sana wanakuwa depressed sana, hata kihisia wanakuwa hawako sawa.

Japokuwa wao pia huwa wana changamoto zao zinazofanya inakuwa ngumu kuishi nao, ila suala la kuwakimbia na kuwaachia mizigo ya watoto linakuwa sio sawa hata kidogo.

Tunachukua maamuzi kama haya inabidi tuqngalie na upande wa mama na watoto pia, sio upande wetu tu, hata kama inaonekana wao ndio wenye makosa
20211025_150702.jpg
 
Lakini pia ukibeba mimba kabla ya ndoa jiandae kipsychologia kulea mtoto katika mazingira yeyote Yale wewe kama wewe bila kumtegemea mtu hiyo itakusaidia ata mwanaume akukimbie hutaathirika Sana mwanamke ndio mlezi ng'ombe halemewi na nundule kwanini mtoto akushinde
 
Alikua na watoto wawili, bila shaka alizaa na mtu mmoja ndani ya ndoa.
 
Unapoamua kuzaa na mwanamke, basi inatakiwa uwe tayari kwa majukumu ya kumlea mtoto ambae Mungu amewa jaalia kumpata.
Akina dada/mama wana sehemu yao kubwa ya uhusika.. Wanalazimishia sana mimba siku hizi.

Watu mpo kwenye mahusiano miezi 15 hamjawahi ona ujauzito, ile mpo kwenye confrontation inayoonesha kila dalili ya mahusiano kushindwa, unaambiwa mimba imetungwa! Halafu unatishiwa, nitamwambia mtoto ulimkataa.
 
Dah, Huyo jamaa ametukosea adabu kwa kweli. Anamuachaje Demu mkali kama huyu.

Ukiwa na mke mzuri ni budi kuvumilia tu kero zake huku unaendelea kufaidi mambo mengine
Acha kabisa bro.. Kero za mahusiano ni habari nyingine.. Unaweza pauka kuzidi nsyuka
 
Back
Top Bottom