Wanaume Wengi Wenye Umri Kuanzia Miaka 30 Wamezaa Kabla ya Kuoa

Mimi kwangu huwa natambulisha kwanza watoto wangu, jamani eee nina watoto...11 enough. ukikubali sawa ukikataa sepa utakuwa umenipunguzia majanga.
 
ngoja nikwambie kisa cha dada mmoja hivi cha ukweli

huyu dada alisomaga boarding enzi zileee shule zikicheza disco usiku, miaka hiyo ilikuwa unakuta mtu unasoma ashira mnaenda ilboru kucheza mziki usiku asbh mnarudi shule. huyu dada siku moja ashira na ilboru waliendaga Momella kujipa raha, sasa kule momella walizunguka sana na ilipofika jioni disco likafunguliwa mida ya saa 2 hivi, basi bluzi za judy bucha enzi hizo


Ashira Idumu, Mungu ibariki, wabariki walimu pia na wanafunzi, Ashira izidi dumu milele......
 
Dah... Ni changamoto kwa kweli.

Mie kuna kaka mmoja hivi nafahamiana naye, aliishi na mwanamke.wa kwanza wakazaa naye watoto wawili bila kufunga ndoa.. Baadae akajapa pata tetesi kuwa mke anamfanyia mambo ya kishirikina wakaachana na akachukua watoto wake.

Hakuishia hapo akaanza uhusiano na mwanamke mwengine mara watoto hao wawili, wakashindwana na huyo mwanamke wakaacha....

Katika pitapita kampa mimba mwanamke mwingine mtoto wa 5 huyoooo hana ndoa visingizio kibao..... Akaachana na huyo mwanamke. mwishowe kabaki alone kwa muda. Si ndo akaja kwangu, ooh nataka ndoa nawe bla bla bla nyiiiingi.

Haya tupeane background, ooh nina watoto watano tena kwa wanawake tofauti, mweeeh nkaona huyu kimeo. Ina maana hao wanawake wote watatu watakuwa na matatizo!!!!

Oooh CL mie, sitaweza..... Nkampa black & white BADO NIPO NIPO SAAAAANAAAA!!!!!
 
Bora ufanye hivo na usitafsiri kila kinachoandikwa kama ndio hali ilivyo..Hizo ni assumptions zangu!!
Kaunyenyekevu naomba tutofautiane maana mtu anajua kitu anachofanya au alichokiona au alichosikia au kukisoma n.k. Hivyo andiko la mtu lina ukweli ndani yake. Ninapotetea hoja ni kuwa naiunga mkono ingawa unaweza kushabikia. Naomba kuishia hapa
 
Kuna wale (wanaume kwa wanawake) ambao wanakuwa wamezaa na watu mtaa wa kwanza au mkoa mwingine labda Kagera, baada ya hayo matukio wanahamia mitaa au mikoa mingine. Ukiwagusa kama wana watoto au la, wanakuambia khaaa, sina!

Baada ya kuoana na kuanza maisha, ghafla unaona watoto wamepakiwa kwenye bodaboda kama watatu hivi unaletewa! -@Mamndenyi na miss strong wanalijua hili vizuri wanaweza kulielezea.

Kutokujiamini ni ugonjwa mbaya sana............kuwa muwazi ni vizuri zaid na kama mtu amekupenda basi atapenda mpaka hao watoto wako na kama hawataki basi utajua ni hatua gani utachukua.
 
ngoja nikwambie kisa cha dada mmoja hivi cha ukweli

huyu dada alisomaga boarding enzi zileee shule zikicheza disco usiku, miaka hiyo ilikuwa unakuta mtu unasoma ashira mnaenda ilboru kucheza mziki usiku asbh mnarudi shule. huyu dada siku moja ashira na ilboru waliendaga Momella kujipa raha, sasa kule momella walizunguka sana na ilipofika jioni disco likafunguliwa mida ya saa 2 hivi, basi bluzi za judy bucha enzi hizo, wakadandiana mwishowe wakavunja amri.

binti baada ya muda tumbo hilo hamkumbuki hata baba manake walikutana siku moja tena disco, basi aliporudishwa home wazazi wake walimsaidia hadi akajifungua, akaacha mtoto nyumban akarudi shule kufanya mtihan wa form 4, uzuri alikuwa na akili aka make vizuri akagonga a-level fresh n akaenda chuo.

akiwa chuoni alikuwa akitongzwa tu na mwanaume anamwambia ukweli kwamba nina mtoto so akawa amejiweka huru kiasi fulan, ikatokea wanaume wawili wanampenda kwa dhati kabisaa na mmoja kati yao alikuwa ni lecturer, huyu mwingine alikuwa ni mwanafunzi mwenzie tuu lkn walipenda zaid hadi wakaoana. kuoana huyu kijana aliye mwoa alimwambia nataka mwanao aitwe ka jina langu, basi yule mtoto aliitwa kwa jina la huyu kijana na mpaka leo ni kijana mkubwa wa form six sasa. anaish nyumban kama watoto wengine waliozaliwa na huyu kaka.

kisa cha huyu dada huwa kinanifunza kwamba mtoto hana shida kabisa iwapo wazazi mtataka iwe hivyo ila mkileta komplikeshen ndipo mtakapo ipata joto ya jiwe.
Umejielezea vizuri!!pole na hongera kwa kufanikisha.
 
Jamani Spanerboy, don take mi wrong my bro!.
Sina roho mbaya hata kidogo!
Mimi naelewa haya mambo wala cjasimliwa.....
Ndo maana nimesema wanaoweza waolewe tu,ila mi cwezi, na wakaka mjitahidi kuoa mliozaa nao kupunguza tatizo

sawa sikulaumu sana kwasababu hata mimi sikubali mtoto ambae sio wangu aniite baba
 
kwa nini kuzaa zaa na kuachana, Kama hujaamua tumia condom, Endeleeni kuwakataa. Mimi mwenyewe ni me wa miaka 30 na sina mtoto. sihangaiki. We unaenda pekupeku wakati hujapanga kuwa na familia. tena siku hizi kila kona ni swala la uzazi wa mpango. we kijana mzima unazaa zaa tu, Nasisitiza wakataani ili nawengine wajirekebishe
 
Mkuu kuishi na mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa kuna changamoto zake kwa mtazamo wangu kijana mwenye mtoto inampasa aweke wazi kwa mwenzake toka mwanzo ili mtoto huyo aweze kupokelewa na mwenzi wako na kama akionyesha yeye hapendezwi na taarifa hiyo na hayuko tayari kuingia na wewe kwenye maisha ya ndoa basi bora ukaheshimu mtazamo wake. Ziko sababu nyingi nzuri/mbaya zinazoweza kumpelekea mtu kukataa au kukubari kuishi na mtoto wa nje ya ndoa. Hivyo baba aliejikuta ana mtoto nje inampasa awe na hekima na busara itakayomuwezesha kubalance issues hasa malezi ya mtoto huyo.
 
Kuna shemeji yangu huwa simuelewe...ana watoto 4 sasa hivi na binti anayekaa naye mpaka leo hakuna ndoa ni kama ali move in sababu ya mimba na any time ata mumuvuzisha out...anamwambiaga wakigombana arudi kwao. In short huyu dada naye ameenda pale kuongeza idadi ndio wamefika hao 4. Wa kwanza ni mkubwa sana alimzaa alipomaliza form six akamkataa mama mkwe kamchukua kamlea mwisho wa siku ame realize ni utoto ulomfanya amkane mwanae ambaye ni carbon copy

Nadhani ni katika kutafuta kuwa protect watoto wake hataki kukaa na mke...tunashindwa kabisa kumuelewa;

Hivyo nakubali inawezekana wanaume wenye watoto ni wagumu sana kuoa sababu ya woga wa mama wa kambo lakini si kwa sababu wanakataliwa...mabinti wanavyopenda ndoa ni wachache wenye jeuri ya kukataa kuolewa sababu kuna mtoto...ila watoto wako cha moto watakiona akishaingia ndani.

Na kweli bana huyo dada alozaa nae kwa sasa ana nyodo za kufa mtu hapo mkaka haja put a ring on it...akiolewa lazima watoto wa shemeji yangu washindie uji
 
Kuna shemeji yangu huwa simuelewe...ana watoto 4 sasa hivi na binti anayekaa naye mpaka leo hakuna ndoa ni kama ali move in sababu ya mimba na any time ata mumuvuzisha out...anamwambiaga wakigombana arudi kwao. In short huyu dada naye ameenda pale kuongeza idadi ndio wamefika hao 4. Wa kwanza ni mkubwa sana alimzaa alipomaliza form six akamkataa mama mkwe kamchukua kamlea mwisho wa siku ame realize ni utoto ulomfanya amkane mwanae ambaye ni carbon copy

Nadhani ni katika kutafuta kuwa protect watoto wake hataki kukaa na mke...tunashindwa kabisa kumuelewa;

Hivyo nakubali inawezekana wanaume wenye watoto ni wagumu sana kuoa sababu ya woga wa mama wa kambo lakini si kwa sababu wanakataliwa...mabinti wanavyopenda ndoa ni wachache wenye jeuri ya kukataa kuolewa sababu kuna mtoto...ila watoto wako cha moto watakiona akishaingia ndani.

Na kweli bana huyo dada alozaa nae kwa sasa ana nyodo za kufa mtu hapo mkaka haja put a ring on it...akiolewa lazima watoto wa shemeji yangu washindie uji
Huyo dada anafanya vibaya. Unajua wapo wanawake wenye tabia njema na wenye upendo wa mama mzazi kwa bahati mbaya nao hujikuta wanaishi na watoto jeuri . Tena baba akionyesha kuwa upande wa watoto basi lazima mama huyo cha moto akione. Pamoja na haya yote bado baba anapaswa kuwa na hekima ya kuishi nao wote kwa furaha na upendo. Mtoto abaki nafac yake na mama nae apewe nafac yake ila wamama wengine baba anapaswa kuwasimamia kwa akili. Kumbuka kuna baadhi ya watoto hufikia hatua ya kupewa ushirikina na mama zao ili wamdhuru mama aliyeko hapo home sasa kwa kuangalia haya yote hekima na maarifa vinahitajika sana.
 
Back
Top Bottom