Wanaume wengine ni hasara tu

Wanaume wengine ni hasara tu

dada yetu tulimsomesha wenyewe ajabu baada tu ya kupata ajira akaleta mpare moja nyumbani eti anataka kuolewa, sasa tangu aolewe hajui ATM inafananaje wala ina rangi gani jamaa kateka kadi ya Benk, na ata akishachukua hiyo salary yake hampi ata mia adi sister anatupigia cm kutuomba tumpige tafu, jamani kweli huu ni ungwana?
Hapana aweke wazi na alete mashtaka kwenu rasmi,hii sio haki kabisa,ila kiuwa na tahadhari upate maelezo toka pande zote!anaweza kuwa bado anatamani vijisenti vyenu hajui mna majukumu ya familia zenu,au
Mligawiwa urithi mkampiga chini anadai vyake kiaina!
Inabidi mambo yawe wazi msije mtuhumu shemeji yenu bure muulizeni hata kama mke wake hiyo sio haki.
 
Ndo maana tutawaita hao mabinti zetu nyumbani kwa ajili ya kusoma zaidi na liwalo na liwe;
 
hizo ndo zile ndoa unasikia mwanamke hadi mahari alijilipia na pete alijinunulia
 
Usiingilie mapenzi ya watu we mzushi ,tafuta wako nawe

kwani hapo anaingilia au anataka kupata uhalisia wa jambo? Afanyaje kwani ni dada yake mwenye ajira tena mwisho wa mwezi anapata salary halafu anaishia kupiga mizinga.
 
Dada yako ndio hasara!!!
Atawapigia mumpige tafu mpaka pesa ya underwear!!!!
 
Si msimupe tafu ndo atapata akili inaonyesha hana uchungu na hela mi husband ata senti asingeona
 
Kuna watu wana roho nzuri hii dunia acha tu
 
Huyo dada yako ---- na hamna kumpa msaada wowote.Kama anachukizwa na hali hiyo atarudi nyumbani yeye mwenyewe.
 
mmewe ndiye aliyemsomesha kwanini kadi ya benk ya ATM asiweze kumtunzia, pia yawezekana anamatumizi mabaya ya fedha kwa nini fatherhouse asichukue responsibility ya kumtunzia? Pia wanawake wengi hata wakiwa na kazi zao kuomba fedha ovyo ovyo nikawaida yao jamaa kaona amtunzie kadi ili amwombe hela vizuri kiharali ni HAYA TU WAZEE
 
Ni kweli sio haki lakini tambua hiyo ni ndoa na inasheria zake ktk maisha labda alegeze hiyoo sheria kwa mkewe.
😉
 
sio uungwana msimpe msaada akipiga simu dada yenu ili atie akili
 
Kama amenyang'anywa kimabavu sio kwa hiari yake mwambie aende Bank akaiblock account yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom