Wanaume wenzangu tusifanye hivi

Akina dada/mama wana sehemu yao kubwa ya uhusika.. Wanalazimishia sana mimba siku hizi.
Watu mpo kwenye mahusiano miezi 15 hamjawahi ona ujauzito, ile mpo kwenye confrontation inayoonesha kila dalili ya mahusiano kushindwa, unaambiwa mimba imetungwa! Halafu unatishiwa, nitamwambia mtoto ulimkataa.
Umeongea point mkuu
 
Lakini pia ukibeba mimba kabla ya ndoa jiandae kipsychologia kulea mtoto katika mazingira yeyote Yale wewe kama wewe bila kumtegemea mtu hiyo itakusaidia ata mwanaume akukimbie hutaathirika Sana mwanamke ndio mlezi ng'ombe halemewi na nundule kwanini mtoto akushinde
Mahitaji ndio tatizo...unakuta binti ameshika mimba na hana kipato cha kutosha inamiwia vigumu kutimiza mahitaji ya mtoto , hivyo anabaki anajilaumu na kuhuzunika mwisho anapata msongo wa mawazo
 
Kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa ndiyo mwanzo wa matatizo yote haya - utoaji mimba, kuwa na single parents, mauaji, n.k. Kama jamii tunapaswa kubadilika.
Vipi na wale waliooana na bado wanachomana moto kwa magunia ya mkaa??
 
Pisi kali kama hii imekuwaje tena imeamua kukwama. Shida ni ulaya, ingekuwa bongo, huyu mchumba anawekwa ndani anaishi kama mwali bila kutoa mia, na watoto analelewa bila shida.
 
Unapoamua kuzaa na mwanamke, basi inatakiwa uwe tayari kwa majukumu ya kumlea mtoto ambae Mungu amewa jaalia kumpata.

Ukweli ni kwamba suala la malezi sio suala la kitoto, linahitaji sacrifice ya kutosha, kwa hiyo kitendo cha kuwakimbia wanawake na kuwaacha na viumbe huwa inakuwa ni jambo zito kidogo kwao.
Shauri yake. Kwani alipoamua kuzaa bila mpangilio alitegemea nini?
 
Inasikitisha ila hapa kuna fundisho mara mbili. (1) Unaweza kukuta mdada anaamua kuzaa tu na kibaka wa kitaa sababu ya tamaa ya kumiliki IPhone 13 au Samsung S21 wakati jamaa hana mpango naye, yeye anataka shoo tu kisha asepe zake. Huyu kibaka hata umsingizie kuwa mimba ni yake hana mpango nawe, utaishia kushinda kwa waganga tu kumrudisha akili akuwaze wewe.

(2) Hii ninaweza sema kidogo inaweza linagana na point namba moja maana unakuta wanawake wengi wanapenda kujiingiza mahala pasipo na pendo ili tu apate kutunzwa na mwanamme. Atajitahidi kujipendekeza hata kama hatakiwi, anaweza kujuwa jamaa ni kicheche ana mademu kila kona ila yeye atajipendekeza tu kwa jamaa kisa ana gari, hela, nyumba nzuri, kazi nzuri, mwisho wa siku anashika mimba ya jamaa bila matarajio, java anamtimua.

HAKUNA mwanamme anayependa kushitukizwa na ujauzito labda apange yeye mwenyewe. Ujinga huu wanao sana mademu wa kibongo haswa hawa macelebrity uchwara wetu.
 
Inasikitisha ila hapa kuna fundisho mara mbili. (1) Unaweza kukuta mdada anaamua kuzaa tu na kibaka wa kitaa sababu ya tamaa ya kumiliki IPhone 13 au Samsung S21 wakati jamaa hana mpango naye, yeye anataka shoo tu kisha asepe zake. Huyu kibaka hata umsingizie kuwa mimba ni yake hana mpango nawe, utaishia kushinda kwa waganga tu kumrudisha akili akuwaze wewe. (2) Hii ninaweza sema kidogo inaweza linagana na point namba
Haya matukio japo yanasikitisha lkn yakawe funzo kwao
 
Akina dada/mama wana sehemu yao kubwa ya uhusika.. Wanalazimishia sana mimba siku hizi.

Watu mpo kwenye mahusiano miezi 15 hamjawahi ona ujauzito, ile mpo kwenye confrontation inayoonesha kila dalili ya mahusiano kushindwa, unaambiwa mimba imetungwa! Halafu unatishiwa, nitamwambia mtoto ulimkataa.
Yamenikuta hayo hayo au wewe ni mimi?
 
Yamenikuta hayo hayo au wewe ni mimi?
😂😂😂😂😂
Acha kabisa!! Unawekwa kwenye majaribu magumu ya kufanya maamuzi--

--huku unajua mahusiano yenu yalishashindwa, huku unajua kuna mtoto anakuja na hautaki mtoto alelewe pasipo baba na mama pamoja!!

Wanaume na wanawake tuna 50% shares kwenye changamoto ya ongezeko la single mothers!
 
Back
Top Bottom